Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,656
KUNA UZALENDO. Hii ni dhana pana sana hasa linapokuja suala la nchi.. Yeyote anayeweka maslahi ya taifa lake mbele kabla ya mengine yote huyo ni mzalendo nambari moja.
Maslahi kiuchumi
Maslahi kijamii
Maslahi kiusalama...nk nk
Uzalendo ni zaidi ya porojo majukwaani...uzalendo ni VITENDO na tafsiri sahihi isiyobagua kwa maslahi ya taifa na watu wake wote...!!!!
KUNA UHUJUMU UCHUMI...Hii nayo ni dhana pana pia...hasa linapokuja swala la uchumi wa nchi....Mhujumu uchumi si lazima awe mwizi wa mamilioni na kuyaficha kwa matumizi binafsi na familia yake...la hasha...Mhujumu uchumi ambaye automatically anahujumu pato la nchi ni yule kwa namna moja ama nyingine atasababisha pesa iliyopaswa kuingia kwenye kibubu cha taifa iende kwingine
Hata kitendo cha daktari kutoa matibabu bandia ni kuhujumu uchumi kwakuwa mgonjwa ataathirika zaidi na kutumia pesa nyingi zaidi kupata matibabu ambayo dawa nyingi tunanunua toka nje
Mhujumu uchumi ni yule afisa wa mamlaka ya mapato anayeidhinisha malipo ya leseni ya udereva kwa kijana asiyepitia shule ya udereva...! Huyu akienda kusabibisha ajali atapoteza wangapi? Wanaotegemewa na taifa na familia ngapi? Atajeruhi wangapi watakaotumia gharama kubwa kutibiwa? Atafanya uharibifu wa mali ngapi ambazo baadhi matengenezo yake yatahitaji vipuri toka nje?
Kipindi cha uchaguzi mkuu kinachotokea mara moja tu kwa miaka mitano ni kipindi muhimu mno kwa kila mmoja wetu na kwa kila kaliba kwenye jamii...ni kipindi ambacho kila mmoja anapaswa kushiriki katika nafasi yake... Ni kipindi cha kutengeneza historia na kujifunza mengi...
Kipindi cha uchaguzi mkuu ni kipindi cha mavuno kwa waandishi wa habari na wanahabari...
Taifa linakuwa na bajeti ya Uchaguzi
Vyama vinakuwa na bajeti ya Uchaguzi
Wagombea wanakuwa na bajeti ya Uchaguzi
Vyombo vya habari navyo hutenga bajeti zao kwa ajili ya Uchaguzi...hakika ni kipindi cha ahueni kubwa kwa wanahabari
Hawa huchaguiza mzunguko wa pesa kwa chochote kitu wanachopata
Wanaosemesha na kusoma watalipa ada
Wanaodaiwa kodi watalipa
Wenye madeni watalipa
Wenye viwanja na ujenzi watafanya manunuzi...nknk ...pesa inakuwa inazunguka ndani ya nchi....
Kwa Uchaguzi wenye vyama vingi ni ngumu kuzuiya jamii kuwa na fikra za chama kimoja kikatiba kimtazamo hata kimaono!
Kwa uchaguzi wenye vyama vingi itakuwa ni kukosa uzalendo na kusababisha uhujumu uchumi mkubwa kwa kuvitisha na kuvipiga pini vyombo vya habari visitangaze maono ya wengine.....kwa kufanya hivyo jamii itakosa msisimko...wanahabari watakosa cha kuripoti kwasababu ya woga na automatically watakosa mapato
Vyama navyo vitatafuta njia ya kuifikia jamii na hapo vitatumia njia ambayo iko nje ya uwezo wa mamlaka kudhibiti ...na hapa vitakuwa ni vyombo vya nje kupitia internet..wote tunatambua watazamaji wa mtandao wanavyoongeza mapato ya mitandao husika kwa idadi yake.
Leo hii YouTube (bombawewe/wewebomba) inatapika mapato kutokana na watazamaji wanaofuatilia kampeni za vyama vya siasa kama njia sahihi ya kupata updates za Uchaguzi.
Tunaua waandishi wetu njaa...tunavikosesha vyombo vyetu vya habari mapato....tunazotosha uchumi wa nchi...tunawanyima fursa ya kujifunza vijana wetu mashuleni na vyuoni kisa tu hatutaki wengine wasikike kuliko sisi
Uzalendo ni dhana pana sana....Uhujumu uchumi ni dhana pana pia...Na ukishindwa kuzitafsiri hizi dhana mbili katika uhalisia wake, unaweza kujikuta wewe ndio mhujumu uchumi number moja na raia namba moja asiye mzalendo na aliyekosa uzalendo katika nchi yake.
Na ukiachana na hayo mawili unajua matokeo yake ninini!? Ni kuzalisha wanahabari huru wasiodhibitiwa kimaadili na walio huru kupost chochote nje na ndani ya mipaka bila kikwazo....UASI HUWA NA VIASILI VINGI..