Tukiyahitaji maisha ya Libya enzi ya Gaddafi, hatuna budi kumpa nafasi zaidi Rais Magufuli

Nyerere aliyeamini katika ujamaa hadi kufikia hatua ya kufilisi na kutaifisha mali za matajiri akiamini matajiri ndio tatizo, lakini mwisho wa yote hayo ujamaa wake ulefeli na yeye akang'atuka bila kupenda.

Mwinyi pamoja na kuamini sera ya soko huru na yeye alishindwa kutokana na kuwa yeye alikuwa Rais lakini mmiliki wa nchi alikuwa mwingine..

Mkapa pamoja na kuwa alikuja na lengo zuri (kubana matumizi) na maneno yenye hisia tamu FUNGENI MIKANDA & ILI MGONJWA APONE MGONJWA HANA BUDI KUNYWA HATA KAMA DAWA NI CHUNGU, mwisho wa yote tulikaza mikanda na kunywa kila aina ya dawa lakini tulikaribisha magonjwa kama ;-
EPA, KAGODA, MEREMETA, RADAR nk.

JK na yeye tuliaminishwa kama chaguo la mungu na kina mama kumwita handsome, aliingia na gia ya ARI MPYA, NGUVU MPYA & KASI MPYA, matokeo yake yalikuwa ni tofauti na matarajio ya walio wengi na kilichotokea wote tunakijua.

TATIZO LETU NI MFUMO NA MFUMO UPO NDANI YA CCM, HIVYO ILI KUONDOA TATIZO BASI NA SHAKA NI LAZIMA TUHAKIKISHE TUNAUKATAA HUO MFUMO.
Unaposema mfumo, hapo mi natamani kuingia akilini mwako nami nijue unachokimaanisha. Ukoje huo mfumo mnaousema? Ccm iko tangu 77 je na huo mfumo upo tangu wakati huo? Je upo ktk katiba au sera za hicho chama (maandishi) au ni kwa watu tu ambao huzaliwa na kufa?
 
Acha uongo wewe! Angekuwa hana tamaa ya mali na kuichukia rushwa asingekuwapua nyumba za Serikali, asingekwapua bilioni 16 za wahanga wa tetemeko, asingetia rushwa ya milioni 10 kwa Wabunge wa MACCM asingelidanganya Bunge kuhusu upotevu wa mabilioni ya shilingi Wizara ya Ujenzi na pia asingenunua kivuko uozo cha mwaka 1978 kwa bilioni 8 na kikafanya kazi wiki tu sasa kiko juu ya mawe zaidi ya mwaka.
Je hapo suluhisho kamili ni lipi? Na je lipo ktk vyama vyetu, hapa namaanisha, kuna chama kinachoongozwa na chenye wanachama malaika? Kama tatizo letu ni ubinafsi wa watanzania, sisi wote ktk ngazi zote, je suluhisho ni lipi na linapatikana ktk vyama?
 
Suluhisho letu ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Haya mawili yatahakikisha chaguzi zetu zinakuwa huru na za haki ni hivyo Watanzania kama haturidhishwi na utendaji wa chama kilichopo madarakani tunakipiga chini chama hicho na kukiteua kingine nacho kikivurunda kinapigwa chini mpaka vyama hivi vianze kuheshimu Watanzania na kura zetu siyo kufuta matokeo ya uchaguzi kwa vile CCM imeshindwa au kuendelea kukumbatia katiba ambayo ni sawa na ya mfumo wa chama kimoja na kuwa na tume ya uchaguzi inayoteuliwa na Mwenyekiti wa MACCM.

Acha ujinga mtoa uzi unafananisha mbingu na dunia Gaddafi na magufuli wapi na wapi
Tofauti yao ni ipi mkuu? Tusaidie nasi tuelimike, Gaddafi hatukumjua vyema, uongozi wake ulikuwaje ktk nyanja kama za kiuchumi, kidemokrasia, kijamii na kiserikali.
 
Uchumi wa Libya ulikua imara serikali ilikua haina hofu maana alijenga misingi imara inayotoa ajira kwa vijana sera nzuri za ugawanaji wa rasilimali za nchi miundombinu bora kuwaunganisha walibya wawe kitu kimoja walibya walifurahia mafuta yao wote maana hakuwa mbinafsi na mchoyo wananchi hawakua na hali ngumu kiuchumi
 
Hamjambo,

Hali ya sasa libya unaipenda? Su bure umetumwa

Nafahamu majonzi aliyoyaacha Gadafi Libya baada ya kifo chake.

Wananchi wa Libya walipata huduma zote za kijamii free, wasio na ajira walilipwa posho, watu walisaidiwa kupewa pesa za kuanzisha familia mara baada ya kuingia kwnye ndoa. Yalikua ni maisha safi kwa Walibya wote.

Nawasihii Watanzania wenzangu, tumssuport Mh. Rais wetu Magufuli namuona akituandalia maisha ya Libya chini ya Gadafi miaka inayokuja.

Tumpe muda akimaliza hii 10, si mbaya tukamuongezea hata mitano mingine.

Nina Imani nae.
 
Suluhisho letu ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Haya mawili yatahakikisha chaguzi zetu zinakuwa huru na za haki ni hivyo Watanzania kama haturidhishwi na utendaji wa chama kilichopo madarakani tunakipiga chini chama hicho na kukiteua kingine nacho kikivurunda kinapigwa chini mpaka vyama hivi vianze kuheshimu Watanzania na kura zetu siyo kufuta matokeo ya uchaguzi kwa vile CCM imeshindwa au kuendelea kukumbatia katiba ambayo ni sawa na ya mfumo wa chama kimoja na kuwa na tume ya uchaguzi inayoteuliwa na Mwenyekiti wa MACCM.
Inawezekana ikawa sawa, kwakuwa katiba ndo sheria mama ya nchi husika. Ila kipi kibebwe na hiyo katiba mpya? Hapo ndo kiini cha swali langu. Serikali 3,mgombea huru, tume huru, mahakama huru, bunge huru,majimbo nk ndo suluhisho la yote haya? Watanzania wengi wanalalamika na ubinafsi wa wenye nafasi, (ufisadi, kukosa uzalendo, uvivu au kutokuwajibika nk) je hayo yatatibu yote hayo? Tufikiri kwa kina kwanza hapa, inachukua miaka mingi katiba kurekebishwa, tufikiri kipi ni tiba haswa?
 
Hayo magonjwa yote uliyoyataja tiba yake imo ndani ya rasimu ya Tume ya Warioba Mkuu. Hivi viswahili swahili vya kukingiana kifua ili kulindana, "Sifukui makaburi ya zamani" ndani ya rasimu ya Tume ya Warioba havina na nafasi ukizembea umekwenda na maji na Bunge linaweza kabisa kukuondoa madarakani kwa kutokuwa na imani na utendaji wako, badala ya hali ilivyo hivi sasa mtu anaonekana kabisa utendaji wake ni janga la Kitaifa lakini hakuna lolote linaloweza kufanywa dhidi yake inakuwa kama ni mfalme vile hata akivurunda vipi hakuna wa kumgusa mpaka amalize awamu yake au awamu zake..

Inawezekana ikawa sawa, kwakuwa katiba ndo sheria mama ya nchi husika. Ila kipi kibebwe na hiyo katiba mpya? Hapo ndo kiini cha swali langu. Serikali 3,mgombea huru, tume huru, mahakama huru, bunge huru,majimbo nk ndo suluhisho la yote haya? Watanzania wengi wanalalamika na ubinafsi wa wenye nafasi, (ufisadi, kukosa uzalendo, uvivu au kutokuwajibika nk) je hayo yatatibu yote hayo? Tufikiri kwa kina kwanza hapa, inachukua miaka mingi katiba kurekebishwa, tufikiri kipi ni tiba haswa?
 
Hamjambo,

Nafahamu majonzi aliyoyaacha Gadafi Libya baada ya kifo chake.

Wananchi wa Libya walipata huduma zote za kijamii free, wasio na ajira walilipwa posho, watu walisaidiwa kupewa pesa za kuanzisha familia mara baada ya kuingia kwnye ndoa. Yalikua ni maisha safi kwa Walibya wote.

Nawasihii Watanzania wenzangu, tumssuport Mh. Rais wetu Magufuli namuona akituandalia maisha ya Libya chini ya Gadafi miaka inayokuja.

Tumpe muda akimaliza hii 10, si mbaya tukamuongezea hata mitano mingine.

Nina Imani nae.
Pole sana,
Gadafi alifadhili magaidi duniani na madikteta afrika. Alikuwa dikteta nchini kwake. Ndio unaoutaka hapa ili mradi uwe unalambishwa vihela.
 
Muleta mada acha kumchafua marehemu Gadafi kwa kumufananisha na Rais wa CCM.
 
Back
Top Bottom