leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,585
- 3,179
Nilishituka sana niliposikia Rais Magufuli amemteua mkuu wa wilaya ya Arumeru kuwa mkuu wa mkoa na jambo hili likanifanya nikumbuke maswahibu yaliyo mpata
rais Trunp wa Marekani hivi karibuni alipogubikwa na lawama kutoka kila kona ya nchi ya Marekani, kisa alishindwa kuonyesha heshima alipopiga simu kumpa pole mke wa mwanajeshi wa marekani aliefia afrika kwenye kikosi cha kurinda amani cha UN.
Tunajifunza nini sisi watanzania kutokana na mkasa huo:-
Hakika watanzania hatutaiepuka dhambi ya unafki uliotukuka.
Tumeiacha hadhi na heshima ya nchi kutwezwa huku tukijificha nyuma ya kichaka cha unafiki wa kuiheshimu taasisi ya rais, vyama vya siasa na chuki binafsi,na sio ajabu tukaona watu wanatetea tendo hili.

- Wamarekani hawamkopeshi Rais wala hawamuonei haya kumwambia ukweli anapomkosea hata raia mmoja tu wa marekani.
- Vyombo vyote vya habari duniani vililipoti taarifa hii vikiwemo vya serikari kama VOA bila kujificha nyuma ya unafki ili kulinda hadhi na heshima ya taifa la Marekani.
- Dhamana ya urais wa USA haiko juu ya haki za raia wa marekani.
- Heshima, haki na utu wa raia wa marekani hauwezi kutwezwa au kuingiliwa na taasisi au mtu yeyote yule.
- Hakuna mtu ama taasisi iliyomtetea rais katika hili ilimbidi ajitetee binafsi kama Trump.
- Wanajua kutenganisha baina ya taasisi ya urais na mtu binafsi kama Trump tofauti na Tanzania ambapo hakuna tofauti kati ya taasisi ya urais na Magufuli kama mtu binafsi.
- kitendo cha kuizuia taasisi ya kupambana rushwa kuendelea na uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa.
- Kumwepusha mtuhumiwa na adhabu inayoweza kumkabili endapo tuhuma dhidi yake zitathibitishwa.
- Kujaribu kufifisha uzito wa makosa ya mtuhumiwa.
- Kukiri kwa mtuhumiwa kujihusisha na alichokiita kununua wapinza na kuwa bado ataendelea kufanya hivyo ni kujaribu kufifisha kosa la rushwa lakini pia ni ujumbe wa dharau dhidi ya raia wa Tanzania.
- Dalili ya wazi kutangazwa kwa tabaka la raia wasioguswa na sheria.