Tukubali Mwendokasi imewashinda rudisheni daladala zetu

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
wana jf,

Wasafiri wote wanaotumia mwendo kasi shida ya kukosa usafiri imezidi kipimo, unakaa kituoni saa nzima. Tunajua wanaohumia ni wale wanaooitwa wanyonge, kila siku kilio cha mwendo kasi hakitatuliwi, basi kama serikali imeshindwa iturudishie daladala zetu mpaka apo watakapokuwa tayari lakini si kwa mateso haya. Mwanzoni tulifurahi sana ujio wa hii huduma sasa ni mateso sana,

kama kuna waziri mwenye zamana apeleke bungeni mabadiliko ya dharula kwa kuomba kurudisha njia za dala dala kwa muda mapa uwatakapokuwa wameleta mabasi ya kutosha.
 
Hili duduwasha linawapa mapato makubwa. Sio rahisi kilio chako kikasikilizwa. Hii ni Zama ya makusanyo zaidi huduma sio kipaumbele.
aisee sasa tutaendelea kuumia na kuambukizana magonjwa , kuibiana maana si kwa kujaza huku, hata hivyo hata milango wanatengeneza kila siku maana wananchi wanaibomoa kwa kujaza kupita kiasi
 
Sio swala la kurudisha daladalA..

Weka wewe points zako unaona Nini kifanyike kutatua tatizo,serikali imeshatumia kodi zetu nyingi sn kwa project hiyo kusema imetushinda Ni kusema hamna mawazo mbadala na usiniambie we ndo msomi hapo na umesomeshwa na serikali..

Unapokuwa na lawama tu bila kutoa solution na hiyo ikawa ndo tabia yako Basi unajiandaa kuwa loser,loser kwa familia yako,loser kwa wenyewe na loser kwa nchi yako. Mmeenda shule kuja kutatua matatizo ya jamii sio kulalamika.
 
Ndio waleeeeee
 
Cha ajabu pale Kituo cha gerezani gari nyingi zimepark ati ni mbovu! Sasa Kwa mwenendo huu baada ya miezi 6 si zitakua zimeisha zote?
 
Sio swala la kurudisha daladalA..

Weka wewe points zako unaona Nini kifanyike kutatua tatizo,serikali imeshatumia kodi zetu nyingi sn kwa project hiyo kusema imetushinda Ni kusema hamna mawazo mbadala na usiniambie we ndo msomi hapo na umesomeshwa na serikali..

Unapokuwa na lawama tu bila kutoa solution na hiyo ikawa ndo tabia yako Basi unajiandaa kuwa loser,loser kwa familia yako,loser kwa wenyewe na loser kwa nchi yako. Mmeenda shule kuja kutatua matatizo ya jamii sio kulalamika.
unaishaurije serikali iliyopaki mabasi mengi eti mabovu, siku za mvua wanayaacha ,makusudi yanalowekwa hadi hata engine
 
Kugoma ni mpango mzuri Sana kufikisha ujumbe. Hayo magari yao mabovu mabovu.
 
Sijui kama watakusikia
Wenzako waendeshwa na mavi8
Full mufindi,foleni ikitokea wanaitumia barabara hyo ya mwendokasi wawahi sehemu zao!
We vumilia tu

Ova
 
Inatakiwa zianzishwe ruti mpya... Mfano kuna bara bara pale Kimara nadhani Korogwe, karibu na kanisa la KKKT Kimara, ile barabara inatokea Tabata Kimanga... Inaweza kuanzishwa route ya dala dala za kutoka pale Kimara kwenda Kimanga, then from there watu wakapata gari za kwenda Mnazi Mmoja na sehemu nyingine za mjini. Pia nyingine inaweza kuanzia Ubungo Makoka hadi Kimanga... Nyingine pia inaweza kuanzia Kimara Mwisho ikapitia Tabata Kisukuru hadi Segerea ambapo hapo wasafiri wanaweza kuunganisha kwa kupata dala dala za kwenda Mnazi mmoja na maeneo mengine.
Kwa sasa bara bara ya mwendo kasi 'imelemewa'. Hii inatokana na ufinyu wa magari ya mwendo kasi...

Pia sasa, its a time serikali inabidi iongeze juhudi ya kuweka lami bara bara zinazounganisha Kimara na upande wa Tabata na pia zile zinazounganisha Kimara na upande wa Makoka.
Kuna mmoja nimemsikia leo akilalamikia bara bara ya kwenda Makabe huko na Mbezi Msumi... Kwa kweli eneo hili la jiji liko nyuma kimiuondombinu ya bara bara...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom