Mipangomingi
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 2,713
- 2,058
Kwa kiasi fulani yes, katiba mpya itakayotoa haki, uhuru na uwajibikaji ndio msingi na tiba bora ya matatizo karibu yote hayo. BAK yuko sahihi. Ubinafsi, ufisadi, uvivu, kukosa uzalendo,sifa, kujikweza nk, vyote ni sehemu ya tabia ya mwanadamu yanayotokana na utashi wa akili yake au mazingira aliyoishi au anayoishi. Katiba moja kati ya jukumu lake kubwa ni kuondoa na kuzuia/limits matumizi ya akili inayotoa utashi wa kufanya mambo hayo. Kwasababu katiba itabainisha mipaka kwa kila kitu hapo.Inawezekana ikawa sawa, kwakuwa katiba ndo sheria mama ya nchi husika. Ila kipi kibebwe na hiyo katiba mpya? Hapo ndo kiini cha swali langu. Serikali 3,mgombea huru, tume huru, mahakama huru, bunge huru,majimbo nk ndo suluhisho la yote haya? Watanzania wengi wanalalamika na ubinafsi wa wenye nafasi, (ufisadi, kukosa uzalendo, uvivu au kutokuwajibika nk) je hayo yatatibu yote hayo? Tufikiri kwa kina kwanza hapa, inachukua miaka mingi katiba kurekebishwa, tufikiri kipi ni tiba haswa?
Angalia kilichotokea Brazil au Korea.
Hisia za rushwa zilipowafikia wananchi, na kubaini kuwa watu hao waliruhusu matumizi ya akili zao kinyume na maslahi ya taifa haikuwa shida kuwakumbusha( kupitia mfumo wa kuwaondoa uliowekwa na katiba zao).
Akili za kibinaadamu ikiwa pamoja na ubinafsi, wizi, matumizi yasiyofaa ya madaraka, uzinzi nk-nk yote yanahitaji sheria ambayo ni deterrence, punishable and enforceable bila kubagua nani au wa cheo gani. Uchaguzi ni moja kati ya deterrence and punishment ambapo wananchi wakiona hawaridhishwi na usimamizi wa wenye dhamana, wanatumia sanduku la kura kuwaadhibu na hivyo walio madarakani kwa kuogopa kuadhibiwa wanalazimika kuwajibika ipasavyo. Kwa msingi huo, ikiwa wanaopaswa kuadhibiwa kwa sanduku la kura wanajua hawawezi kuadhibiwa, uchaguzi unakuwa si deterrent tena na unakuwa hauna maana yoyote.
Kiongozi yoyote mwenye mema na anachokiongoza, mpime kupitia utayari wake wa kuondoka/kuachia madaraka. Ukiona kiongozi anaweka mifumo complex (na isiyoendana na uwajibikaji) ya yeye kutoondoka madarakani, hapo inabidi ujenge shaka kubwa, WHY? Kiongozi anatakiwa aruhusu wapiga kura waamue, na maamuzi yao yabaki hivyo hata kama kura zutahesabiwa mbele ya Malaika au Mungu muumba wa vyote.
Hivyo tume ambayo inaamua kwa haki matokeo ya wapiga kura ni jambo ambalo muhimu, kinyume cha hapo itakuwa tunajiongopea wenyewe na matatizo yote hayo hayatapungua abadan wachilia mbali kuondoka.