Tukubali tusikubali wenzetu Kenya wanachanja mbuga, sisi na CCM yetu mmh !

Acha ubabaishaji ndugu yangu, watu wanahamia mijini kwa sababu huko vijijini hakukaliki kwa ugumu wa maisha. Jaribu kuachana na data za kupikwa ambazo ndio zimekuwa kama dira zinazoiongoza serikali yetu ya CCM. Nitakupa mfano;

Lakini hapo hapo wanaongezea;

Kwa lugha nyingine ni kuwa wakati wanadai uchumi unakua, umasikini uko pale pale kama si kuongezeka na watu wanaoumia zaidi ni wale wa kijijini.

Shamu unaongea kama vile huko vijijini hakuna tena watu wakati asilimia kubwa ya Watanzania karibu 80% tayari wanaishi huko huko. Sasa ni kwa nini hawa si matajiri ama kuna watu special ambao wamehamia mijini lakini kama wangekuwa vijijini wangefanikiwa katika kilimo na ufugaji, ni watu gani hao ? au hao waliokimbilia mjini kama ndio wanaosababisha umasikini vijijini - ni asilimia ngapi ?

Jamani tuache mzaha kwa mambo ya msingi - ardhi tunayo, watu tunao na tunachokosa ni uongozi bora kwa sababu CCM hivi sasa ni kama genge tu la wezi na wachumia tumbo, ukweli ambao hawako tayari kuupokea. Wako tayari kuwaua Watanzania wanaodai mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji nchi kuliko kukubali kuwa wamefikia upeo wao na kuachia madaraka - yamewashinda.



Umezungumzia vitu viwili, Economic inequalities na positive growth ktk uchumi. Sasa unapozumguzia uchumi wa nchi, uchumi wa nchi unakuwa vizuri, pamoja na data zako zinakubali.

Unapozumzia issue ya economic inequalities miongoni mwa WTZ hilo ndilo tatizo la free market. Ukiangalia ktk reply zilizopita tumeangalia hizo issues za inequalities. Kwanza, inequalities zipo ktk kila nchi. Ni jambo zuri? No. Tupo kwenye progress ya growth.
 
I'm talking about putting this valuable labour force into work. If you invite the chinese to come to Kiwira, that's fine. But when you allow their labor force to take the jobs which were supposed to be done by the local labor force that's not Nyerere's problem. The chinese or any other foreign investor are welcome to invest in Tanzania, but under certain terms and conditions which benefit wananchi too just like other countries are currently doing. But when you have bogus contracts that the current government is being tied up with these chinese investors then who's to blame? Are you gonna still blame Nyerere for this? pleaseeeeeeeeeeeeeee


Wachina wana tabia hiyo ktk kila nchi, lazima wafanye kazi zao wao wenyewe. Hata ile Tazara railways Wachina wallikuja kujenga kwa wingi.
 
You've got to be kidding me that Tanzania's inflation has been short term!
Tanzania has been under inflation during much of the recent past and is getting even worse. The cost of living, food prices, gasoline, energy and other basic needs continue to significantly raise on a daily basis while the wages have remained flat or with negligible increase, and that's why life has been very unkind to majority of common citizen. This is not misleading
To make the matter even worse, some services and products are being rendered/sold using the USD.

I did not know that you also have a negative view of the way CCM is leading this country; most of your posts have been praising CCM!!
 
I did not know that you also have a negative view of the way CCM is leading this country; most of your posts have been praising CCM!!

I don't belong to any party. I'm an independent/non-partisan citizen just trying to give the best for this country
 
Hiyo ndiyo issue inayokuja TZ, kwa sababu kila mtu anataka kukaa Dar, nani atakaelima vijijini? Unajua Free Market haiweleki miongoni mwa WTZ wengi. Kwa sababu WTZ wengi wanafikiri kwenye Free Market lazima wafanye kazi viwandani, maofisini, wakati si kweli. Unajua matajiri wakubwa ktk nchi kubwa zilizoendelea zenye kutumia system ya Free Market ni Wakulima. Ktk system ya Free Market kama unaishi vijijini na unaproduce food, mifugo unachance kubwa ya kuwa tajiri kuliko kukaa Dar kufanya kazi ofisini au viwandani.

Nilikuwa Mlali na Kipera Morogoro, nilshuhudia mkulima anauza tenga la nyanya kwa sh 3000 lakini anatakiwa alipe ada kama mtu anyeishi Dar au Arusha. Nilikuwa mpanda mkulima ameuza mahindi yake kwa bei ya sh 20,000 kwa gunia lakini mahitaji kama sukari yanalingana kwa bei na Dar.
Niliwauliza vijana kwanini wahamie mjini? jibu lilikuwa rahisi, rafiki zao wanaobeba lumbesa pale soko la mahindi wanapata sh 15,000 hadi 20,000 kwa siku, yaani bei ya matenga 5 ya nyanya yaliyotumia nguvu nyingi kwa miezi mingi.

My point is, watu hawahamii mijini kwa uzembe bali ni kutafuta unafuu wa maisha. Kama serikali yetu ingekuwa na mipango mahususi ya kuhakikisha mkulima anapata maisha bora kwanini mtu aje kuishi kwa dhiki ? Mfano mzuri ni pale tunapoagiza mahindi nje na kuacha ya Sumbawanga yanaoza sasa hapa unataka mkulima afanye nini. Kumbuka wengi wa wakulima si watu wa mitaji mikubwa na ukuaji wao unategemea mipango mizuri na si nguvu za kulima. Ma-settler wa nchi zilizoendelea wana uhakika wa masoko ya mazo yao, wana insurance kwa mambo kama ya hali ya hewa n.k.
Ukitembea vijijini na kuongea na watu utaelewa tatizo lipo wapi.
 
Ukingalia statistic data za GDP ya TZ utaona kwamba tuna positive growth, kwa hiyo uchumi wa nchi unakuwa.
Mimi nadhani uchumi wa nchi unaokuwa ni wa viongozi tu lakini kwa wananchi wa kawaida wenye hali duni uchumi wao unaporomoka kila siku na ugumu wa maisha unazidi kila iitwapo leo,mbona huo uchumi ambao viongozi wanatuambia unakuwa haumnufaishi mtu wa hali ya chini?
 
Kenya wanachanja mbuga kweli kweli, hapo walipo wanaendelea haswa! Sisi tumekalia Amani na utulivu!
 
Thamani ya hela SI kigezo cha kuwa na uchumi mzuri wa nchi. China wanaibeg hela yao isiwe na thamani ili waweze kuoffer cheap labor, na capital investments, nk.

Ithiwe na thamani na hela ipi? Shilingi au? unajua Yuan ngapi ni Dola moja?
By the way wao ni wazalishaji wanahaki ya kufanya hivyo zidi ya Dola,
Vipi sisi WACHUUZI?
kwanini waishusha?
kwa manufaa ya nani?
 
Thamani ya hela SI kigezo cha kuwa na uchumi mzuri wa nchi. China wanaibeg hela yao isiwe na thamani ili waweze kuoffer cheap labor, na capital investments, nk.

Very right mkuu. Ndiyo maana kila siku Marekani wanawalalamikia China kuhusu kushusha thamani ya sarafu yao maana kwa kufanya hivyo wanawafaidisha exporters wao na vile vilehiyo cheap labour ikilipwa kwa dola, conversion inawasaidia kupata fedha nyingi. Lakini wenzetu wanapaswa kufahamu kwamba, hata Kenya wanalalamika sana kuhusu kushuka kwa sarafu yao ambayo sasa imefikia shilingi 91/92 kwa dola moja, kutokashilinigi 76/77 chini ya mwaka mmoja uliopita. Kenya mpaka leo wabunge wamekuwa wakipinga kulipa kodi licha ya malalamiko ya wananchi wao na hilo la Musyoka limekuja baada ya Raila kuonyesha njia.
 
Back
Top Bottom