Teamo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2009
- 12,272
- 1,034
SOURCE:SAUTI TA WATU TANZANIA DAIMA-salehe moohamed
MWANZONI mwa wiki hii, Rais Jakaya Kikwete, aliamua kumfukuza kazi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali, kwa kosa la kuwachapa viboko walimu wa shule za msingi, ambao shule zao hazikufaulisha wanafunzi wengi kuingia shule za sekondari.
Binafsi sikukipenda kitendo alichokifanya mkuu huyo wa wilaya, kwa kuwa kiliwadhalilisha walimu lakini pia alitoa adhabu bila ya kuangalia mazingira magumu wanayofanyia kazi walimu hapa nchini.
Tuangalie upande wa pili wa shilingi, hivi ni kweli DC yule alifanya kitendo kile kwa kuwa anawachukia walimu au kwa kuwa aliudhika na matokeo mabovu ya wanafunzi ambao tunaamini ndio taifa la kesho na wanahitaji elimu bora ili waweze kukabiliana na changamoto za dunia kwa lengo la kuikwamua nchi kiuchumi.
Pamoja na kutokubalina na uamuzi aliouchukua DC huyo lakini nampongeza kwa kuwa mbunifu wa adhabu inayofaa kwa watu wasiotenda kazi kwa ufanisi unaotakiwa katika jamii, hasa wale ambao sekta zao zinaonekana kuwa na mazingira mazuri ya utendaji kazi.
Mfumo huu kama ukianza kutumika, watendaji wa halmashauri, mkoa na wizara nina hakika utakuwa mzuri kwa kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, tena kwa kuendekeza urasimu ili mradi yule ambaye anatakiwa kupata huduma asiweze kuipata kwa muda unaotakiwa na ikiwezekana atoe rushwa ili ahudumiwe.
Leo hii askari wa usalama wa barabarani kila kukicha wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya rushwa kwa kuyaachia mabasi makubwa na daladala kuvunja sheria mbalimbali za barabarani, ambazo mwisho wake ni ajali na vifo vya watu wasio na hatia.
Hawa tukiwachapa viboko kwa uzembe wao hatutakuwa na tatizo na tena kama ikiwezekana wachapwe mbele ya vyombo vya habari ili kesho na wengine wenye nia ya kufanya makosa hayo wasiweze kuyafanya ili kukwepa kudhalilishwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwemo kufukuzwa kazi.
Baada ya hapo tuhamie kwa watendaji wa wizara ambao muda mwingi hukaa na kubuni mbinu za kufuja rasilimali za taifa bila kujali wizi huo huathiri wananchi, hasa kwa kukosa huduma za kijamii kama vile maji, umeme, dawa zahanati na nyinginezo.
Hawa wamekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya taifa ambapo wakati mwingine wamekuwa wakiingia mikataba mbalimbali kwa lengo la kujipatia asilimia 10 ten pacent ili hali wakijua kabisa wawekezaji hao hawana uwezo wa kuendesha mradi husika au mwekezaji husika ana lengo la kuinufaisha zaidi nchi anayotoka.
Ni aibu leo hii mwekezaji wa hoteli kuajiri mpaka mfagiaji kutoka nje ilhali Watanzania wapo wengi, wengine huagiza hata nyanya, vitunguu, kuku na bidhaa nyinginezo kutoka nchi za nje ilhali Iringa, Mbeya, Morogoro na mikoa mingine inazalisha kwa wingi bidhaa hizo mpaka nyingine zinaozea mashambani.
Viboko wanastahili watendaji hawa na wala si walimu ambao kuanzia malazi, chakula, mishahara na huduma za jamii huzipata kwa kiwango duni kulinganisha na wanasiasa ambao wamekuwa mstari wa mbele kuandaa na kutetea masilahi manono wawapo ndani na nje ya Bunge.
Wakati mwingine ili binadamu aweze kujifunza ni lazima yatokee makosa na atokee mtu wa kuyasahihisha makosa hayo, DC Mnali ametuonyesha njia, si vibaya na sisi kuangalia utaratibu huu ambao nina imani ipo siku tutaanza kuwachapa na viongozi wa ngazi za juu.
Nitafurahi zaidi pale rais atakapochapwa viboko hadharani kwa kosa la kutotimiza ahadi yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania kama alivyoahidi katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2005.
Si kila mtu ni shuhuda wa hayo maisha yaliyoahidiwa kama yametimia? Leo hii maisha yamezidi kudorora na hata yule aliyekuwa na uwezo wa kununua fungu la dagaa hivi sasa hana tena uwezo wa kununua kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Tukimaliza kumchapa viboko rais tuhamie kwa mawaziri wake ambao nao wamekuwa mzigo mkubwa kwa taifa kuliko hata kile wanachokizalisha, hasa kwa kushindwa kufanya mambo mbalimbali yenye tija kwa nchi na badala yake wamekuwa wakijilimbikizia mali kiasi ya kuonekana ni wafanyabiashara, badala ya watoa huduma kwa jamii.
Leo hii waziri amekuwa mfalme na mwananchi wamegeuzwa kuwa mtwana wakati mwananchi ndiye ambaye anapaswa kuhudumiwa (mfalme), huu ni udhaifu na kama tusipochapana viboko hatutaweza kubadilika.
Kwa nini tusiwachape watendaji wa baraza la mitihani la taifa ambao kwa miaka kadhaa hivi sasa wamekuwa wakidaiwa kuvujisha mitihani pamoja na kuuza baadhi ya vyeti kwa watu wasiohitimu elimu husika au kupata alama ndogo katika mitihani yao ya mwisho.
Mbona hatuwachapi viboko wahadhiri wa vyuo vyetu ambao hutoa shahada kwa wahitimu wa vyuo baada ya kupewa rushwa ya ngono au fedha, hawa si ndio hatari kwa maendeleo ya taifa kuliko hata ugonjwa wa ukimwi?
Hawa wanastahili viboko, tena vya mkia wa taa, athari ya kuwa na wataalamu wenye elimu bandia ni kubwa zaidi katika sekta ya uchumi, afya elimu na nyinginezo kuliko hata huku kumfukuza DC aliyejaribu kuweka historia katika jamii kwa kuwacharaza viboko walimu ambao kwake aliona kutofika kazini mapema ni moja ya sababu zilizowakwamisha wanafunzi kufaulu.