Tukubali tukatae Mwanaume kukosa utawala wa kiuchumi nyumbani heshima ya MUME hupungua kama sio kutoweka kabisa

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,392
4,468
Iwe ni kwa wale wa kipato cha juu kati au cha chini...yaani kama Mke anatengeneza shilingi mia tano kwa siku na wewe Bw Mkubwa ni apeche alolo, ni ngumu sana kuwa na ndoa imara ya Mume na Mke wanaosikilizana na kuheshimiana.

Huenda kwa nje mtafanikiwa kutuonesha kana kwamba ndoa yenu ipo imara ila bado kuna mengi tu Mwanaume atakuwa anayakosa...Mwanaume bila uhuru wa 'kiume' ndani ya nyumba ni adhabu tosha.

Pale ambapo Mama ndiye anaweka chakula mezani, analipa kodi ya chumba, ananunua madaftari na kalamu za Watoto..... na wewe bwana mkubwa kila siku unarudi na koti begani huna hata pee mfukoni ni mtihani mkubwa hata kama utanyamaza kimya.

Mbaya zaidi kwa zile ndoa mabazo Jamaa alizifumania za mkupuo mahali, akafanikiwa kumsomesha Mtoto Mkali aliyetimia, mlaini kama sufi....na mkafanya harusi moja ya kifahari iliyoacha gumzo mjini.....miaka mitatu baadae ile milioni 50 ndio imekatika, shughuli haziend na Marafiki wamepukutika, my friend usitarajie mambo yatabaki kama yalivyozoeleka...ni either Mzee baba uwe mvumilivu wa visa vya Mke, au umkimbie umuache kama sio yeye kufanya hivyo.

Mimi siungi mkono hii tabia ya kikatili ya kukatisha uhai wa Mtu mwingine kama njia ya kulipiza kisasi, muachane kwa amani au muachane kwa amani mtaonana Mungu akipenda....maana kiukweli kuna mambo yanaweza yakakukwaza mpaka ukatamani tu liwalo na liwe.
 
Tamati imekaa vizuri sana
 
Siku hizi kuna wanaume kama wanawake na wanawake kama wanaume kiutendaji, uwajibikaji na akili. Anyway WANAUME tuamke aiseee tutagongewa mpk utamu uishe
Ndio hicho ninachosema, ila kama Mwanaume umeridhia kulelewa bila shaka utakubaliana na kila kinachoamuliwa na Mke....ni sidhani kama ni sahihi kwa hii nayo kuiita ndoa rasmi.
 
Nahani kila kitu ni makubaliano tu.
 
Ukiwa na pesa 'mingi' unagongewa wife na dereva bajaji au bodaboda 'brazameni' mwenye 'chembechembe' za uhuni!

Ukiwa 'apeche alolo' nayo msala . ..

Kweli mapenzi ni 'sayansi'
Screenshot_20201008-201834_1602320417899.jpg
 
Maisha ya sasa baba ukiwa huna ramani jua kabisa upo karibu na kifo hata kama mkeo alikupenda kiasi gani!

Vituko vya mke vitakuondoa haraka sana kwa msongo wa mawazo. Hawajuagi kuelewa ugumu wa life hao.
Kabisa, ni vigumu sana eti umemuoa Mtoto aliyezoea good times, mwaka mmoja baadae uje umwambie 'tufunge mkanda'....walahi utabaki mwenyewe.
 
nimeona na haya mamb ya kukimbilia matako yanatuponza sanaa
Si mbaya ila uwe na uhakika kwamba uta maintain kipato chako kwa muda mrefu.

Mwanamke akisema nakupenda basi anamaanisha anapenda Wallet yako ilivyonona.
 
Tatizo liko hivi:-
Si kwamba Wanawake waaminifu na wenye mapenzi ya kweli hakuna, ila tatizo linaanzia haswa kwa Wanaume.

Mwanaume awayeyote hutamani kumpata Mwanamke mrembo kadri inavyowezekana kuwa ndani ya uwezo wake...na upande wa Wanawake nao huamini kuwa kama amejaaliwa urembo basi anastahili Mwanaume shujaa, na shujaa wa zama hizi tofauti na zamani ni Mwanaume mwenye uwezo wa kumuhudumia kwa kila kitu.

Hivyo inapotokea Mwanaume una fake kuwa na mali na baadae Mwanamke agundue kuwa huna uwezo ule uliokuwa unajinadi kwamba unao..sasa afanyeje? abaki kwako usiyeweza kutimiza ndoto zake akama ulivyojinadi au atoke atafute mwingine mwenye uwezo huo?.
 
Back
Top Bottom