Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Dec 2, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,759
  Trophy Points: 280
  Wanabodi

  Siasa za Tanzania ni kizungumkuti!. Ni siasa za ubabe, uongo, chuki, fitna na kukomoana badala ya kuleta maendeleo. Chama tawala CCM ni chama dola, hivyo kinatumia uchama tawala wake kwa kutumia nguvu ya vyombo vya dola kunyanyasa wapinzani na kutumia mbinu safi na chafu kushinda chaguzi kwa msaada wa vyombo vya dola na kubebwa na Tume yake "huru" ya uchaguzu, katika uchaguzi "huru na wa haki", huku serikali ya CCM imegubikwa na mlolongo wa kashfa, EPA, Richmond na sasa Escrow, ambazo vinara ni serikali ya CCM na main players ni vigogo wa CCM na makada wa chama, hivyo huu sasa ni uthibitisho tuu kuwa Taifa letu Tanzania tuko vitani, kwenye vita ya pili ya ukombozi wa taifa hili, dhidi ya maadui, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi!. Kwenye vita hii, ni vita ya ndani kwa ndani, walaji rushwa wakuu ni viongizi wa CCM na serikali, mafisadi wakuu, ni viongozi wa CCM serikali na makada, huku wapiganaji wakuu, wakitegemewa ni hao hao CCM!.

  Kwenye vita hii, kuna wapiganaji wa aina mbili, na Watazamaji. Hawa ni, kuna wapiganaji shupavu, wapiganaji makini na kuna watazamaji tuu!. Jee wewe uko kwenye kundi gani?!.

  Ili kujijua, uko wapi, ni lazima kwanza uyajue makundi haya.

  Naomba kukiri wazi kuwa nimekuwa inspired kuandika hii mada kutokana na mchango wa mwana jf mwenzetu kwenye uzi, ambapo mimi nimemsifu mtuhumiwa mmoja wa ufisadi, kuwa ni kweli fulani fisadi huyo ni ndiye "baniani mbaya, kiatu chake dawa!", Pamoja Na Ufisadi Wake Wote, Chenge is One of Best Brains Kwenye Bunge Full of Ignorants, thread hiyo imepelekea mimi kushutumiwa kuwa ninawakumbatia mafisadi!, hivyo mimi ni mmoja wao!, Mwana jf huyu akanishauri na mimi ni lazima nichague upande!, hakuna "standing" on the fence!"
  Mkuu Olesa, asante kwa kunieleza ukweli, kwanza nakiri wazi kabisa kuwa mimi Pasco wa jf, ni mtu mwenye matatizo!, na tatizo langu kubwa kabisa siku zote ni kuueleza ukweli halisi vile ulivyo na sio ukweli ambao watu wanautaka kuusikia!, siku zote ukweli halisi huwa mmoja tuu lakini ukweli ambao watu wanapenda kuusikia, sio ukweli mmoja bali kila mtu anakuwa na ukweli wake ule anaopenda!.

  Ukweli halisi ndio ule ambao utasimama mpaka mwisho!, mimi ndani ya moyo wangu na nafsi yangu, sina upande kabisa, japo kuna watu ninawakubali, lakini pamoja na kuwakubali kote, bado ninasimama kwenye ukweli halisi kuwa hao ambao ninawakubali, sii hao watakaoshinda vita hii, nawakubali wataoshinda vita hii ni wale wale kwa mbinu zile zile, japo siwakubali lakini fact ni facts, lazima uzikubali, uwapende usiwapende, uwakubali usiwakubali, ukweli ndio huu!.

  Tanzania tuko kwenye vita vya ukombozi wa pili wa nchi yetu!. Kwenye vita hii, tuna wapiganaji mashujaa walioko mstari wa mbele wa mapambano, ambao wao kazi yao ni kupigana tuu, no matter what!. Na kuna wapiganaji makini ambao hawaamua kupigana pale tuu kwenye uhakika wa posibility ya kushinda vita!, lakini kundi kubwa zaidi ni kundi la watazamaji!. Hawa ndio determinant ya kundi lipi lishinde hii vita kwa sababu ushindi wa vita unaitegemea support ya hawa watazamaji na sio nguvu ya jeshi la adui!.

  Wapiganaji Shupavu, Shujaa!.
  Ndani ya vita hii kuna wapiganaji shupavu, hawa ni wale waliodhamiria kuingia vitani, na ni kweli wameingia vitani, na sasa wako vitani kupigana kufa na kupona, kuikomboa nchi yetu!. Wanapigana kwa ari kubwa huku "motto" yao ni "fight fight fight no matter what!", "no retreat!, no surrender!", hawa watapigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata kama wanajua kabisa kuwa hawatashinda vita hii, na watashindwa tuu kutokana na kuwa na jeshi dogo na silaha duni kuliko adui yao, lakini wataendelea kupigana tuu, na mwisho wa siku, watashindwa and all will be wiped!, ila watakuwa declared "mashujaa wa ukombozi wa taifa" na majina yao, yataandikwa na kumbukwa milele!.

  Wapiganaji Makini!.
  Wapiganaji makini, hawaingii vitani mpaka kwanza wajue nguvu ya jeshi la adui!, na wakijipima na nguvu yao, wanaamua kutopeleka kwanza majeshi vitani ili kuepuka a loosing battle!, yaani kushindwa!, hawa formula yao ni "never fight a loosing battle", na wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, wakiona dalili za kushindwa, kuliko kuendelea kupigana na kushindwa, yaani just to fight na kuwa wiped out, watarudi nyuma, retreat, kwenda kujijenga upya, mpaka wawe na nguvu ya kutosha to hit back and win, vinginevyo baada ya majaribio kadhaa ya kushindwa, then wanaamua "if you can't beat them, join them" and learn their secrets of battlefields" kinachowafanya washinde!. Hawa watazomewa ni waoga, wanarudi nyuma!, wanakimbia vita!, That is me!, mimi niko kwenye kundi hili!.

  Wengi wa wapinzani Tanzania ni wapiganaji mashujaa so does wengi wa wana jf, mimi ni miongoni mwa wale wachache tunaosema ukweli huu mchungu bila kumung'unya maneno, ili angalau watusikie, sometimes tunalazimika kutumia maneno makali kama hili la "ignorant!' tunaowaambia kuwa, upinzani Tanzania, bado sana!, kuliko kujiunga na upinzani, ni bora kusimama tuu na kuangalia kuepuka kupoteza muda!, hata kwenye urais wa 2015 ni CCM tena!, simply kwa sababu wapinzani bado hawajawa tayari kushika dola, au kutawala!, vyama vya upinzani Tanzania bado ni vyama vya kianaharakati wa ukombozi badala ya wanamikakati ya kutawala!. Wapinzani wakiambiwa ukweli huu mchungu, wanakasirika!, mimi nitaendelea kuusema ukweli huu mchungu no matter what, kwa sababu ndio ukweli wenyewe halisi!, kwenye urais 2015, wapinzani bado!.

  Hivyo 2015, pamoja na rushwa yake, pamoja na ufisadi wake, pamoja na kutufanyia umasikini wote huu kwa Zaidi ya miaka 50, bado CCM itashinda kwa sababu hakuna chama cha kushindana na CCM na kushinda.

  Kwenye makundi haya ya wapiganaji, wapo wana CCM ambao wao ni wapiganaji mashujaa, wako tayari kuifia CCM no matter what, ili CCM iendelee kutawala Tanzania milele, hata kama ni kwa kutumia rushwa, ufisadi na kila mbinu chafu ili kuendelea kutawala, watabariki mbinu hizi, ndio maana 2005 EPA kupitia kampuni ya Kagoda, ilitumika kuipatia CCM ushindi wa kishindo!.

  Lakini ndani ya CCM hiyo hiyo, ndani yake wapo wapiganaji makini wachache ambao hawa ni kiukweli kabisa, wanakerwa umasikini wa taifa letu, wanakerwa na rushwa na ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM na viongozi wake!, hawa wanakerwa na madudu yanayofanywa na mawaziri wa JK ndio maana walidiriki kuwasema wazi wazi mchana kweupe tena kwenye kadamnasi ya watu, kuwa kina fulani na fulani ni mawaziri mizigo!, au fulani na fulani ni mafisadi, waondoke ndani ya chama chetu kwa kujivua gamba!, wawajibike!. Hawa Wanataka hata kama CCM itaendelea kushinda, ushinde kwa kuchaguliwa kwa haki na uhalali na Watanzania na sio ushinde kwa mbinu chafu!.

  Na kwenye upinzani pia wapo wapinzani ambao ni wapigani shupavu, wao target yao ni Ikulu tuu, hata kama wanajua hawana askari wa kutosha kuwafikisha ikulu, wao ni kupigana tuu kuelekea ikulu hata kama wataishia njiani, ndoto yao ni ikulu tuu!.

  Ndani ya upinzani, pia wako wapiganaji makini ambao tayari wameishajua mbinu zinazotumiwa na wapinzani haziwezi kuwapa ushindi wa vita hii!, wamegundua udhaifu wa makamanda wao, silaha zao duni na mbinu hafifu za medani zinazotumiwa na viongozi wao wachovu, haziwezi kuwaletea ushindi!, wamejaribu kuhamasisha mageuzi ya ndani, (internal reforms) ndani ya vyama vyao ili vyama vyao viongozwe na majemedari wa vita wenye uwezo wa kutumia mbinu zakisasa za medani, wameishia kuzomewa, kuitwa wasaliti na wengine kuhukumiwa vifo!. Hawa watafika mahali watakatishwa tamaa na upinzani, na mtawashuhudia wakirejea CCM, katika ile falsafa ya "if you cant beat them, join them".

  Watazamaji.
  Kati ya wapiganaji wa kambi hizi zote mbili, nyuma yao kuna kundi kubwa zaidi la watazamaji!, hawa sio wapiganaji wa kundi lolote, ila ndio wanaoshikilia turufu ya ushindi wa kundi lolote kwa sababu hawa ndio wapigakura. Ili kundi lolote lishinde vita hii, ni lazima kwanza lipate uungwaji mkono wa kundi hili kubwa zaidi la watazamaji!. Jee kwenye hizi kambi mbili, za wapiganaji, jee kuna juhudi zozote za dhati kuwafikia watazamaji?!, au concentrations ni kuwalega tuu wapiganaji ili kuwaangamiza huku tukiwasahau watazamaji ambao ndio determinant wenye turufu ya ushindi?!. Hili ndilo kosa kubwa la upinzani Tanzania.

  Ndugu zangu, rafiki zangu, na wapenda mageuzi wa kweli, wameelekeza nguvu kubwa na support yao na mategemeo makubwa kwa Chadema!. Lakini masikini Chadema wenyewe, hawajui watendalo!, concentration ya Chadema, wameielekeza kwa CCM kama adui yao number moja ni CCM!, badala ya ku concentrate on mass mobilization, kuwafikia wapiga kura!. Ikitokea Chadema wakashindwa tena kuitwaa ikulu safari hii ya uchaguzi wa 2015, kosa lao litakuwa ni hili ambalo niliwahi kuwashauri hivi Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa ...
  Chadema ikishindwa hapa, ndio itakuwa imefikia peak, baada ya hapo itaanza kuporomoka!.

  Jee katika hii safari ya ukombozi wa pili wa taifa hili, wewe mwenzangu umesimama wapi?, uko kwenye kundi gani?!, Jee ni mpiganaji shujaa, mpiganaji makini au ni mtazamaji tuu kama mimi Paskali?.

  Paskali
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #21
  Dec 13, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,759
  Trophy Points: 280
  Vita vinaendelea, nimesikia wapiganaji wamekubali kuweka silaha chini na kumsusia ngedere shamba la mahindi.

  Jee tutafika?.

  Pascal
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #22
  Dec 17, 2017
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 13,081
  Likes Received: 6,869
  Trophy Points: 280
  Very sad ....wanaposusa tena kwenye ubunge ndio wanasaidia uumaliza upinzani ...tunarudi tulikotoka while tulishapiga hatua kubwa sana ...
   
 4. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #23
  Mar 28, 2018
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,541
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  Vita hii ni ngumu kwa sababu CCM Jeshi lao lipo huru linafanya mazoezi linafanya mikutano lina kila kitu, lakini Jeshi la Wapinzani halipo huru mikutano ni marufuku hata vikao vya ndani vinavamiwa na polisiccm huku wakiwabambikia kesi na mahakamaccm ikiwafunga na Heri mlinzi wa Bashite na akina Jerry muro ( wasiojulikana) wakitumia Nissan nyeupe kuwapiga Risasi akina Lisu na kuwateka akina ben sanane, ni vita ya upande mmoja wenye bunduki zote ukitaka kupigana na upande usio na siraha yeyote wala fimbo, Bondia wa chadema mwenye kg40 amefungwa kamba kwa nyuma alafu wanataka apambane na bondia wa CCM mwenye kg 150 ambaye kashiba na mikono ipo wazi. Kwa utawala huu wa kidikteta ni vigumu Wapinzani kupenya wakafanya siasa, njia pekee ya kuwaokoa Wapinzani ni kwenda kufungua kesi kwenye mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague.
   
 5. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #24
  Mar 28, 2018
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,541
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  Njia pekee iliyosalia ni chadema kwenda haraka kufungua kesi kwenye mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague na endapo chadema hawatafanya hivyo wajue moja kwa moja wanapotea watakuwa kama TLP na NCCR kisha Msajili ataifuta milele na CCM kurejesha mfumo wa chama kimoja.
   
 6. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #25
  Mar 28, 2018
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,541
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  njia za kudai Uhuru ni kwenda UN, pia kwenda kwenye Taasisi za haki za binadamu haki za Uhuru wa Habari za kimataifa, mahakama za kimataifa huko ndipo watapaza Sauti na kuwazindua Mtukufu malaika toka na Naibu Rais Maliyamungu Bashite waache Udikteta wao na kurejesha umoja wa kitaifa ambao inaelekea kubaya zaidi.
   
 7. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #26
  Mar 28, 2018
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,541
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni mwanachama wa UN na huko wana vitengo vya kudhibiti serikali za kidikteta na serikali zibazofanya mambo yanayokiuka haki za binadamu ni kwa nini chadema na Wapinzani wanaogopa kwenda huko?
   
 8. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #27
  Mar 28, 2018
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,541
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  Chadema na Wapinzani kwa ujumla wasipotumia unyanyasaji huu wa sasa kuishitaki serikali ya Awamu ya Tano kwenye mahakama za uhalifu wa kimataifa na jumuia za haki za binadamu mapema wapewe haki zao watambue kuwa mwaka 2020 hakutakuwa na Mbunge wa chadema atarejea bungeni tena, kuanzia mwaka 2020 serikali ya Tanzania itakuwa kama China ni mwendo wa mfumo wa chama kimoja mpaka milele na Msajili anajiandaa kuvifuta vyama vyote vya upinzani.
   
 9. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #28
  Mar 28, 2018
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,541
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  Kuna mamluki wengi wapo CCM baada ya kununuliwa na kile kikundi cha Naibu Rais Maliyamungu Bashite huko baadae watasaidia kutoa taarifa kwa chadema na upinzani kwa ujumla lakini endapo CCM hawatafanya kama walivyopanga kufanya sasa ambapo Msajili anajipanga kuvifuta vyama vya upinzani huku mwaka 2020 wakitaka wabunge wote wawe wa CCM pekee Nchi iwe ya chama kimoja kama China na Rais atawale milele na milele kama China na Burundi
   
 10. M

  Maharo JF-Expert Member

  #29
  Mar 28, 2018
  Joined: Aug 22, 2016
  Messages: 2,334
  Likes Received: 1,382
  Trophy Points: 280
  hii ni thread ya mwaka 2014 kumbe haya mambo yalikuwepo ila tumeshayasahau
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #30
  Apr 14, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu Muyovozi, kwanza asante kwa ushauri huu, mimi niko kwenye hili Kundi hapa chini, hivyo kuitwa tuu Dodoma ni vita kati ya uhuru wa kujieleza na vitisho kutoka mhimili wa dola, hivyo nasubiri barua rasmi nijipange, na utetezi wangu utakuwa na sentensi tatu tuu, "Yote yaliyosemwa ni kweli, nimekubali makosa, naomba mnisamehe!", ukiishakiri kosa, kinachofuatia ni hukumu, hivyo nitakwenda kwa ajili ya kuhukumiwa na sio kubishana na Bunge!.
  Mini ni kati ya lile Kundi linalokubali kuwa if you can't beat them, join them!.
  If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

  P
   
 12. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #31
  Apr 14, 2018
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,513
  Likes Received: 1,800
  Trophy Points: 280
  Weyw Paskali weye! Ukifwanya hivo utakuwa UMEWARUHUSU kutunyanyasa wengine. Pigana. Waoneshe hali halisia. Napenda kuuliza swali: Mtu akilikosea Bunge na "kukutwa na Hatia"
  HUKUMU yake ni NINI?
   
 13. k

  komamgo JF-Expert Member

  #32
  Apr 14, 2018
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 956
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 80
  Pascal
  Pascal wewe ni great thinker na siyo mpambanaji. Hapo umejenga kitu cha thamani zaidi ya kupambana
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...