Elections 2015 Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?

Vita vinaendelea, nimesikia wapiganaji wamekubali kuweka silaha chini na kumsusia ngedere shamba la mahindi.

Jee tutafika?.

Pascal
 
Vita vinaendelea, nimesikia wapiganaji wamekubali kuweka silaha chini na kumsusia ngedere shamba la mahindi.

Jee tutafika?.

Pascal
Very sad ....wanaposusa tena kwenye ubunge ndio wanasaidia uumaliza upinzani ...tunarudi tulikotoka while tulishapiga hatua kubwa sana ...
 
Vita vinaendelea, nimesikia wapiganaji wamekubali kuweka silaha chini na kumsusia ngedere shamba la mahindi.

Jee tutafika?.

Pascal
Njia pekee iliyosalia ni chadema kwenda haraka kufungua kesi kwenye mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague na endapo chadema hawatafanya hivyo wajue moja kwa moja wanapotea watakuwa kama TLP na NCCR kisha Msajili ataifuta milele na CCM kurejesha mfumo wa chama kimoja.
 
Kwa hili la Max, JF iko vitani. Serikali ya Magufuli kupitia waziri wake ambaye ni mwana JF, mwenzetu, Mhe.Mwigulu Nchemba, na mwana JF mwingine kwa jina la TCRA, wametangaza vita na JF.

Zingatia angalizo hili muhimu.

Paskali
njia za kudai Uhuru ni kwenda UN, pia kwenda kwenye Taasisi za haki za binadamu haki za Uhuru wa Habari za kimataifa, mahakama za kimataifa huko ndipo watapaza Sauti na kuwazindua Mtukufu malaika toka na Naibu Rais Maliyamungu Bashite waache Udikteta wao na kurejesha umoja wa kitaifa ambao inaelekea kubaya zaidi.
 
Mkuu Danny, nakubaliana na wewe, dawa ya adui sii kumkimbia au kumpisha bali kukabiliana nae, na hata kama utaangamia katika kukabiliana huko, na kupoteza maisha, jina lako ndilo litabaki kama shujaa, cha muhimu cha kujiuliza, ni nani muhimu zaidi kati ya shujaa mfu, au mfungwa hai aliye gerezani?!, au aliyejificha mwituni?!.

Kwa maoni yangu, kama unakiona kifo kile, halafu unakikimbilia na kufa tuu ili uonekane shujaa, wewe ni shujaa mjinga!. Kama unataka kushindana au kupigana na mtu mwenye nguvu zaidi yako, hivyo unaingia kwenye mapambano ili hali unajua utawawa, wewe pia ni shujaa mjinga!. Shujaa mwerevu ni yule ambaye hawezi kuingia kwenye vita ambayo anajua atashindwa!, bali atampisha huyo mwenye nguvu, huku yeye akijijenga mpaka awe na nguvu za kukabiliana na kushinda!.

Naomba take time kasome bandiko langu hili, utanielewa ninamaanisha nini
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na ...

Pasco
Tanzania ni mwanachama wa UN na huko wana vitengo vya kudhibiti serikali za kidikteta na serikali zibazofanya mambo yanayokiuka haki za binadamu ni kwa nini chadema na Wapinzani wanaogopa kwenda huko?
 
Chadema na Wapinzani kwa ujumla wasipotumia unyanyasaji huu wa sasa kuishitaki serikali ya Awamu ya Tano kwenye mahakama za uhalifu wa kimataifa na jumuia za haki za binadamu mapema wapewe haki zao watambue kuwa mwaka 2020 hakutakuwa na Mbunge wa chadema atarejea bungeni tena, kuanzia mwaka 2020 serikali ya Tanzania itakuwa kama China ni mwendo wa mfumo wa chama kimoja mpaka milele na Msajili anajiandaa kuvifuta vyama vyote vya upinzani.
 
Kuna jamaa yangu fulani mimi nilimdhania ni mpigaji shupavu!, lakini leo nimeshangazwa amebwaga manyanga na kuikimbia vita!. Wapiganaji shupavu, hupigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike!, leo imekuweje tena?!. Nasikia sikia, nasubiria kusikia kwa masikio yangu mwenyewe!.

Pasco
Kuna mamluki wengi wapo CCM baada ya kununuliwa na kile kikundi cha Naibu Rais Maliyamungu Bashite huko baadae watasaidia kutoa taarifa kwa chadema na upinzani kwa ujumla lakini endapo CCM hawatafanya kama walivyopanga kufanya sasa ambapo Msajili anajipanga kuvifuta vyama vya upinzani huku mwaka 2020 wakitaka wabunge wote wawe wa CCM pekee Nchi iwe ya chama kimoja kama China na Rais atawale milele na milele kama China na Burundi
 
Ushauri kwa ndugu yangu Mayalla ukitwa kwa kuhojiwa, kaa kimya usijibu maswali ukubali kuomba radhi maana ukipambana na nguvu usyoiweza hiyo itakuwa unacommit suicide na binadamu mwenye akili hachukui suicidal stand.
Mkuu Muyovozi, kwanza asante kwa ushauri huu, mimi niko kwenye hili Kundi hapa chini, hivyo kuitwa tuu Dodoma ni vita kati ya uhuru wa kujieleza na vitisho kutoka mhimili wa dola, hivyo nasubiri barua rasmi nijipange, na utetezi wangu utakuwa na sentensi tatu tuu, "Yote yaliyosemwa ni kweli, nimekubali makosa, naomba mnisamehe!", ukiishakiri kosa, kinachofuatia ni hukumu, hivyo nitakwenda kwa ajili ya kuhukumiwa na sio kubishana na Bunge!.
Wanabodi
Siasa za Tanzania ni kizungumkuti!. Ni siasa za ubabe, uongo, chuki, fitna na kukomoana badala ya kuleta maendeleo. Chama tawala CCM ni chama dola, hivyo kinatumia uchama tawala wake kwa kutumia nguvu ya vyombo vya dola kunyanyasa
Wapiganaji Makini!.
Wapiganaji makini, hawaingii vitani mpaka kwanza wajue nguvu ya jeshi la adui!, na wakijipima na nguvu yao, wanaamua kutopeleka kwanza majeshi vitani ili kuepuka a loosing battle!, yaani kushindwa!, hawa formula yao ni "never fight a loosing battle", na wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, wakiona dalili za kushindwa, kuliko kuendelea kupigana na kushindwa, yaani just to fight na kuwa wiped out, watarudi nyuma, retreat, kwenda kujijenga upya, mpaka wawe na nguvu ya kutosha to hit back and win, vinginevyo baada ya majaribio kadhaa ya kushindwa, then wanaamua "if you can't beat them, join them" and learn their secrets of battlefields" kinachowafanya washinde!. Hawa watazomewa ni waoga, wanarudi nyuma!, wanakimbia vita!, That is me!, mimi niko kwenye kundi hili!.
Paskali
Mini ni kati ya lile Kundi linalokubali kuwa if you can't beat them, join them!.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

P
 
Weyw Paskali weye! Ukifwanya hivo utakuwa UMEWARUHUSU kutunyanyasa wengine. Pigana. Waoneshe hali halisia. Napenda kuuliza swali: Mtu akilikosea Bunge na "kukutwa na Hatia"
HUKUMU yake ni NINI?
 
Pascal
Mkuu Muyovozi, kwanza asante kwa ushauri huu, mimi niko kwenye hili Kundi hapa chini, hivyo kuitwa tuu Dodoma ni vita kati ya uhuru wa kujieleza na vitisho kutoka mhimili wa dola, hivyo nasubiri barua rasmi nijipange, na utetezi wangu utakuwa na sentensi tatu tuu, "Yote yaliyosemwa ni kweli, nimekubali makosa, naomba mnisamehe!", ukiishakiri kosa, kinachofuatia ni hukumu, hivyo nitakwenda kwa ajili ya kuhukumiwa na sio kubishana na Bunge!.

Mini ni kati ya lile Kundi linalokubali kuwa if you can't beat them, join them!.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

P
Pascal wewe ni great thinker na siyo mpambanaji. Hapo umejenga kitu cha thamani zaidi ya kupambana
 
Mkuu Paskali sikupingi, naheshimu michango yako. Wewe una uzoefu na mambo haya kwa sababu ya kuwa kwenye media na kukutana na viongozi. Hivi pekee havikufanyi ukufuru. Milele maana yake ni isiyo na mwisho, ya kudumu ,isiyozuilika.

Is something holy because it is holy or is it holy because it is loved by the gods? Hii ni nukuu ninayoipenda sana ya mwanafalsafa Socrates. Hapa ndipo ulipo mtego. Kudhani kuwa nguvu pekee zinatosha kumbakiza mtu au kikundi madarakani milele, is very unbecoming.

Wewe unajua sana kwa nini CCM bado iko madarakani. CCM si chama cha siasa kama vyama vingine. Ni chama dola. Kina-cling kwenye dola na kutumia excessive and brutal force ili kisiondoke kwenye power. Bila dola; Polisi, Jeshi, Usalama wa Taifa na rais anayechukia mawazo mbadala, CCM hakina uwezo unaoonekana kuwa nao sasa.

By the way, (sisemi kwa kukunanga) hukumbuki kuwahi kuingia matatani na Serikali kwa ulichokiandika JF? Wewe ni verified member, ni journalist. Serikali nyingi au zote za Afrika zinaogopa sana criticism ya waandishi wa habari. Hiyo ni dalili ya udhaifu. With all due respect sishangai ukiegamia upande unaouegamia kwa kuwa inakupa usalama. Hatukosoi kwa kuwa tunawachukia tunaowakosoa, tunataka wakae kwenye mstari. Hiyo si dhambi. Tunatumia majina feki kwa kuwa kutumia majina halisi ni deadly attempt. Wewe husemi ukweli, unatimiza wajibu, hasa kwa siku za karibuni.

Uniwie radhi sana kama nimevuka mpaka ila lengo ni kujaribu kuweka clarity. Be more pragmatic in your threads not more open.
Usisahau kwenda kumjulia hali Neville pale Muhimbili.
TS.
Mkuu Too Sweet, kwanza asante kwa kuwa bold, truthfully na very objective katika kuusema ukweli na ukosoaji very genuine, honest na truthfully.
Watanzania wengi tukiwemo sisi jf, hatuna tabia ya kujishughulisha kusoma. Hili la umilele wa CCM nimelifafanua vizuri hapa
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. - JamiiForums

Hujafanya kosa lolote, tena in fact nimefurahi sana kwani ni watu wachache sana humu wana level yako ya uelewa, na haswa uliposema maneno haya "Serikali nyingi au zote za Afrika zinaogopa sana criticism ya waandishi wa habari. Hiyo ni dalili ya udhaifu. With all due respect sishangai ukiegamia upande unaouegamia kwa kuwa inakupa usalama. Hatukosoi kwa kuwa tunawachukia tunaowakosoa, tunataka wakae kwenye mstari".

Japo mimi ni mtu wa media, ila media yetu naijua
Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo? - JamiiForums

Mimi pia ni Mtanzania, mkweli na muwazi, na siku zote huwa naweka msimamo wangu wazi, nimesimama wapi na ninasimamia nini
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ? - JamiiForums

Pia nimetoa angalizo la the real situation Tanzania tuliopo
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! - JamiiForums
Asante tena na asante kunikumbusha Neville.
P
 
Wanabodi

Wapiganaji Makini!.
Wapiganaji makini, hawaingii vitani mpaka kwanza wajue nguvu ya jeshi la adui!, na wakijipima na nguvu yao, wanaamua kutopeleka kwanza majeshi vitani ili kuepuka a loosing battle!, yaani kushindwa!, hawa formula yao ni "never fight a loosing battle", na wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, wakiona dalili za kushindwa, kuliko kuendelea kupigana na kushindwa, yaani just to fight na kuwa wiped out, watarudi nyuma, retreat, kwenda kujijenga upya, mpaka wawe na nguvu ya kutosha to hit back and win, or baada ya majaribio kadhaa ya kushindwa, then wanaamua to surrender kwa kanuni ya "if you can't beat them, join them" and learn their secrets of battlefields" kinachowafanya washinde!. Hawa watazomewa ni waoga, wanarudi nyuma!, wanakimbia vita!, That is me!, mimi niko kwenye kundi hili!.

Paskali
Shikamoo baba, Hata wewe pia unaweza ukawa mchambuzi Bora zaidi kuliko tunavyokutazama leo, ila kinachokuvunjia heshima ya taaluma yako na umahiri wako ni siasa na hasa kutaka kuwa kiongozi wa kisiasa badala ya kutumia ile nafasi ya utaalamu aliokupa Mungu.

Ukweli mkuu unaulewa wa Mambo mengi na tena pengine huenda ukawa mchambuzi Bora kuliko hata tunaowafikiria ila umeamua kujitwisha beseni la takataka kichwani na kutuonyesha kuwa wewe huna uelewa na Mambo, ukweli unaujua mwenyewe kwanini umeamua kuwa hivi ulivyo.
Mungu akusaidie uelewe na utambue karama na nafasi aliokupa Mungu uitumikie badala ya kuwa bendera fuata upepo.

Nisamehe sana maana kwa umri wako sikutakiwa niseme haya ila msema kweli ni mpenzi wa Mungu jaribu kujiangalia baba angu umevaa shati kwa kuligeuza alafu unatuambia upo sawa.
Hii inaitwa point blank, na the jf spirit, where we dare talk openly. Nimeipokea hoja yako, maneno yako japo ni makali, lakini ndio ukweli wenyewe, na mtu unapoambiwa ukweli, hata kama ukweli huo utakuuma vipi, inakubidi, uupokee na uukubali. Hivyo nimepokea na nimekubali.

P.
 
Back
Top Bottom