Tukubali tu: Sisi wajinga... (I know, it hurts)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
BoT: We`ve no control over earnings by foreign firms

2008-05-09 09:20:15
By Patrick Kisembo

The central bank has said it has no control over the money foreign contractors generate in the country.

Bank of Tanzania Governor Prof. Benno Ndulu told a consultative meeting on Financial Management that it was difficult to control the income of foreign contractors as they won contracts as foreigners.

The meeting, organized by the Contractors Registration Board (CRB), was held in Dar es Salaam yesterday.
Prof. Ndulu said: ``If a company comes from Britain to work here at the end of the contract it will take back the money it has collected here,`` he said.

It is believed that foreign companies command more than 70 per cent of construction contracts in the country, a big chunk of whose earnings is remitted outside Tanzania.

Prof Ndulu said Tanzania would only manage to retain the remitted earnings when local contractors attain competence to compete equally with foreign firms.

Local contractors constitute about 97 per cent of all contractors in the country, although they garner only 30 per cent of the market share of the construction business.
The governor said the situation was disheartening for local contractors despite its importance and contribution to the national economy.

He cited lack of funding from financial institutions as one of the biggest challenges facing local contractors.
``This is due to the fact that most of the local contractors are small with no tract record and lack collateral to enable them access loans from financial institutions,`` he said.

Prof. Ndulu said the BoT had taken measures directed at reducing interest rates which were still very high following financial institutions` use of treasury bills rates as a benchmark to set interest rates to bank customers.

The governor said contractors would now benefit following the government`s move to embark on second generation financial reforms including putting in place the Lease Finance Act that would also enable contractors to acquire equipment on lease basis for construction purposes.

He said the government had prepared a bill to amend laws that hinder the development of mortgage finance in the country.

``We are currently administering, on behalf of the government, guarantee schemes which contractors can also utilize to access requisite financing from financial institutions,`` said Prof Ndulu.

CRB Registrar Boniface Muhegi admitted that foreign contractors benefited a lot owing to the fact that they were able to access finance, plant and machinery, as well as support, from their home countries or institutions.
 
mwkjj
Unajua ukikubali ukweli ndipo utapoona ujinga ukowapi na urekebishe kimtindo muafaka.

Mimi nakubali kabisa hadi sasa ninapoingia mitamboni SISI ni WAJINGA.
ukweli unauma lakini ndivyo tulivyo
 
Kweli, Kabisa, Sasa Tukianza Kufundishwa Kiingereza Tutakuwa Bora Zaidi Kidogo?
 
CRB Registrar Boniface Muhegi admitted that foreign contractors benefited a lot owing to the fact that they were able to access finance, plant and machinery, as well as support, from their home countries or institutions.
Mwanakijiji, thats why EU wataendelea kulisha familia zetu huku akina Mkulo wakikubaliana na ujinga huo. Wanajua wanachofanya kwani wanauhakika wa kutengeneza faida na ajira ya watu wao licha ya uchumi wao kuwa Stagnant!

Sidhani kama wahenga walikosea kusema "Wajinga ndio ...:confused:".
 
Kinachoniuma mm zaidi si ujinga wetu tu kwa sasa bali ni fact iliyopo kwamba ujinga utaendelea for centuries mpaka basi kwani hakuna juhudi zinazofanyika kuuondoa huo ujinga. Unlike other countries ambako uchumi ndio unaoendesha siasa hapa kwetu siasa ndizo zinazoendesha uchumi. So kila kitu kiinakuwa treated kisiasa. It's fun kwamba unachosikia toka kwa gavana ni completely different na utakachokisikia toka kwa waziri wake.I don't know ila inauma sana sana huko kwenye madini ndio usitake hata kusikia.
 
tanzania inaliwa kila kona, and the suprising thing is nobody who matters is doing anything about it!
 
Sasa ujinga huondoka; hivyo tusijisikie vibaya kwani katika kutambua ujinga wetu ndivyo tunavyotambua ni jinsi gani tunahitaji kujua zaidi (yaani kuondoa ujinga).

Nakumbuka vijitabu vya mfululizo wa "Ujinga wa Mwafrika", vilikuwa vinatumiwa sana na kina David Wakati na Khalid Ponera katika mazungumzo baada ya habari; lakini baadaye vilipigwa marufuku.

Nadhani wakati umefika wa kuvirudisha au nitaanzisha makala ya "ujinga wa Mtanzania"..
 
Mambo ya Tz ukuyasikia unawez kukosa usingizi yanaudhi sana, kama kweli tuna mwaziri wasomi wanaweka wapi usomi wao kwenye kusaini mikataba?? Can't they read and tell this is fishy?? au ndio wanakatiwa % ili waiue nchi? kwakweli inauma sana ndio maana wakatia mwingine watu wanafumba macho na kuziba masikio na kuisahau Tz sio kwa kupenda, its too painfull to bear what our country is going through, kwa manufaa ya majasusi wachache!!Inauma sana...
 
Lakini Huyo mjinga akierevuka,basi mwerevu yuko mashakani.

siku si nyingi busati lilotufunika litaisha kwa kuwa tumeanza kufunuka macho kutoka ktk ujinga baada ya kukanyagwa na kukaliwa sana.
 
Kibaya zaidi ni pale ambapo unajua kabisa hili ni jambo la kijinga, halafu unaendelea kulifanya na huyo mwingine anayejua wewe mjinga, na anajua kuwa unajijua kuwa mjinga, anaona kuwa Tanzania yuko paradise. Anafurahi sana kutuchezea.
 
Mambo ya Tz ukuyasikia unawez kukosa usingizi yanaudhi sana, kama kweli tuna mwaziri wasomi wanaweka wapi usomi wao kwenye kusaini mikataba?? Can't they read and tell this is fishy?? au ndio wanakatiwa % ili waiue nchi? kwakweli inauma sana ndio maana wakatia mwingine watu wanafumba macho na kuziba masikio na kuisahau Tz sio kwa kupenda, its too painfull to bear what our country is going through, kwa manufaa ya majasusi wachache!!Inauma sana...

Mashoo, I hear you!

Wakati mwingine inabidi uchukue days off na usisome kabisa JF kwa siku tatu hivi kwani unaweza kupasuka kwa hasira na uchungu.

Mara nyingi mimi huikimbia JF siku za weekend ili kusafisha kichwa kwani nikiendelea kupata habari kama hizi kila siku na kuendelea kuona hakuna kinachofanyika naweza kujikuta nimelaza kwa mshtuko wa moyo au nikajikuta nikiwapigia simu hit men wa kirussia watusaidie kupunguza mafisadi nchini (kitu ambacho sio plan yangu kabisaaaaa).
 
Hapana bwana wajinga ni hao tuliowakabidhi kuendesha vyombo vyetu lakini wamesalimu amri kwa hao wazungu.
 
KM, sasa tulipowakabidhi wajinga kuendesha vyombo vyetu kulitufanya sisi tuwe nani, wajinga zaidi? LOL
 
Ikulu: Tukimtaka Ballali tutampata

na Irene Mark

SERIKALI imesema haimtafuti aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali, ambaye mapema mwaka huu alifutwa kazi na Rais Jakaya Kikwete kutokana na kubainika kwa wizi wa mamilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema kuwa serikali ina mkono mrefu na iwapo itafikia hatua ya kumtafuta gavana huyo wa zamani wa BoT, haitashindwa kamwe kumfikia alipo.
Alisema kutokuwepo nchini kwa Ballali, au kutojulikana alipo, si jambo linaloisumbua serikali kwa sasa, kwa sababu hivi sasa yeye ni raia wa kawaida, hivyo anao uhuru wa kuishi popote anapopenda.
"Serikali haimtafuti Ballali (kwa sasa), lakini ikiamua kufanya hivyo haitashindwa. Kwanza ni private citizen (raia huru) siyo mwajiriwa wa serikali tena," alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa, mkono wa serikali ni mrefu hautashindwa kumpata Ballali iwapo itamhitaji.
Akifafanua zaidi, alisema baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wake, serikali iliunda timu ya kuwachunguza watuhumiwa wa EPA, kuhakikisha fedha zilizoibwa zinarudi na kuwachukulia hatua waliohusika, akiwemo Ballali.
Alisema: "Ninachofahamu ni kwamba, timu iliyopewa kazi kuhusu ubadhirifu wa EPA inaendelea na kazi yake na tunaona jinsi fedha zinavyorudishwa." Mkurugenzi huyo pia alikiri kwamba serikali haifahamu hospitali aliyokuwa akitibiwa Ballali, licha ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kukaririwa akisema alimtafuta Ballali bila mafanikio alipokuwa jijini Washington, Marekani.
"Kwa kweli sifahamu hasa Ballali alikuwa akitibiwa katika hospitali gani, lakini najua alikuwa nchini Marekani katika Jimbo la Boston, ila hospitali kwa kweli siijui.
"Lakini huyu ni mtu huru, hivyo anaweza kuishi popote… huyu ana nyumba yake nchini Marekani… yupo huko anaishi na familia yake," alisisitiza Rweyemamu katika ufafanuzi wake.
Alisema mafanikio ya timu inayochunguza suala la EPA yanaonekana, hivyo aliwaomba Watanzania kusubiri ripoti itakayotolewa baada ya kukamilika kwa kazi hiyo.
Hivi karibuni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye pia ni kiongozi wa timu hiyo, alibainisha kuwa kazi ya timu hiyo inafanyika kwa siri na kwamba zaidi ya sh bilioni 67 zilikuwa zimerejeshwa na kampuni zilizodaiwa kujichotea fedha hizo kutoka EPA.
Kwa upande wake, mjumbe wa timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, aliwahi kukaririwa akisema aina ya uchunguzi unaofanywa dhidi wa kampuni na wamiliki hao haitakiwi kuwataja watuhumiwa wanaorudisha fedha hizo hadi watakapohitimisha kazi yao.
Timu hiyo ina wajumbe watatu ikihusisha pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).
Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, baada ya taarifa ya uchunguzi wa hesabu uliofanywa na Kampuni ya Ukaguzi ya Ernst & Young na kubaini ubadhirifu wa zaidi ya sh bilioni 133.
Taarifa hiyo ilibaini kuwapo kwa kampuni hewa 22 zilizolipwa mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti hiyo kati ya mwaka 2005 na 2006.
Hata hivyo, ilibainika kwamba, baadhi ya kampuni hizo zilidanganya kuhusu usajili na wamiliki wake huku nyingine zikimilikiwa na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wengine wakitumia nyaraka za kughushi kuiba mabilioni hayo.
Mbali na udanganyifu huo,fedha za EPA zinadaiwa kusaidia kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Kutokana na kashfa hiyo na nyingine zilizoikumba serikali ya awamu ya nne, nchi wahisani na washirika wa maendeleo walitishia kusitisha misaada yao katika bajeti ya serikali.
Tishio hilo la wahisani ambao mchango wao kwenye bajeti ya serikali ni asilimia 43, liliifanya serikali kuwaangukia kwa kuchukua hatua za haraka katika mapambano dhidi ya ufisadi. Jitihada hizo za serikali zinaonekana kuzaa matunda kwani siku mbili zilizopita, wahisani hao wametangaza kuendelea kuchangia bajeti ya serikali baada ya kuridhishwa jinsi Rais Kikwete alivyoshughulikia suala la ufisadi nchini. Hata hivyo, uamuzi huo wa wahisani uliingia doa juzi baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe kuutuhumu hadharani Umoja wa Ulaya (EU) akisema uamuzi wao wa kurejesha misaada unaonyesha kwamba umekuwa na ajenda ya siri ya kulinda ufisadi kwa ushirikiano na serikali.

Kama na sisi tunakubaliana na hayo niliyo yahighlight then its definetly true?!
Na hayo yenye red ndio dangerous kabisaa!
 
Sasa ujinga huondoka; hivyo tusijisikie vibaya kwani katika kutambua ujinga wetu ndivyo tunavyotambua ni jinsi gani tunahitaji kujua zaidi (yaani kuondoa ujinga).

Nakumbuka vijitabu vya mfululizo wa "Ujinga wa Mwafrika", vilikuwa vinatumiwa sana na kina David Wakati na Khalid Ponera katika mazungumzo baada ya habari; lakini baadaye vilipigwa marufuku.

Nadhani wakati umefika wa kuvirudisha au nitaanzisha makala ya "ujinga wa Mtanzania"..

Mzee Mwanakijiji,

Hata mimi nakubali wa Tz tu wajinga sana.
Anyway tupo kwenye ka kikao flani nadhani umeelewa.
 
Naomba nifahamishwe, katika hili suala ni kipi kinachothibitisha ujinga wetu? Kuwa makampuni ya kigeni ndiyo yanayoshikilia sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi ambayo mara nyingi inafadhiliwa na kodi za wananchi wao? Au kuwa wanaremit faida wanayoipata? Au kuna jambo ambalo mimi sijalielewa!
 
BoT: We`ve no control over earnings by foreign firms

2008-05-09 09:20:15
By Patrick Kisembo

The central bank has said it has no control over the money foreign contractors generate in the country.

Bank of Tanzania Governor Prof. Benno Ndulu told a consultative meeting on Financial Management that it was difficult to control the income of foreign contractors as they won contracts as foreigners.

The meeting, organized by the Contractors Registration Board (CRB), was held in Dar es Salaam yesterday.
Prof. Ndulu said: ``If a company comes from Britain to work here at the end of the contract it will take back the money it has collected here,`` he said.

It is believed that foreign companies command more than 70 per cent of construction contracts in the country, a big chunk of whose earnings is remitted outside Tanzania.

Prof Ndulu said Tanzania would only manage to retain the remitted earnings when local contractors attain competence to compete equally with foreign firms.

Local contractors constitute about 97 per cent of all contractors in the country, although they garner only 30 per cent of the market share of the construction business.
The governor said the situation was disheartening for local contractors despite its importance and contribution to the national economy.

He cited lack of funding from financial institutions as one of the biggest challenges facing local contractors.
``This is due to the fact that most of the local contractors are small with no tract record and lack collateral to enable them access loans from financial institutions,`` he said.

Prof. Ndulu said the BoT had taken measures directed at reducing interest rates which were still very high following financial institutions` use of treasury bills rates as a benchmark to set interest rates to bank customers.

The governor said contractors would now benefit following the government`s move to embark on second generation financial reforms including putting in place the Lease Finance Act that would also enable contractors to acquire equipment on lease basis for construction purposes.

He said the government had prepared a bill to amend laws that hinder the development of mortgage finance in the country.

``We are currently administering, on behalf of the government, guarantee schemes which contractors can also utilize to access requisite financing from financial institutions,`` said Prof Ndulu.

CRB Registrar Boniface Muhegi admitted that foreign contractors benefited a lot owing to the fact that they were able to access finance, plant and machinery, as well as support, from their home countries or institutions.

UJINGA?
Mimi naona ni UKICHAA!
Kauli mbiu ambayo Obama anapenda kuitumia...Kwasababu ukichaa pia hupimwa kwa namna hii....
DOING THE SAME THINGS OVER AND OVER AGAIN EXPECTING DIFFERENT RESULTS=ELECTING THE SAME LEADERS OVER AND OVER AGAIN EXPECTING MAENDELEO!
 
KATIKA kauli ambazo zitawashitua watawala, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema nchi ina viongozi dhaifu, umma unanyonywa, rushwa imeongezeka, wezi wa fedha za EPA waanikwe na Rais Msitaafu, Benjamin Mkapa akajibu tuhuma zake mahakamani.
Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, Warioba amesema kuna dalili ya kuwapo watu wakubwa nyuma ya kashfa ya fedha zilizopotea katika sakata la EPA na kwamba yaliyotokea ni wizi wa hali ya juu na baadhi wameghushi na kwamba hatua za kisheria ni lazima zichukue mkondo wake.

26.jpg

JAJI Warioba

"Niliyosoma hasa kutokana na taarifa ile ya Serikali, ukiisoma kwa makini unaona kuwa haukuwa ununuzi wa madeni, huo ulikuwa ni wizi wa fedha za umma," anasema Jaji Warioba.
Anasema kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, baadhi ya madeni si madeni bali kuna watu wametumia ulaghai kuchukua madeni ambayo yamekwisha kulipwa na wao kufanya udanganyifu kuyadai.
"Wapo ambao wamefanya hivyo kwa kughushi. Sasa kuna makosa mawili hapo. Wizi na kughushi, ni makosa mazito, na kama nilivyosema wakati ule ilipotoka mara ya kwanza, ukiona makampuni ambayo yametajwa si makampuni makubwa na mengi yake yaliundwa kwa kazi hii tu," alisema katika mahojiano ambayo sehemu yake ya kwanza imechapishwa katika kurasa za 12 na 13 za toleo hili.
Akionyesha kuwapo kwa watu wakubwa nyuma ya wizi wa fedha za EPA, Warioba anasema biashara ya kununua madeni inataka mtu mwenye fedha na mwenye ujuzi wa biashara hiyo lakini makampuni yaliyoorodheshwa na serikali mengi yanamilikiwa na watu wa kawaida kabisa wasio na uwezo huo.
"Kampuni hizi ni ndogo, watu wenye kampuni hizi wameandikwa watu wenye majina ya kawaida. Kwa mtu yeyote mwenye busara atajua hii ni hadaa tu. Wanaoshughulika hawakujiandika kwenye kampuni hizi, wamechukua watu wengine tu. Kwa hiyo, kuna kazi, kuna kazi ya kuwatafuta hawa wazito waliokuwa wanahusika. Na kama ni wazito na wameingia katika wizi wa mali ya Taifa na kughushi, suala hili ni zito kuliko tunavyoliona," anasema na kuongeza;
"Mimi naamini kama kweli tunaishughulikia kwa nguvu zote, EPA ni kubwa kuliko Richmond, kuliko haya yaliyotokea. Kwa hiyo tutangojea matokeo. Na hapa kwa kuwa walau ushahidi wa kawaida upo, taarifa zinasema zile nyaraka zilizowezesha madeni hayo kununuliwa ni za kughushi, basi unaanzia hapo. Ukihakikisha kwamba ni za kughushi, kwamba haya madeni hayakuwapo, ukithibitisha kwamba hili deni halikuwapo sasa huyo aliyechukua fedha hizo alitumia wapi?"
Alisema akiwa kama raia mwema wa Tanzania anasubiri kwa makini kuona matokeo ya EPA, na kuongeza kwamba kama kweli nia ya kusafisha ipo, ni lazima waliofanya makosa wapatikane na kushughulikiwa na si wale waliotangulizwa.
"Mimi sijui utaratibu wanaotumia. Lakini kwa utaratibu wa kawaida, mimi nilikuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi, kwa suala hili la jinai unalishughulikia linakwenda mahakamani. Adhabu inatolewa pamoja na kurudisha hizo fedha, hilo ndilo nalitarajia," anasema.
Anasema kwa kawaida hatua za kisheria ni lazima zichukuliwe na kwamba unapokwenda mahakamani unaweza kutumia sheria kurudisha fedha zilizoibwa hata ikibidi kufilisi wahusika.
Hivi karibuni timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia waliochukua fedha za EPA ilieleza wazi kwamba imekua ikipokea fedha kutoka kwa watuhumiwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kuepuka kupoteza fedha hizo huku wanaozirejesha wakiendelea kuwa siri.
Timu hiyo ya Rais inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema, na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea, wote wakisaidiwa na maofisa kutoka ofisi zao na kutoka asasi nyingine za umma.
Akizungumzia kitendo cha viongozi hao wa juu wa dola kufanya mazungumzo na watuhumiwa, Jaji Warioba anasema; "Kwamba hawa ndio kweli viongozi wa ngazi ya juu wa vyombo vya dola vinavyoshughulika na uhalifu wanafanya kazi hiyo. Imani yangu ni kwamba hawatapinda sheria. Wakipinda sheria tutakuwa tumeleta madhara makubwa sana kwa nchi hii. Kwa sababu wananchi lazima kwa upande wa sheria waamini ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ni lazima waamini ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, lazima waamini ofisi ya TAKUKURU."
Warioba anasema watendaji hao wa dola wakipinda sheria, imani ya wananchi itapungua na hivyo ni jukumu lao ni kubwa, na kwamba yeye ana imani kwamba hawatapinda sheria.
Akizungumzia hali ya kisiasa ya nchi kutokana na kukwama kwa mambo mengi ikiwamo muafaka wa kisiasa Zanzibar na kuibuka kwa wimbi kubwa la tuhuma za ufisadi, Jaji Warioba anaonekana kutokua na imani na hali hiyo na anakiri kuwapo kwa udhaifu katika uongozi wa juu wa kitaifa.
"Kama nilivyosema, kila mtu ni kuzungumzia ufisadi, hata mafisadi wenyewe, maana ukiona wote hawa wanaozungumzia, huwezi kusema ni watu safi, pamoja na vyombo vya habari, navyo haviwezi kujisifu. Wengine wanaoandika juu ya ufisadi ndio hao hao waliokuwa wakichukua fedha za hawa, wanawaandika kuwa ni wazuri wakati wa uchaguzi. Walikuwa wakiwapamba. Kwa hiyo kuna wengine ni unafiki tu, ama ni ufisadi na wenyewe," anasema.
Warioba anapongeza juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari na wabunge katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini anaonya vita hiyo isitumike kufunika madhambi yaw engine ama kuwaumiza baadhi yao.
"Sina hakika kama wote wamezinduka hivi. Jana walikuwa wanasema hakuna rushwa, hakuna ufisadi. Leo ndiyo wako msitari wa mbele wanatafuta mafisadi na ukiangalia zaidi ni viongozi. Na hasa wabunge ndio wanaongoza vita hii. Ni vizuri Bunge liongoze lakini je, tunawaamini wote? Kwamba nia yao hasa ni kumaliza ufisadi au kuna sababu nyingine?
"Ikifika mahali tuwaulize hawa ambao sasa wanaonekana wana uchungu sana na ufisadi. Mwaka 2005 tuliona yaliyotokea. Hivi ni wangapi ambao wako safi? Mwananchi akimwuliza mbunge wake, na hii inawezekana kwa zaidi ya nusu ya wabunge, kwamba mbona wewe ulikuja na fedha nyingi sana kwenye uchaguzi na wewe si tajiri, ulizipata wapi?" anahoji Jaji Warioba.
Anasema wamo wengi ambao ni sehemu ya uongozi, na hivyo isije tokea mapambano ndani ya uongozi yakageuzwa kuwa ni vita ya kweli kumaliza ufisadi.
"Mimi nataka niwe na uhakika tukifika mwaka 2010 tuweze kuchagua viongozi safi, tusipate viongozi ambao katika mchakato wa uchaguzi watakwenda na takrima kwa sababu kama wanakwenda na takrima wamezipata fedha hizo kwa ufisadi," anasema.
Akizungumzia muafaka kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Jaji Wariona anasema tatizo kubwa ni mgawanyiko katika uongozi. Anasema wapo ambao hawataki muafaka wanaona njia ni kusema tupate maoni ya wananchi wakitarajia kwamba wananchi watakataa.

Kuhusu wanaotishia kurejea kwenye Afro Shirazi Party (ASP) kuliko kuingia katika Muafaka na CUF, Warioba anasema hivyo ni vitisho visivyo na maana katika mazingira ya sasa kwani hata wakiachwa hawana uwezo huo na kwamba tatizo kubwa ni udhaifu wa viongozi.
"Zaidi wanaosema warudi ASP ni watu wa Zanzibar, lakini nadhani pia kuna udhaifu katika viongozi Bara. Wakiisha kusikia madai hayo ya ASP, wanasema jamani waachieni mambo yao! Lakini haya si mambo yao, ni mambo ya nchi. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, likitokea tatizo Zanzibar ni tatizo la Tanzania. Hawa wanaosema waachieni haya ni mambo yao ni viongozi dhaifu," anasema na kuongeza;
"Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa. Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaumu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana. Manufaa ya Taifa sasa hivi ni kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Lolote linalohitajika kumaliza mpasuko huo ni vizuri viongozi wakachukua uamuzi, utakuwa ni mgumu lakini ni wajibu wao kuchukua uamuzi."
Pamoja na kuonekana kukwepa kumshutumu Rais Mstaafu Mkapa, Jaji Warioba anasema kinga waliyonayo viongozi akiwamo rais ni ya kisiasa tu, na hivyo kwake yeye suala la kinga ya kisheria si tatizo bali ukweli na uhakika wa tuhuma zinazomgusa kiongozi husika na kwamba ni mahakama inayoweza kutoa uamuzi wa haki.
"Nimeona wanaandika na nimeona mjadala mkubwa tu unaolenga kwenye immunity. Mimi nafikiri suala hilo si la msingi kwa sasa hivi. Na mjadala unalenga kwamba aseme, naona si la msingi. Kwa sababu hatutaki kwamba huyu awe tried na vyombo vya habari. Maana hapa naona kama ni trial kwenye vyombo vya habari.
"Waseme ni kosa gani, amefanya kwa msingi wa sheria gani, sasa waendelee. Sasa mengi wanayosema ni ya kisiasa. Yakisemwa ya kisiasa unataka mtu awajibike kisiasa. Kama ni kosa la jinai, waseme amevunja wapi sheria, lakini kusema kweli mimi sioni kwa vyombo vya habari kusema yote haya na wanachotaka ni kwamba ajitetee, ajitetee wao ndio wamekuwa Mahakama?" anahoji Jaji Warioba ambaye amewahi kufanya kazi kwa karibu na Mkapa.
Warioba anasema vyombo vya habari vinataka kuwa Mahakama na akashauri kwamba kama kuna kosa alilofanya Mkapa ni vyema wakasubiri afikishwe mahakamani ambako atakuwa na nafasi ya kujitetea na kueleza upande wake.
"Immunity nasema sasa hivi siyo issue. Sema kosa lililotendeka. Anashitakiwa lakini wanasema hatuwezi kuendelea kwa sababu kuna immunity. Bila kusema kosa huwezi kufika kwenye immunity. Huwezi kuanza na immunity bila kuwa na kosa, kwa hiyo mimi sitaki kujiingiza katika mjadala wa immunity. Hii ni ya kisiasa tu," anasema.

KWANINI KABLA HATUJA CONCLUDE KUWA SISI NI WAJINGA TUSI ZINGATIE HAYA YA ALIYEWAHI KUWA MWANASHERIA MKUU..JAJI SINDE WARIOBA NA WENGINEO?
UJINGA UKO KWENYE UTAMBUZI WA VIONGOZI WAZALENDO?
progress.gif
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom