Tukubali kuwatetea wazanzibar wanaoishi Tanganyika kwa kuiuwa Zanzibar kumezwa na muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukubali kuwatetea wazanzibar wanaoishi Tanganyika kwa kuiuwa Zanzibar kumezwa na muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 16, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Mimi hushangazwa sana na viongozi wetu wa Smz kusema kuwa Muungano ukivunjika Wazanzibar waloko Tanganyika waatapata tabu.

  Viongozi wenye mawazo haya hawafai kabisa kuwa viongozi wa Serekali ya watu wa Zanzibar na nizaaifu kiuongozi.

  Hivi kweli tukubali kuwatetea Wale waloko ugenini huku wandani ya nchi na nchi yao ikipotea kwa visingizio visivyo na Machiko? Maneno haya yamezoweleka na hata kufika hadi viongozi wa Tanganyika kuona ndio kisingizio cha kulinda Muungano na kutula kwa matonge.

  Hivi kweli inaingia akilini kuza nchi yetu kwa kisingizio cha wenzetu waloko ugenini au viongozi kuekeza Tanganyika na kuwa na nyumba kule?

  Mimi nahisi hichi sio kigezo sahihi cha kuto kulivua hili Jindamizi la Muungano kwa kisingizio cha kiongozi kaekeza miradi yake kule au Wazanzibar wenye kuishi kule, kwani chakujiuliza wenye kuishi Tanganyika ni Wazanzibar tu ndio wageni wa Muungano?.

  Jee Muungano ukivunjika ni Wazanzibar tu ndio walengwa, kuna nchi nyingi ziliungana na bada ya kuona Muungano haukizi mahitajio yao na kuamua kuuvunja, mfano Senegali/Gambia, Syria/Egypt, Cheko/Slovakia, South Korea/North Korea etc.

  Jee wachina, Wahindi, Walebanoni, Wasouthafrica, Wazambia na nchi jirani za Bara la Tanganyika Muungano ukivunjika hao vipi? Kwani kuna tatizo gani Wazanzibar kuishi Tanganyika na kufuataa sheria zote kama vile wageni wengine wachina na wengine walio Pakana na Tanganyika?.

  Ikiwa viongozi wa Tanganyika wamekuwa wakitumia kigezo na ngao ya Kuvunjika kwa Muungano na Wazanzibar waloko Tanganyika, jee nyuma ya upande wa shilingi tukibiruza Watanganyika waloko Zanzibar vipi?

  Nashindwa kuona viongozi wa Smz wakijizalilisha kwa kusema Wazanzibar walioko Tanganyika tu na kusahau Watanganyika waloko Zanzibar.

  Tuangalie Faida na hasara za Wazanzibar walioko Tanganyika na Watanganyika waloko Zanzibar pindipo Muungano ukivunjika.

  Wazanzibar walioko Tanganyika wengi wao ni wafanya biashara na wanaingiza pato kubwa katika Serekali ya Tanganyika kwa kulipa kodi.

  Sasa tuangalie Watanganyika na biashara zao za Karanga, Dawa ya Panya na biashaza nyengi wazifanyazo Zanzibar zinaingiza pato gani katika Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar?.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa taarifa yako Watanganyika walioko Zanzibar ni wachache kulinganishwa na Wazanzibari walioko bara. Tafakari.
   
 3. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Zanzibar kuna viongozi au makanjanja, wachumia tumbo?
   
 4. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,110
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  kama nyinyi hamuwataki watu wa bara kwanini mtulazimishe na sisi tukae na wazanzibar kwani hizo bar mnazochoma moto mnajua zinaingiza kodi kiasi gani kama wazanzibar wanaoishi bara wanachangia kodi kubwa ni heri warudi kwao ili waijenge nchi yao.Nyinyi ni sawasawa na mtu anayeendesha gari halafu likamgonga mwenyewe muungano una mazuri na mabaya yake lakini tukiyaweka kwenye mizani kuna mazuri zaidi kuliko mabaya nyinyi anzeni sisi tutamaliza
   
 5. J

  John W. Mlacha Verified User

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  mke anaililia talaka
   
 6. Ukoo Flani

  Ukoo Flani Senior Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani eeeeeeh si mtoke tu kwenye huo Muungano kwani mmefungwa minyororo na watanganyika? Kila siku wimbo uleule zanzibaaar zanzibaaaarr hadi na wenyewe umekuwa Kero nyingine ya Muungano. Waambieni akina Dr. Bilal waachie nyadhifa zao kwenye Serikali ya Muungano warudi huko muijenge nchi yenu. Hakuna mantiki yoyote kuendelea kuwatukana watanganyika ambao zaidi ya 75% hawajawahi kukanyaga ardhi ya Zanzibar na wala hawafaidiki kwa namna yoyote ile na aina hii ya Muungano. Wakomalieni viongozi wenu mjitoe hata kesho.
   
 7. angedizzle

  angedizzle JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 560
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 80
  ndo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia?,aliekwambia wa-bara tunautaka muungano nani?.......mkafie mbele,eboooo
   
 8. Ukoo Flani

  Ukoo Flani Senior Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hahhah, naona mdau alikuja kuPost tu!
   
Loading...