Tukuiachana na mahubiri kupigwa marufuku kwenye mabasi ni kero gani nyingine zinazomkabiri abiria?

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
733
Tumesikia tamko la kiongozi wa latra akipiga marufuku mahubiri kwenye mabasi lakini sisi wananchi nadhani tunayafahamu mengi ambayo ni kero lakini kutokana na kutendeka kwa muda mwingi tukaona ndio utaratibu rasmi.

Wafanya biashara wa vinywaji na vitu vingine kurundikana kwenye korido za basi huku wakipishana kwa shida na kuwabudhi abiria.

Suala la kudaiwa na kukaguliwa tiketi Mara baada ya kuingia na kukaa kwa kutulia kwenye Basi, hapa kwanini wasiwe wakihakiki kabla mtu hajaingia ndani ya basi badala yake wamuache abiria aingie akae kwa utulivu kabisa halafu ndipo usumbufu wa kudaiwa uanze?

Suala la picha za video kwa maana ya miziki, filamu au series zinazo onyeshwa kwa sauti kubwa lakini bado baadhi ya hizo zikikosa maadili kabisa kwakuwa ndani ya gari moja kunaweza kuwa na wanafamilia wakisafiri kwa pamoja lakini ule mchanganyiko wa abiria wenye umri tofauti ambao wengine wamekaa siti moja . Suala la sauti kubwa wakati mwingine hata ukipigiwa simu huwezi kuongea ukaelewana na aliyekupigia simu kutokana na sauti za akina dj mark na akina mkojani

Baadhi ya wahudumu kuwa na kauli mbovu kwa abiria, yaani wale wahudumu wanamnyenyekea abiria akiwa kabla hajapanda gari Ila akisha panda wao wanageuka na kuwa wababe kwa abiria yaani ukitokea ukamuomba akushushe sehemu fulani unaweza ukajibiwa vibaya kisa tu eneo hilo si kituo pasipo kujali kama abiria ni mgeni eneo hilo ama lah. Hapa serikali itoe maelekezo kwamba ikitokea mtoa huduma akamnyanyasa abiria ni hatua gani zichukuliwe.

Kufaulishwa, hapa kumekuwa na kero kubwa sana yaani ukifika stendi unaweza kukuta kondakta anakuambia hii ni gari ya mwanza kumbe ni gari ya singida au tabora anajua atakufaulishia kituo gani. Pia unaweza pandishwa gari bovu wakijua halifiki safari kwamba mkifika sehemu fulani mtafaulishwa hapo kwenye kufaulishwa Kuna abiria kupoteza baadhi ya vitu lakini kubwa zaidi huwaga ni kupoteza muda wa kufika sehemu unakoenda. Hapa litolewe tamko Kali kuzuia.

Kuwekwa siti moja na abiria mwenye watoto zaidi ya mmoja ambao ni wakubwa au kuwekwa na siti moja na abiria mwenye maumbile ya unene uliopitiliza, hapa ni busara tu ya wahudumu wa basi ili tu kutoleta kero kwa abiria mwingine.

Ushauri:

Zile filamu, series na miziki vipitiwe na mamlaka ili ziruhusiwe kuonyeshwa ndani ya basi la abiria pia utolewe muongozo kuwa sauti ya mziki kwenye mabasi viishie volume ngapi ambapo kitaalamu haviwezi kuwa kero kwa abiria.

Zile maiki kwenye mabasi zitumike kutoa taarifa za maeneo husika mfano kama gari inatoka mkoa wa dar es salaam kuingia mkoa wa pwani basi mhudumu wa Basi awe na taarifa za vituo vyote ambapo Basi linaweza kushusha abiria lakini kuwe na briefing ya taarifa za mkoa husika juu ya tamaduni na shughuli za uchumi za mkoa husika hii itasaidia kuisogeza nchi kiuchumi kwani hizo taarifa zinaweza zikaibua fursa kwa baadhi ya abiria.

Nimemaliza
 
Tumesikia tamko la kiongozi wa latra akipiga marufuku mahubiri kwenye mabasi lakini sisi wananchi nadhani tunayafahamu mengi ambayo ni kero lakini kutokana na kutendeka kwa muda mwingi tukaona ndio utaratibu rasmi...
Zile movie na miziki kwenye basi imekua tatxo hawangalua inatakiwa iangaliwe na watu wa umri gsni...unakuta mtu upo ma watoto lakini wanachoonosha kina enda kinyume na umri ulioruhusiwa kuona
 
Tumesikia tamko la kiongozi wa latra akipiga marufuku mahubiri kwenye mabasi lakini sisi wananchi nadhani tunayafahamu mengi ambayo ni kero lakini kutokana na kutendeka kwa muda mwingi tukaona ndio utaratibu rasmi...
Binafsi nafikiri suala moja ndio nimekuwa nikiliona mara kwa mara likivumiliwa, kupanda na watoto wakubwa wasio na seat ... Ni kero sio tu kwa abiria na pia ni hatari kiusalama.

Nafikiri ni muda muafaka mabasi hasa yale ya daraja la kwanza na la pili ku up there standard na wafuate utaratibu wa mtoto above 2 years kuwa na seat yake kama kwenye ndege.

Hilo nimeona linavumiliwa si tu na wenye mabasi bali hata askari wa usalama barabarani
 
Wale wahubiri na wauza vipodozi vya ofa afadhali wametolewa

Pia hata customer service mbovu ya wahudumu huwa inanikera sana
 
Back
Top Bottom