Tuko radhi kukosa mapato na kuipaisha YouTube kiuchumi huku Watanzania wenzetu wanahabari wakifa njaa?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
150,098
2,000
KUNA UZALENDO. Hii ni dhana pana sana hasa linapokuja suala la nchi.. Yeyote anayeweka maslahi ya taifa lake mbele kabla ya mengine yote huyo ni mzalendo nambari moja.
Maslahi kiuchumi
Maslahi kijamii
Maslahi kiusalama...nk nk
Uzalendo ni zaidi ya porojo majukwaani...uzalendo ni VITENDO na tafsiri sahihi isiyobagua kwa maslahi ya taifa na watu wake wote...!!!!

KUNA UHUJUMU UCHUMI...Hii nayo ni dhana pana pia...hasa linapokuja swala la uchumi wa nchi....Mhujumu uchumi si lazima awe mwizi wa mamilioni na kuyaficha kwa matumizi binafsi na familia yake...la hasha...Mhujumu uchumi ambaye automatically anahujumu pato la nchi ni yule kwa namna moja ama nyingine atasababisha pesa iliyopaswa kuingia kwenye kibubu cha taifa iende kwingine

Hata kitendo cha daktari kutoa matibabu bandia ni kuhujumu uchumi kwakuwa mgonjwa ataathirika zaidi na kutumia pesa nyingi zaidi kupata matibabu ambayo dawa nyingi tunanunua toka nje

Mhujumu uchumi ni yule afisa wa mamlaka ya mapato anayeidhinisha malipo ya leseni ya udereva kwa kijana asiyepitia shule ya udereva...! Huyu akienda kusabibisha ajali atapoteza wangapi? Wanaotegemewa na taifa na familia ngapi? Atajeruhi wangapi watakaotumia gharama kubwa kutibiwa? Atafanya uharibifu wa mali ngapi ambazo baadhi matengenezo yake yatahitaji vipuri toka nje?

Kipindi cha uchaguzi mkuu kinachotokea mara moja tu kwa miaka mitano ni kipindi muhimu mno kwa kila mmoja wetu na kwa kila kaliba kwenye jamii...ni kipindi ambacho kila mmoja anapaswa kushiriki katika nafasi yake... Ni kipindi cha kutengeneza historia na kujifunza mengi...

Kipindi cha uchaguzi mkuu ni kipindi cha mavuno kwa waandishi wa habari na wanahabari...
Taifa linakuwa na bajeti ya Uchaguzi
Vyama vinakuwa na bajeti ya Uchaguzi
Wagombea wanakuwa na bajeti ya Uchaguzi
Vyombo vya habari navyo hutenga bajeti zao kwa ajili ya Uchaguzi...hakika ni kipindi cha ahueni kubwa kwa wanahabari
Hawa huchaguiza mzunguko wa pesa kwa chochote kitu wanachopata
Wanaosemesha na kusoma watalipa ada
Wanaodaiwa kodi watalipa
Wenye madeni watalipa
Wenye viwanja na ujenzi watafanya manunuzi...nknk ...pesa inakuwa inazunguka ndani ya nchi....

Kwa Uchaguzi wenye vyama vingi ni ngumu kuzuiya jamii kuwa na fikra za chama kimoja kikatiba kimtazamo hata kimaono!
Kwa uchaguzi wenye vyama vingi itakuwa ni kukosa uzalendo na kusababisha uhujumu uchumi mkubwa kwa kuvitisha na kuvipiga pini vyombo vya habari visitangaze maono ya wengine.....kwa kufanya hivyo jamii itakosa msisimko...wanahabari watakosa cha kuripoti kwasababu ya woga na automatically watakosa mapato

Vyama navyo vitatafuta njia ya kuifikia jamii na hapo vitatumia njia ambayo iko nje ya uwezo wa mamlaka kudhibiti ...na hapa vitakuwa ni vyombo vya nje kupitia internet..wote tunatambua watazamaji wa mtandao wanavyoongeza mapato ya mitandao husika kwa idadi yake.

Leo hii YouTube (bombawewe/wewebomba) inatapika mapato kutokana na watazamaji wanaofuatilia kampeni za vyama vya siasa kama njia sahihi ya kupata updates za Uchaguzi.

Tunaua waandishi wetu njaa...tunavikosesha vyombo vyetu vya habari mapato....tunazotosha uchumi wa nchi...tunawanyima fursa ya kujifunza vijana wetu mashuleni na vyuoni kisa tu hatutaki wengine wasikike kuliko sisi

Uzalendo ni dhana pana sana....Uhujumu uchumi ni dhana pana pia...Na ukishindwa kuzitafsiri hizi dhana mbili katika uhalisia wake, unaweza kujikuta wewe ndio mhujumu uchumi number moja na raia namba moja asiye mzalendo na aliyekosa uzalendo katika nchi yake.

Na ukiachana na hayo mawili unajua matokeo yake ninini!? Ni kuzalisha wanahabari huru wasiodhibitiwa kimaadili na walio huru kupost chochote nje na ndani ya mipaka bila kikwazo....UASI HUWA NA VIASILI VINGI..
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
10,984
2,000
Sisi Chadema tunatuma Maombi Maalum kwa Mgombea Urais wa CCM Mzee Daktari bingwa wa kemia duniani Bwana Magufuli Kukubali Kuwa na MDAHALO na Mgombea Urais Wa Chadema Kamanda Tundu Lissu ili Kushindanisha SERA na Mitazamo Yao kwa Nchi Yetu Live kwenye TV na Redio Zote za Duniana na Wananchi Wote Watasikiliza!:
 
Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
2,688
2,000
Akikubali magufuri kufanya mdahalo na kichaa nitashangaa sana.
Hivi chadema hanjui kuwa mmesimamisha kichaa kugombea?? Huyo alishaasirika kisaikorojia , zile risasi hazikumuacha salama kiakili.

Labda tundu lisu wafanye mdahalo na mzee lungwe spunda mzee wa ubwabwa hapo nchi itasimama.
Kwani Kiswahili hajui, Kiingereza nacho mtihani Mkubwa, huyu Mhutu atafanya mdahalo kwa lugha gani?
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,723
2,000
Ukiachaga yale Mambo yako ya kutishana huwa una madini yakutosha .. nenda Sasa kabebe tutunguli fulani huko unakuja kutubadilikia..😂

Hata hivyo hongera umedadavua vizuri lkn pia waambie wale viongozi wasiotumia maneno yenye staha wanahujumu uchumi pia maana vyombo vya habari vipo kusikiliza hoja au sera za wagombea na si masimango au kejeli ama maneno yasiyostaha.. ni wakatii wa huyu tu ndo vyombo vibaniwe kwanini haikuwa kwa lowasa kipindi kile au dr slaa au mbowe ama mama Anna au rungwe..
Ni Jambo la kuwekana sawa tu.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,361
2,000
Sisi Chadema tunatuma Maombi Maalum kwa Mgombea Urais wa CCM Mzee Daktari bingwa wa kemia duniani Bwana Magufuli Kukubali Kuwa na MDAHALO na Mgombea Urais Wa Chadema Kamanda Tundu Lissu ili Kushindanisha SERA na Mitazamo Yao kwa Nchi Yetu Live kwenye TV na Redio Zote za Duniana na Wananchi Wote Watasikiliza!:
Mdahalo uwe wa wagombea wote sio hao wawili tu.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,361
2,000
Uzalendo na uhujumu uchumi ni dhana pana. Mifano ni;
Unapouza nyumba za serikali na kusababisha watumishi wapya, hasa walioteuliwa, waliopata uhamisho baada ya mauzo ya nyumba za serikali, kuishi hotelini wao na familia zao, serikali kulipia mabilioni ya hela kwenye hoteli binafsi kwa muda mrefu.
Unashiriki kwenye uuzwaji na kufilisiwa kwa mashirika ya umma na mali zake, unarudi baada ya miaka kadhaa na kutumia pesa za serikali kufufua na kununua tena mali ili shirika mliloliua lisimame tena, kuliendesha kwa hasara kwa kutumia pesa za walipa kodi.
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,948
2,000
Nimefatilia mikutano kadha ya wagombea Urais,simuelewi kabisa Magu anachoongea ukiachilia mbali watu kulazimishwa/kununuliwa kwaajili ya kusifia na kushangilia.
Watanzania tusipo jiongeza na kwenda mbali zaidi,tunaiangamiza nchi yetu kwa ujinga wetu.
Kuna hujuma za makusudi kuharibu uchumi wa nchi hii,uwe na mwelekeo wa kuneemesha wale tu wanaosujudia utawala na mateso kwa wale wasio sujudia utawala.Huu si uzalendo hata kidogo,ni uhujumu.
Mungu pekee asimame!
#NI YEYE
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
150,098
2,000
Ukiachaga yale Mambo yako ya kutishana huwa una madini yakutosha .. nenda Sasa kabebe tutunguli fulani huko unakuja kutubadilikia..

Hata hivyo hongera umedadavua vizuri lkn pia waambie wale viongozi wasiotumia maneno yenye staha wanahujumu uchumi pia maana vyombo vya habari vipo kusikiliza hoja au sera za wagombea na si masimango au kejeli ama maneno yasiyostaha.. ni wakatii wa huyu tu ndo vyombo vibaniwe kwanini haikuwa kwa lowasa kipindi kile au dr slaa au mbowe ama mama Anna au rungwe..
Ni Jambo la kuwekana sawa tu.
Unajaribu kwa umakini mkubwa sana kuuma na kupuliza...nimeandika kidogo sana na ndio maana nikasema hizo dhana mbili ni pana sana...hivi unatambua hata miradi mikubwa bila bajeti ni mojawapo ya uhujumu uchumi?
BTW uchawi siachi ndio unaniweka town..nakula vinono...natembelea makalio...halafu new brand tano kasarobo.....sefulikama bonus.....!!!
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
150,098
2,000
Uzalendo na uhujumu uchumi ni dhana pana. Mifano ni;
Unapouza nyumba za serikali na kusababisha watumishi wapya, hasa walioteuliwa, waliopata uhamisho baada ya mauzo ya nyumba za serikali, kuishi hotelini wao na familia zao, serikali kulipia mabilioni ya hela kwenye hoteli binafsi kwa muda mrefu.
Unashiriki kwenye uuzwaji na kufilisiwa kwa mashirika ya umma na mali zake, unarudi baada ya miaka kadhaa na kutumia pesa za serikali kufufua na kununua tena mali ili shirika mliloliua lisimame tena, kuliendesha kwa hasara kwa kutumia pesa za walipa kodi.
Taifa limehujumiwa pakubwa mno.......mikopo ya siri yenye riba isiyojulikana...mikataba ya siri kwenye miradi mikubwa...utawala wa sheria uliominywa ...maamuzi yaliyozingatia ushirikishwaji wa wananchi kupitia vyombo vyao.....nknk
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,723
2,000
Unajaribu kwa umakini mkubwa sana kuuma na kupuliza...nimeandika kidogo sana na ndio maana nikasema hizo dhana mbili ni pana sana...hivi unatambua hata miradi mikubwa bila bajeti ni mojawapo ya uhujumu uchumi?
BTW uchawi siachi ndio unaniweka town..nakula vinono...natembelea makalio...halafu new brand tano kasarobo.....sefulikama bonus.....!!!
We ni wakukuroga wewe..😅

Sawa nyie tuteseni tusionavyo tunaotembelea mamiguu.
Tena huwa tunalawama😂
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
150,098
2,000
We ni wakukuroga wewe..

Sawa nyie tuteseni tusionavyo tunaotembelea mamiguu.
Tena huwa tunalawama
KENZY kalale kidogo upumzishe meddula usiichoshe sana utaota unakimbizwa na wachawi halafu huna pumzi...ni uchovu tuu
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,723
2,000
KENZY kalale kidogo upumzishe meddula usiichoshe sana utaota unakimbizwa na wachawi halafu huna pumzi...ni uchovu tuu
😂😂 Unanikataza kujadili nawe unahujumu uchumi sahivi 6:53 nilale unini Sasa wakati kifurushi cha usingizi kkmefikia tamati..!

Ukae ujue wahujumu uchumi wapo wengi na kila mmoja wetu ktk namna yake alishawahi kuhujumu uchumi hata kutoa rushwa kwa kukwepa kulipa Kodi..
 
Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,221
2,000
Uzalendo na uhujumu uchumi ni dhana pana. Mifano ni;
Unapouza nyumba za serikali na kusababisha watumishi wapya, hasa walioteuliwa, waliopata uhamisho baada ya mauzo ya nyumba za serikali, kuishi hotelini wao na familia zao, serikali kulipia mabilioni ya hela kwenye hoteli binafsi kwa muda mrefu.
Unashiriki kwenye uuzwaji na kufilisiwa kwa mashirika ya umma na mali zake, unarudi baada ya miaka kadhaa na kutumia pesa za serikali kufufua na kununua tena mali ili shirika mliloliua lisimame tena, kuliendesha kwa hasara kwa kutumia pesa za walipa kodi.
Kwani aliuza akiwa rais? Kama waziri ana mamlaka kuuza. Siyo kwamba alipewa maagizo kutoka juu yake?
 
Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,221
2,000
Nimefatilia mikutano kadha ya wagombea Urais,simuelewi kabisa Magu anachoongea ukiachilia mbali watu kulazimishwa/kununuliwa kwaajili ya kusifia na kushangilia.
Watanzania tusipo jiongeza na kwenda mbali zaidi,tunaiangamiza nchi yetu kwa ujinga wetu.
Kuna hujuma za makusudi kuharibu uchumi wa nchi hii,uwe na mwelekeo wa kuneemesha wale tu wanaosujudia utawala na mateso kwa wale wasio sujudia utawala.Huu si uzalendo hata kidogo,ni uhujumu.
Mungu pekee asimame!
#NI YEYE
Nani anaeleweka katka hizi kampeni?
 
Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,221
2,000
KUNA UZALENDO...!!! hii ni dhana pana sana...hasa linapokuja suala la nchi....Yeyote anayeweka maslahi ya taifa lake mbele kabla ya mengine yote huyo ni mzalendo nambari moja...
Maslahi kiuchumi
Maslahi kijamii
Maslahi kiusalama...nknk
Uzalendo ni zaidi ya porojo majukwaani...uzalendo ni VITENDO na tafsiri sahihi isiyobagua kwa maslahi ya taifa na watu wake wote...!!!!

KUNA UHUJUMU UCHUMI...Hii nayo ni dhana pana pia...hasa linapokuja swala la uchumi wa nchi....Mhujumu uchumi si lazima awe mwizi wa mamilioni na kuyaficha kwa matumizi binafsi na familia yake...la hasha...Mhujumu uchumi ambaye automatically anahujumu pato la nchi ni yule kwa namna moja ama nyingine atasababisha pesa iliyopaswa kuingia kwenye kibubu cha taifa iende kwingine

Hata kitendo cha daktari kutoa matibabu bandia ni kuhujumu uchumi kwakuwa mgonjwa ataathirika zaidi na kutumia pesa nyingi zaidi kupata matibabu ambayo dawa nyingi tunanunua toka nje

Mhujumu uchumi ni yule afisa wa mamlaka ya mapato anayeidhinisha malipo ya leseni ya udereva kwa kijana asiyepitia shule ya udereva...! Huyu akienda kusabibisha ajali atapoteza wangapi? Wanaotegemewa na taifa na familia ngapi? Atajeruhi wangapi watakaotumia gharama kubwa kutibiwa? Atafanya uharibifu wa mali ngapi ambazo baadhi matengenezo yake yatahitaji vipuri toka nje?

Kipindi cha uchaguzi mkuu kinachotokea mara moja tu kwa miaka mitano ni kipindi muhimu mno kwa kila mmoja wetu na kwa kila kaliba kwenye jamii...ni kipindi ambacho kila mmoja anapaswa kushiriki katika nafasi yake... Ni kipindi cha kutengeneza historia na kujifunza mengi...

Kipindi cha uchaguzi mkuu ni kipindi cha mavuno kwa waandishi wa habari na wanahabari...
Taifa linakuwa na bajeti ya uchaguzi
Vyama vinakuwa na bajeti ya uchaguzi
Wagombea wanakuwa na bajeti ya uchaguzi
Vyombo vya habari navyo hutenga bajeti zao kwa ajili ya uchaguzi...hakika ni kipindi cha ahueni kubwa kwa wanahabari
Hawa huchaguiza mzunguko wa pesa kwa chochote kitu wanachopata
Wanaosemesha na kusoma watalipa ada
Wanaodaiwa kodi watalipa
Wenye madeni watalipa
Wenye viwanja na ujenzi watafanya manunuzi...nknk ...pesa inakuwa inazunguka ndani ya nchi....

Kwa uchaguzi wenye vyama vingi ni ngumu kuzuiya jamii kuwa na fikra za chama kimoja kikatiba kimtazamo hata kimaono!
Kwa uchaguzi wenye vyama vingi itakuwa ni kukosa uzalendo na kusababisha uhujumu uchumi mkubwa kwa kuvitisha na kuvipiga pini vyombo vya habari visitangaze maono ya wengine.....kwa kufanya hivyo jamii itakosa msisimko...wanahabari watakosa cha kuripoti kwasababu ya woga na automatically watakosa mapato

Vyama navyo vitatafuta njia ya kuifikia jamii na hapo vitatumia njia ambayo iko nje ya uwezo wa mamlaka kudhibiti ...na hapa vitakuwa ni vyombo vya nje kupitia internet..wote tunatambua watazamaji wa mtandao wanavyoongeza mapato ya mitandao husika kwa idadi yake....
Leo hii YouTube (bombawewe/wewebomba) inatapika mapato kutokana na watazamaji wanaofuatilia kampeni za vyama vya siasa kama njia sahihi ya kupata updates za uchaguzi....

Tunaua waandishi wetu njaa...tunavikosesha vyombo vyetu vya habari mapato....tunazotosha uchumi wa nchi...tunawanyima fursa ya kujifunza vijana wetu mashuleni na vyuoni kisa tu hatutaki wengine wasikike kuliko sisi

Uzalendo ni dhana pana sana....Uhujumu uchumi ni dhana pana pia...Na ukishindwa kuzitafsiri hizi dhana mbili katika uhalisia wake....unaweza kujikuta wewe ndio mhujumu uchumi number moja na raia namba moja asiye mzalendo na aliyekosa uzalendo katika nchi yake....!!!!!

Na ukiachana na hayo mawili unajua matokeo yake ninini!? Ni kuzalisha wanahabari huru wasiodhibitiwa kimaadili na walio huru kupost chochote nje na ndani ya mipaka bila kikwazo....UASI HUWA NA VIASILI VINGI...
Watanzania hata jirani akishikwa ugoni tunapeleka YouTube na tunaandika sana. Tatizo siyo uhuru wa vyombo vya habari. Taizo ni akili zetu tu. Hatujui tunachohitaji.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom