Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Dec 2, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,649
  Likes Received: 23,866
  Trophy Points: 280
  Wanabodi

  Siasa za Tanzania ni kizungumkuti!. Ni siasa za ubabe, uongo, chuki, fitna na kukomoana badala ya kuleta maendeleo. Chama tawala CCM ni chama dola, hivyo kinatumia uchama tawala wake kwa kutumia nguvu ya vyombo vya dola kunyanyasa wapinzani na kutumia mbinu safi na chafu kushinda chaguzi kwa msaada wa vyombo vya dola na kubebwa na Tume yake "huru" ya uchaguzu, katika uchaguzi "huru na wa haki", huku serikali ya CCM imegubikwa na mlolongo wa kashfa, EPA, Richmond na sasa Escrow, ambazo vinara ni serikali ya CCM na main players ni vigogo wa CCM na makada wa chama, hivyo huu sasa ni uthibitisho tuu kuwa Taifa letu Tanzania tuko vitani, kwenye vita ya pili ya ukombozi wa taifa hili, dhidi ya maadui, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi!. Kwenye vita hii, ni vita ya ndani kwa ndani, walaji rushwa wakuu ni viongizi wa CCM na serikali, mafisadi wakuu, ni viongozi wa CCM serikali na makada, huku wapiganaji wakuu, wakitegemewa ni hao hao CCM!.

  Kwenye vita hii, kuna wapiganaji wa aina mbili, na Watazamaji. Hawa ni, kuna wapiganaji shupavu, wapiganaji makini na kuna watazamaji tuu!. Jee wewe uko kwenye kundi gani?!.

  Ili kujijua, uko wapi, ni lazima kwanza uyajue makundi haya.

  Naomba kukiri wazi kuwa nimekuwa inspired kuandika hii mada kutokana na mchango wa mwana jf mwenzetu kwenye uzi, ambapo mimi nimemsifu mtuhumiwa mmoja wa ufisadi, kuwa ni kweli fulani fisadi huyo ni ndiye "baniani mbaya, kiatu chake dawa!", Pamoja Na Ufisadi Wake Wote, Chenge is One of Best Brains Kwenye Bunge Full of Ignorants, thread hiyo imepelekea mimi kushutumiwa kuwa ninawakumbatia mafisadi!, hivyo mimi ni mmoja wao!, Mwana jf huyu akanishauri na mimi ni lazima nichague upande!, hakuna "standing" on the fence!"
  Mkuu Olesa, asante kwa kunieleza ukweli, kwanza nakiri wazi kabisa kuwa mimi Pasco wa jf, ni mtu mwenye matatizo!, na tatizo langu kubwa kabisa siku zote ni kuueleza ukweli halisi vile ulivyo na sio ukweli ambao watu wanautaka kuusikia!, siku zote ukweli halisi huwa mmoja tuu lakini ukweli ambao watu wanapenda kuusikia, sio ukweli mmoja bali kila mtu anakuwa na ukweli wake ule anaopenda!.

  Ukweli halisi ndio ule ambao utasimama mpaka mwisho!, mimi ndani ya moyo wangu na nafsi yangu, sina upande kabisa, japo kuna watu ninawakubali, lakini pamoja na kuwakubali kote, bado ninasimama kwenye ukweli halisi kuwa hao ambao ninawakubali, sii hao watakaoshinda vita hii, nawakubali wataoshinda vita hii ni wale wale kwa mbinu zile zile, japo siwakubali lakini fact ni facts, lazima uzikubali, uwapende usiwapende, uwakubali usiwakubali, ukweli ndio huu!.

  Tanzania tuko kwenye vita vya ukombozi wa pili wa nchi yetu!. Kwenye vita hii, tuna wapiganaji mashujaa walioko mstari wa mbele wa mapambano, ambao wao kazi yao ni kupigana tuu, no matter what!. Na kuna wapiganaji makini ambao hawaamua kupigana pale tuu kwenye uhakika wa posibility ya kushinda vita!, lakini kundi kubwa zaidi ni kundi la watazamaji!. Hawa ndio determinant ya kundi lipi lishinde hii vita kwa sababu ushindi wa vita unaitegemea support ya hawa watazamaji na sio nguvu ya jeshi la adui!.

  Wapiganaji Shupavu, Shujaa!.
  Ndani ya vita hii kuna wapiganaji shupavu, hawa ni wale waliodhamiria kuingia vitani, na ni kweli wameingia vitani, na sasa wako vitani kupigana kufa na kupona, kuikomboa nchi yetu!. Wanapigana kwa ari kubwa huku "motto" yao ni "fight fight fight no matter what!", "no retreat!, no surrender!", hawa watapigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata kama wanajua kabisa kuwa hawatashinda vita hii, na watashindwa tuu kutokana na kuwa na jeshi dogo na silaha duni kuliko adui yao, lakini wataendelea kupigana tuu, na mwisho wa siku, watashindwa and all will be wiped!, ila watakuwa declared "mashujaa wa ukombozi wa taifa" na majina yao, yataandikwa na kumbukwa milele!.

  Wapiganaji Makini!.
  Wapiganaji makini, hawaingii vitani mpaka kwanza wajue nguvu ya jeshi la adui!, na wakijipima na nguvu yao, wanaamua kutopeleka kwanza majeshi vitani ili kuepuka a loosing battle!, yaani kushindwa!, hawa formula yao ni "never fight a loosing battle", na wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, wakiona dalili za kushindwa, kuliko kuendelea kupigana na kushindwa, yaani just to fight na kuwa wiped out, watarudi nyuma, retreat, kwenda kujijenga upya, mpaka wawe na nguvu ya kutosha to hit back and win, vinginevyo baada ya majaribio kadhaa ya kushindwa, then wanaamua "if you can't beat them, join them" and learn their secrets of battlefields" kinachowafanya washinde!. Hawa watazomewa ni waoga, wanarudi nyuma!, wanakimbia vita!, That is me!, mimi niko kwenye kundi hili!.

  Wengi wa wapinzani Tanzania ni wapiganaji mashujaa so does wengi wa wana jf, mimi ni miongoni mwa wale wachache tunaosema ukweli huu mchungu bila kumung'unya maneno, ili angalau watusikie, sometimes tunalazimika kutumia maneno makali kama hili la "ignorant!' tunaowaambia kuwa, upinzani Tanzania, bado sana!, kuliko kujiunga na upinzani, ni bora kusimama tuu na kuangalia kuepuka kupoteza muda!, hata kwenye urais wa 2015 ni CCM tena!, simply kwa sababu wapinzani bado hawajawa tayari kushika dola, au kutawala!, vyama vya upinzani Tanzania bado ni vyama vya kianaharakati wa ukombozi badala ya wanamikakati ya kutawala!. Wapinzani wakiambiwa ukweli huu mchungu, wanakasirika!, mimi nitaendelea kuusema ukweli huu mchungu no matter what, kwa sababu ndio ukweli wenyewe halisi!, kwenye urais 2015, wapinzani bado!.

  Hivyo 2015, pamoja na rushwa yake, pamoja na ufisadi wake, pamoja na kutufanyia umasikini wote huu kwa Zaidi ya miaka 50, bado CCM itashinda kwa sababu hakuna chama cha kushindana na CCM na kushinda.

  Kwenye makundi haya ya wapiganaji, wapo wana CCM ambao wao ni wapiganaji mashujaa, wako tayari kuifia CCM no matter what, ili CCM iendelee kutawala Tanzania milele, hata kama ni kwa kutumia rushwa, ufisadi na kila mbinu chafu ili kuendelea kutawala, watabariki mbinu hizi, ndio maana 2005 EPA kupitia kampuni ya Kagoda, ilitumika kuipatia CCM ushindi wa kishindo!.

  Lakini ndani ya CCM hiyo hiyo, ndani yake wapo wapiganaji makini wachache ambao hawa ni kiukweli kabisa, wanakerwa umasikini wa taifa letu, wanakerwa na rushwa na ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM na viongozi wake!, hawa wanakerwa na madudu yanayofanywa na mawaziri wa JK ndio maana walidiriki kuwasema wazi wazi mchana kweupe tena kwenye kadamnasi ya watu, kuwa kina fulani na fulani ni mawaziri mizigo!, au fulani na fulani ni mafisadi, waondoke ndani ya chama chetu kwa kujivua gamba!, wawajibike!. Hawa Wanataka hata kama CCM itaendelea kushinda, ushinde kwa kuchaguliwa kwa haki na uhalali na Watanzania na sio ushinde kwa mbinu chafu!.

  Na kwenye upinzani pia wapo wapinzani ambao ni wapigani shupavu, wao target yao ni Ikulu tuu, hata kama wanajua hawana askari wa kutosha kuwafikisha ikulu, wao ni kupigana tuu kuelekea ikulu hata kama wataishia njiani, ndoto yao ni ikulu tuu!.

  Ndani ya upinzani, pia wako wapiganaji makini ambao tayari wameishajua mbinu zinazotumiwa na wapinzani haziwezi kuwapa ushindi wa vita hii!, wamegundua udhaifu wa makamanda wao, silaha zao duni na mbinu hafifu za medani zinazotumiwa na viongozi wao wachovu, haziwezi kuwaletea ushindi!, wamejaribu kuhamasisha mageuzi ya ndani, (internal reforms) ndani ya vyama vyao ili vyama vyao viongozwe na majemedari wa vita wenye uwezo wa kutumia mbinu zakisasa za medani, wameishia kuzomewa, kuitwa wasaliti na wengine kuhukumiwa vifo!. Hawa watafika mahali watakatishwa tamaa na upinzani, na mtawashuhudia wakirejea CCM, katika ile falsafa ya "if you cant beat them, join them".

  Watazamaji.
  Kati ya wapiganaji wa kambi hizi zote mbili, nyuma yao kuna kundi kubwa zaidi la watazamaji!, hawa sio wapiganaji wa kundi lolote, ila ndio wanaoshikilia turufu ya ushindi wa kundi lolote kwa sababu hawa ndio wapigakura. Ili kundi lolote lishinde vita hii, ni lazima kwanza lipate uungwaji mkono wa kundi hili kubwa zaidi la watazamaji!. Jee kwenye hizi kambi mbili, za wapiganaji, jee kuna juhudi zozote za dhati kuwafikia watazamaji?!, au concentrations ni kuwalega tuu wapiganaji ili kuwaangamiza huku tukiwasahau watazamaji ambao ndio determinant wenye turufu ya ushindi?!. Hili ndilo kosa kubwa la upinzani Tanzania.

  Ndugu zangu, rafiki zangu, na wapenda mageuzi wa kweli, wameelekeza nguvu kubwa na support yao na mategemeo makubwa kwa Chadema!. Lakini masikini Chadema wenyewe, hawajui watendalo!, concentration ya Chadema, wameielekeza kwa CCM kama adui yao number moja ni CCM!, badala ya ku concentrate on mass mobilization, kuwafikia wapiga kura!. Ikitokea Chadema wakashindwa tena kuitwaa ikulu safari hii ya uchaguzi wa 2015, kosa lao litakuwa ni hili ambalo niliwahi kuwashauri hivi Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa ...
  Chadema ikishindwa hapa, ndio itakuwa imefikia peak, baada ya hapo itaanza kuporomoka!.

  Jee katika hii safari ya ukombozi wa pili wa taifa hili, wewe mwenzangu umesimama wapi?, uko kwenye kundi gani?!, Jee ni mpiganaji shujaa, mpiganaji makini au ni mtazamaji tuu kama mimi Paskali?.

  Paskali
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2014
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,103
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  SIlaha za maangamizi tumepewa, basi tu hatujaamua kuzitumia kwa akili. Na shibe ya siku moja, t shirt, kofia na kanga ndio vinatuangamiza.

  Silaha ya maangamizi kwa sasa ni kura yako, tumeshaona mengi, hope tumejifunza.

  Ukishatetea tummoja wa mafisadi kuongoza nchi hii, tunabaki na walakini.
   
 3. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #3
  Dec 2, 2014
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,618
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Pasco

  Nitachangia baadae. Nataka kukusoma between words not only lines. Maana huwa unapenda kuwa confuser.

  Lakini naomba nitoe concern moja kwa sasa, considering you are a senior fellow in the professionalism and you have a reputable backgroud in the same, vichwa vyako vya habari vinapaswa kuwa tofauti na watu wengine kaka.

  Si mara moja au mara mbili unakiuka kabisa basics za hata writing skills achilia mbali uandishi wa habari. Unawezaje kuandika headline ya namna hiyo inayokiuka skills za uandishi. Mfano, unawekaje nukta mbele ya alama ya kushangaa au kuuliza. You, you must be different bwana. Huwezi kuwa kama akina Lukosi hivi...

  Asante. Samahani kwa kutoku-pm maana hii inaweza kusaidia wengine pia labda...utanisamehe kama nitakuwa nimekukwaza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Azizi Mussa

  Azizi Mussa Verified User

  #4
  Dec 2, 2014
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,792
  Likes Received: 2,450
  Trophy Points: 280
  @Pasco , mimi niko kundi hili: naamini wengi wako kundi hili, nawe nakukaribisha kundini.Karibu sana!
  [​IMG]
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2014
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,712
  Likes Received: 7,936
  Trophy Points: 280
  Hili jambo unalikuza mno bila sababu za msingi labda "kutisha" wananchi. Hatuko kwenye vita vya kimiwili, damu, na nyama mithili ya vita vya mizinga, magari ya deraya, na B52's ambavyo jeshi linatakiwa kujipanga ipasavyo!

  "Vita" hivi ni rahisi sana - just UTASHI wa kisiasa. Jemadari Mkuu ambaye tumekabidhi mamlaka yote kwake na tukampa nguvu za ajabu Kikatiba na aseme neno moja tu, nchi itapona.
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2014
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 23,169
  Likes Received: 6,881
  Trophy Points: 280
  Hivi Pasco uliwahi kusoma hii novel? Naamini wewe ni old school kama mimi na enzi zetu tulisoma sana vitabu vya huyu jamaa. kama hujakisoma nenda pale SCHOLARSTIC Bookshop Mlimani City utakipata!

  [​IMG]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Dec 2, 2014
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  Sitachagua A,B au C kwa sababu sina chaguo,Unajua...

  Ninachoweza kusema This is one of the best threads.

  Hii ni kwa Great thinkers tu.Comments za watu automatically zitawa-position.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. t

  twijuke JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2014
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu Pasco umeeleza vizuri na umejipambanua vyema.

  Kwanza unaposema vita kuna kundi kubwa la watanzania ambao macho yao hayaoni hiyo vita. Watu wanahitaji waelimishwe kwanza wajibu wao na uhuru na ukomo wa mipaka ya Uhuru wao.

  Hatuwezi shinda vita hii tukiwa hatujielewi, hatuwezi kushinda vita hii tukiwa tunaona matumbo yetu ni ya maana kuliko taifa. Heri umasikini wa kipato kuliko wa kifkra.

  Nimeshuhudia wananchi wakibebwa na magari,vibajaji na bodaboda wakipelekwa kuandikishwa ili badaye wapige kula ktk chaguzi za serikali za mitaa.

  Hapa aliye anzisha wazo hili ni wazi alijua hawawezi kwenda wenyewe. Ni imani yangu kuwa aliye wapeleka kujiandikisha ni wazi kuwa atawapeleka pia wakapige kura.

  Hiki ni kiwango cha juu cha ubwege kuwa na watanzania wa namna hii. Je! Unawatanzania wa aina hii utapigana vita gani?

  Kuna wakati nakuwa na mashaka juu ya kinachoitwa "AMANI" napata mashaka kusema tunaamani katikati ya watu wasiojua haki zao, ndiyo maana hata ufisadi unastawi, ni kwasababu mafisadi wanaami wako katikati ya kundi la mabwege na wanatenda haya wakijua hakuna madhara.

  Magazeti ya udaku na michezo yanaongoza kwa mauzo kuliko magazeti yanayoandika mambo yanahusu mstakabali wa taifa.

  Baadhi ya watazania wanajifanya wanahitaji mabadiliko lakini si washiriki wa mabadiliko.

  Sasa tuna kundi lenu la wana habari,baadhi ya wanahabari wamekuwa wakiwalisha sumu watanzania, wana habari wengi leo wanasujudu matumbo kuliko uzalendo. "TUMBO INVESTMENT" yaani baada ya kuwapa elimu watanzania wao wanawalisha sumu.

  Leo ukikuta mwandishi ameandika habari lazima kati ya matakwa mawili awe amekidhi moja, kama hamjengi mtu,kikundi au taasisi, basi anabomoa.

  Pasco hapa vita inapiganwaje? Kwa wingi wetu vita naiona lakini wapambanaji ni wachache sawa na hakuna. Nashindwa kujipambanua wala kupambanua.
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Dec 2, 2014
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280

  twijuke unaweza kuwa miongoni mwa watu wachache sana waliomuelewa Pasco
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2014
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,840
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  mkuu hata mimi nipo kundi lako but nadhani, ma wangu unakaribia wakua mpambanaji wa kweli
   
 11. t

  twijuke JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2014
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu Ben, maana yangu vita ipo lakini sioni wapiganaji, na kama wapo, kwa wingi wetu ni wachache sana sawa na hakuna. Leo tupo wastan wa 46million wapambanaji 100 Napa unasemaje? Ndiyo maana sikuona hata namna ya upambanuaje, kama mada ya Mkuu Pasco inavyosema.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,649
  Likes Received: 23,866
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa yangu fulani mimi nilimdhania ni mpigaji shupavu!, lakini leo nimeshangazwa amebwaga manyanga na kuikimbia vita!. Wapiganaji shupavu, hupigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike!, leo imekuweje tena?!. Nasikia sikia, nasubiria kusikia kwa masikio yangu mwenyewe!.

  Pasco
   
 13. P

  Prince k JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2015
  Joined: Jan 10, 2015
  Messages: 2,103
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nachojua mimi sipo chama cha mafisi ...na mafisi aka ccm
   
 14. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2015
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,439
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Kwa tanzania yetu hii ya kuishi bila elimu ya uraia Usijeshangaa Watazamaji wakivamia uwanja wa Mapambano na kumtangaza aliyeshindwa kuwa ndiye mshindi.
  Rejea uchaguzi mkuu 2010 Rostam pale Igunga alipochukua kura za Kikwete na zake akampa Kikwete na mambo yanasonga.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,649
  Likes Received: 23,866
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza naheshimu mawazo yako, japo huu nao ni uchochezi wa aina yake!, nimeamua nikukaribishe hapa katika thread ya vita, ujipime, ila Lowassa ni mpigaji shujaa, shupavu na makini. October 25, ataiingiza Chadema Ikulu ya Magogoni!.

  Wapiganaji wengine wote, wenye mapenzi ya kweli na mageuzi, wataunga mkono juhudi hizi, ila wale wote wenye mapenzi ya upinzani kwa nje, and pays lots of lip services, lakini sasa CCM inakwenda kupata kipigo cha kweli, kipigo kitakatifu, na kifo cha kweli, ndio sasa mnaibuka na kuoanza kuumia mioyoni mwenu!.

  Pole na karibu hapa!.

  Pasco
   
 16. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2015
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,862
  Likes Received: 10,525
  Trophy Points: 280

  Nami nimeshangazwa sana na hii ya wapiganaji kurudi nyuma baada ya kuteka kamanda wa adui zao....
   
 17. mgosi9

  mgosi9 JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2015
  Joined: Jun 17, 2014
  Messages: 1,585
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 133
  no turning back makamanda.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,649
  Likes Received: 23,866
  Trophy Points: 280
  Naendelea kuwafuatilia baadhi ya makamanda na wapiganji, kuwapima wamesimama wapi!.

  Pasco
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,649
  Likes Received: 23,866
  Trophy Points: 280
  Mkuu Danny, nakubaliana na wewe, dawa ya adui sii kumkimbia au kumpisha bali kukabiliana nae, na hata kama utaangamia katika kukabiliana huko, na kupoteza maisha, jina lako ndilo litabaki kama shujaa, cha muhimu cha kujiuliza, ni nani muhimu zaidi kati ya shujaa mfu, au mfungwa hai aliye gerezani?!, au aliyejificha mwituni?!.

  Kwa maoni yangu, kama unakiona kifo kile, halafu unakikimbilia na kufa tuu ili uonekane shujaa, wewe ni shujaa mjinga!. Kama unataka kushindana au kupigana na mtu mwenye nguvu zaidi yako, hivyo unaingia kwenye mapambano ili hali unajua utawawa, wewe pia ni shujaa mjinga!. Shujaa mwerevu ni yule ambaye hawezi kuingia kwenye vita ambayo anajua atashindwa!, bali atampisha huyo mwenye nguvu, huku yeye akijijenga mpaka awe na nguvu za kukabiliana na kushinda!.

  Naomba take time kasome bandiko langu hili, utanielewa ninamaanisha nini
  Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na ...

  Pasco
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,649
  Likes Received: 23,866
  Trophy Points: 280
  Kwa hili la Max, JF iko vitani. Serikali ya Magufuli kupitia waziri wake ambaye ni mwana JF, mwenzetu, Mhe.Mwigulu Nchemba, na mwana JF mwingine kwa jina la TCRA, wametangaza vita na JF.

  Zingatia angalizo hili muhimu.
  Paskali
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...