Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,442
- 113,452
Wanabodi
Siasa za Tanzania ni kizungumkuti!. Ni siasa za ubabe, uongo, chuki, fitna na kukomoana badala ya kuleta maendeleo. Chama tawala CCM ni chama dola, hivyo kinatumia uchama tawala wake kwa kutumia nguvu ya vyombo vya dola kunyanyasa wapinzani na kutumia mbinu safi na chafu kushinda chaguzi kwa msaada wa vyombo vya dola na kubebwa na Tume yake "huru" ya uchaguzu, katika uchaguzi "huru na wa haki", huku serikali ya CCM imegubikwa na mlolongo wa kashfa, EPA, Richmond na sasa Escrow, ambazo vinara ni serikali ya CCM na main players ni vigogo wa CCM na makada wa chama, hivyo huu sasa ni uthibitisho tuu kuwa Taifa letu Tanzania tuko vitani, kwenye vita ya pili ya ukombozi wa taifa hili, dhidi ya maadui, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi!. Kwenye vita hii, ni vita ya ndani kwa ndani, walaji rushwa wakuu ni viongizi wa CCM na serikali, mafisadi wakuu, ni viongozi wa CCM serikali na makada, huku wapiganaji wakuu, wakitegemewa ni hao hao CCM!.
Kwenye vita hii, kuna wapiganaji wa aina mbili, na Watazamaji. Hawa ni, kuna wapiganaji shupavu, wapiganaji makini na kuna watazamaji tuu!. Jee wewe uko kwenye kundi gani?!.
Ili kujijua, uko wapi, ni lazima kwanza uyajue makundi haya.
Naomba kukiri wazi kuwa nimekuwa inspired kuandika hii mada kutokana na mchango wa mwana jf mwenzetu kwenye uzi, ambapo mimi nimemsifu mtuhumiwa mmoja wa ufisadi, kuwa ni kweli fulani fisadi huyo ni ndiye "baniani mbaya, kiatu chake dawa!", Pamoja Na Ufisadi Wake Wote, Chenge is One of Best Brains Kwenye Bunge Full of Ignorants, thread hiyo imepelekea mimi kushutumiwa kuwa ninawakumbatia mafisadi!, hivyo mimi ni mmoja wao!, Mwana jf huyu akanishauri na mimi ni lazima nichague upande!, hakuna "standing" on the fence!"
Ukweli halisi ndio ule ambao utasimama mpaka mwisho!, mimi ndani ya moyo wangu na nafsi yangu, sina upande kabisa, japo kuna watu ninawakubali, lakini pamoja na kuwakubali kote, bado ninasimama kwenye ukweli halisi kuwa hao ambao ninawakubali, sii hao watakaoshinda vita hii, nawakubali wataoshinda vita hii ni wale wale kwa mbinu zile zile, japo siwakubali lakini fact ni facts, lazima uzikubali, uwapende usiwapende, uwakubali usiwakubali, ukweli ndio huu!.
Tanzania tuko kwenye vita vya ukombozi wa pili wa nchi yetu!. Kwenye vita hii, tuna wapiganaji mashujaa walioko mstari wa mbele wa mapambano, ambao wao kazi yao ni kupigana tuu, no matter what!. Na kuna wapiganaji makini ambao hawaamua kupigana pale tuu kwenye uhakika wa possibility ya kushinda vita!, lakini kundi kubwa zaidi ni kundi la watazamaji!. Hawa ndio determinant ya kundi lipi lishinde hii vita kwa sababu ushindi wa vita unaitegemea support ya hawa watazamaji na sio nguvu ya jeshi la adui!.
Wapiganaji Shupavu, Shujaa!.
Ndani ya vita hii kuna wapiganaji shupavu, hawa ni wale waliodhamiria kuingia vitani, na ni kweli wameingia vitani, na sasa wako vitani kupigana kufa na kupona, kuikomboa nchi yetu!. Wanapigana kwa ari kubwa huku "motto" yao ni "fight fight fight no matter what!", "no retreat!, no surrender!", hawa watapigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata kama wanajua kabisa kuwa hawatashinda vita hii, na watashindwa tuu kutokana na kuwa na jeshi dogo na silaha duni kuliko adui yao, lakini wataendelea kupigana tuu, na mwisho wa siku, watashindwa and all will be wiped!, ila watakuwa declared "mashujaa wa ukombozi wa taifa" na majina yao, yataandikwa na kumbukwa milele!.
Wapiganaji Makini!.
Wapiganaji makini, hawaingii vitani mpaka kwanza wajue nguvu ya jeshi la adui!, na wakijipima na nguvu yao, wanaamua kutopeleka kwanza majeshi vitani ili kuepuka a loosing battle!, yaani kushindwa!, hawa formula yao ni "never fight a loosing battle", na wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, wakiona dalili za kushindwa, kuliko kuendelea kupigana na kushindwa, yaani just to fight na kuwa wiped out, watarudi nyuma, retreat, kwenda kujijenga upya, mpaka wawe na nguvu ya kutosha to hit back and win, or baada ya majaribio kadhaa ya kushindwa, then wanaamua to surrender kwa kanuni ya "if you can't beat them, join them" and learn their secrets of battlefields" kinachowafanya washinde!. Hawa watazomewa ni waoga, wanarudi nyuma!, wanakimbia vita!, That is me!, mimi niko kwenye kundi hili!.
Wengi wa wapinzani Tanzania ni wapiganaji mashujaa so does wengi wa wana jf, mimi ni miongoni mwa wale wachache tunaosema ukweli huu mchungu bila kumung'unya maneno, ili angalau watusikie, sometimes tunalazimika kutumia maneno makali kama hili la "ignorant!' tunaowaambia kuwa, upinzani Tanzania, bado sana!, kuliko kujiunga na upinzani, ni bora kusimama tuu na kuangalia kuepuka kupoteza muda!, hata kwenye urais wa 2015 ni CCM tena!, simply kwa sababu wapinzani bado hawajawa tayari kushika dola, au kutawala!, vyama vya upinzani Tanzania bado ni vyama vya kianaharakati wa ukombozi badala ya wanamikakati ya kutawala!. Wapinzani wakiambiwa ukweli huu mchungu, wanakasirika!, mimi nitaendelea kuusema ukweli huu mchungu no matter what, kwa sababu ndio ukweli wenyewe halisi!, kwenye urais 2015, wapinzani bado!.
Hivyo 2015, pamoja na rushwa yake, pamoja na ufisadi wake, pamoja na kutufanyia umasikini wote huu kwa Zaidi ya miaka 50, bado CCM itashinda kwa sababu hakuna chama cha kushindana na CCM na kushinda.
Kwenye makundi haya ya wapiganaji, wapo wana CCM ambao wao ni wapiganaji mashujaa, wako tayari kuifia CCM no matter what, ili CCM iendelee kutawala Tanzania milele, hata kama ni kwa kutumia rushwa, ufisadi na kila mbinu chafu ili kuendelea kutawala, watabariki mbinu hizi, ndio maana 2005 EPA kupitia kampuni ya Kagoda, ilitumika kuipatia CCM ushindi wa kishindo!.
Lakini ndani ya CCM hiyo hiyo, ndani yake wapo wapiganaji makini wachache ambao hawa ni kiukweli kabisa, wanakerwa umasikini wa taifa letu, wanakerwa na rushwa na ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM na viongozi wake!, hawa wanakerwa na madudu yanayofanywa na mawaziri wa JK ndio maana walidiriki kuwasema wazi wazi mchana kweupe tena kwenye kadamnasi ya watu, kuwa kina fulani na fulani ni mawaziri mizigo!, au fulani na fulani ni mafisadi, waondoke ndani ya chama chetu kwa kujivua gamba!, wawajibike!. Hawa Wanataka hata kama CCM itaendelea kushinda, ushinde kwa kuchaguliwa kwa haki na uhalali na Watanzania na sio ushinde kwa mbinu chafu!.
Na kwenye upinzani pia wapo wapinzani ambao ni wapigani shupavu, wao target yao ni Ikulu tuu, hata kama wanajua hawana askari wa kutosha kuwafikisha ikulu, wao ni kupigana tuu kuelekea ikulu hata kama wataishia njiani, ndoto yao ni ikulu tuu!.
Ndani ya upinzani, pia wako wapiganaji makini ambao tayari wameishajua mbinu zinazotumiwa na wapinzani haziwezi kuwapa ushindi wa vita hii!, wamegundua udhaifu wa makamanda wao, silaha zao duni na mbinu hafifu za medani zinazotumiwa na viongozi wao wachovu, haziwezi kuwaletea ushindi!, wamejaribu kuhamasisha mageuzi ya ndani, (internal reforms) ndani ya vyama vyao ili vyama vyao viongozwe na majemedari wa vita wenye uwezo wa kutumia mbinu zakisasa za medani, wameishia kuzomewa, kuitwa wasaliti na wengine kuhukumiwa vifo!. Hawa watafika mahali watakatishwa tamaa na upinzani, na mtawashuhudia wakirejea CCM, katika ile falsafa ya "if you cant beat them, join them".
Watazamaji.
Kati ya wapiganaji wa kambi hizi zote mbili, nyuma yao kuna kundi kubwa zaidi la watazamaji!, hawa sio wapiganaji wa kundi lolote, ila ndio wanaoshikilia turufu ya ushindi wa kundi lolote kwa sababu hawa ndio wapigakura. Ili kundi lolote lishinde vita hii, ni lazima kwanza lipate uungwaji mkono wa kundi hili kubwa zaidi la watazamaji!. Jee kwenye hizi kambi mbili, za wapiganaji, jee kuna juhudi zozote za dhati kuwafikia watazamaji?!, au concentrations ni kuwalega tuu wapiganaji ili kuwaangamiza huku tukiwasahau watazamaji ambao ndio determinant wenye turufu ya ushindi?!. Hili ndilo kosa kubwa la upinzani Tanzania.
Ndugu zangu, rafiki zangu, na wapenda mageuzi wa kweli, wameelekeza nguvu kubwa na support yao na mategemeo makubwa kwa Chadema!. Lakini masikini Chadema wenyewe, hawajui watendalo!, concentration ya Chadema, wameielekeza kwa CCM kama adui yao number moja ni CCM!, badala ya ku concentrate on mass mobilization, kuwafikia wapiga kura!. Ikitokea Chadema wakashindwa tena kuitwaa ikulu safari hii ya uchaguzi wa 2015, kosa lao litakuwa ni hili ambalo niliwahi kuwashauri hivi Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa ...
Chadema ikishindwa hapa, ndio itakuwa imefikia peak, baada ya hapo itaanza kuporomoka!.
Jee katika hii safari ya ukombozi wa pili wa taifa hili, wewe mwenzangu umesimama wapi?, uko kwenye kundi gani?!, Jee ni mpiganaji shujaa, mpiganaji makini au ni mtazamaji tuu kama mimi Paskali?.
Paskali

Mkuu Olesa, asante kwa kunieleza ukweli, kwanza nakiri wazi kabisa kuwa mimi Pasco wa jf, ni mtu mwenye matatizo!, na tatizo langu kubwa kabisa siku zote ni kuueleza ukweli halisi vile ulivyo na sio ukweli ambao watu wanautaka kuusikia!, siku zote ukweli halisi huwa mmoja tuu lakini ukweli ambao watu wanapenda kuusikia, sio ukweli mmoja bali kila mtu anakuwa na ukweli wake ule anaopenda!.Tatizo lako kaka ni moja tu, unajua mbivu na mbichi ila hutaki kuchagua kundi moja!!!!