Tukubaliane; Endapo Ripoti ya CAG kwa mwaka 2021/2022 itabaini dosari lazima viongozi wawajibike

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,076
7,647
Wananchi wamekuwa wakishuhudia kila mwaka Ripoti za CAG zikibaini ubadhirifu wa fedha za Serikali haswa ktk Halmashauri zetu na baadhi ya taasisi za umma.
ufujaji, ubadhirifu, wizi, upotevu n.k n.k.
Sasa tunashauri jambo moja;

1. Endapo Ripoti ya Ukaguzi ya mwaka wa 2021/2022 itabaini ubadhirifu, upotevu, wizi na ufisadi wa fedha za umma, tunaomba viongozi watendaji au wanao simamia wajiuzulu mara moja.

sisi wananchi tunachukizwa sana na ubadhirifu wa mara kwa mara unao jitokeza hivyo hatuko tayari tena kuona ubadhirifu ukitokea., na endapo utatokea basi viongozi wenye dhamana ya kusimamia mamlaka mbalimbali watapaswa wajiuzulu mara moja, na ikiwezekana watatakiwa wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Ripoti ya mwaka 2022 lazima iwe ni fundisho.
 
Kwani ubadhirifu ushatokea mara ngapi wewe!! Na ukitokea wewe kama wewe utafanya nini!! Endelea kulipa kodi na tozo zote acha kelele..wewe kazi yako ni kulipa kodi ili sisi wenye nchi tustarehe.
 
hii report ya mwisho ya CAG iliyoibua ufisadi wa kina Kigwangalla kuna hata kuku aliyewajibika????

wapumbavu hawatakaa wajue kwanini MaCCM hayataki mabadiliko ya katiba.
Pambafu.
 
Kauli na maelezo ya PM kuhusu wizi hazina nani alihukumiwa tena majina feki waliolipana.
Huyo CAG ameteuliwa na nani.
2021/2022 matumizi yatakuwa makubwa kuliko pato.
 
Ubadhirifu na ufunjwaji wa fedha za umma unao ibuliwa na Ripoti za CAG kila mwaka ni ushihidi wa viongozi wetu kuto kuwajibika ipasavyo ktk usimamizi.

Tunamuomba sana Waziri Mkuu awasimamie vilivyo walio chini yake, haswa Mawaziri, Mnaibu, wakuu wa Mikoa, Wolaya, Wakurugenzi, na wakuu wa Idara zingine.

Vivyo hivyo tunawaomba hao wanao simamiwa pia na wao watimize majukumu yao ya kuwasimamia walio chini yao.

Naamini kila mmoja akitimiza wajibu wake inavyo takiwa hakuna hata shilingi moja itaibiwa.

Tupunguze maneno mengi, tufanye vitendo,
pesa za umma haziitaji siasa bali vitendo,
viongozi wetu tuwe wakali kwenye fedha za umma.
 
Wakati mwingine hati chafu haina maana kuna wizi. Ni kukosa umakini kwa wahasibu na wakaguzi wa ndani, kwa mfano unafanya manunuzi bila kudai risiti
 
Ukiona tume imeagizwa ifanye uchunguzi halafu matokeo hayatangazwi ujue ufisadi uliwanufaisha viongozi au uchunguzi uliagizwa kwa kukurupuka.

Labda tuanze kujikumbusha maagizo ya PM majaliwa ambazo mpaka leo matokeo hayajatangazwa
1.Kuungua kwa Soko la kariakoo
2.ufisadi wa bandari ya Dsm
3.mradi wa mabasi ya haraka Dar.(BRT)

ongeza na wewe

1

1.
 
Wakati mwingine hati haina maana kuna wizi. Ni kukosa umakini kwa wahasibu na wakaguzi wa ndani, kwa mfano unafanya manunuzi bila kudai risiti
inawezekana ni kukosekana kwa umakini au kukosekana kwa weledi ktk sekta za fedha.
au inawezekana wamezoe kufanya kazi kwa mazoea.

Tunamuomba CAG na Kikosi chake wafanye Kazi zao kwa utaalamu wa hali ya juu na kwa uzalendo, kamwe wasimung'unye maneno ktk masilahi ya Taifa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom