Tukiwa na wabunge watano wa hivi nchi itakuwa hatarini eti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukiwa na wabunge watano wa hivi nchi itakuwa hatarini eti!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dijovisonjn, Mar 19, 2012.

 1. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama makini, kikongwe, chenye uzoefu na sera nzuri sana tofauti na chama chochote kile hapa Tz lakin tatizo kubwa la CCM huwa ni viongozi wake, pamoja na CCM kuwa na wataalamu na wasomi wengi lakini ina viongozi ambao wakiongea lazima mtu ujiulize mara mbili mbili kama kiongozi huyo kweli alisimama mbele ya umati wa watu na kuwashawishi kumpa kura.

  Tatizo la viongozi kama hawa sio kwamba wapo CCM tu bali hata vyama vingine wapo tena wengi tu (haswa wale wa viti maalumu) ila kwa CCM is too much jaman (sio kwamba naishambulia CCM bali najaribu kuwaomba kuwa makini na wale mliowateua au kuwachagua, hebu soma hii habari kutoka gazeti la Mwananchi then ntaongea kitu.

  WANANCHI wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wameombwa kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Sioi Sumari ili kumfuta machozi yaliyotokana na kifo cha baba yake mzazi, Jeremiah Sumari ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

  Mbali na hilo wananchi hao wameelezwa kuwa kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejipatia baraka kwa Mungu kwani watamwezesha Sioi kupata mshahara utakaomwezesha kuendesha familia aliyoachiwa na baba yake.

  Mwito huo ulitolewa juzi katika Kijiji cha Migadini, Kata ya Mororoni na Mbunge wa Mtera(CCM), Livingstone Lusinde alipokuwa akimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzimdogo zinazoendelea jimboni humo.

  Lusinde alisema wananchi hao wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua kwa kura nyingi ili ajipatie mshahara wa kumwezesha kumudu familiaaliyoachiwa na marehemu baba yake, ikiwa ni moja ya njia ya kumfuta machozi.

  ¡°Mkimchagua Sioi mtapata baraka za Mungu kwa vile mtakuwa mmewezesha kutokea kwa mambo matatu¡* kwanza kura zenu zitamfuta machozi ya kufiwa na baba yake, pili mtamwezesha kupata mshahara utakaomwezesha kulea familia yake ambayo sasa haina baba,¡± alisema Lusinde.

  Pia aliwaambia wananchi hao kwamba kumchagua Sioi kuwa mbunge wa jimbo hilo ni kumfurahisha Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye chaguo lake na ndiye aliyeongoza vikao vya Kamati Kuuiliyokutana mara mbili kupitisha jina lake kuwa mgombea wakati wa mchakato wa kura za maoni.

  Alisema katika kura hizo za maoni zilizofanyika mara mbili, zote Sioi alionekana kushinda na kuibuka kidedea.
  ¡°Njia pekee ya kumfurahisha Raisni kumchagua Sioi kwa kuwa ni chaguo lake, hakika mtamfurahisha na Sioi ataweza kutekeleza vyema ilani ya chama,¡± alisema Lusinde....

  My take.
  Kama kiongozi anawashawishi watu wachague kiongozi kwa sababu eti amefiwa na baba yake, wamchague ili apate ajira ili aweze kutunza familia yake na wamchagua ili waweze kumfurahisha mtu fulani, kiongozi huyo hatufai na hata huyo anayepigiwa debe pia hatufai.
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kiongozi huyu anatoa mtazamo wake Na ulio ndani ya viongozi wenzake kwamba Kwao Ubunge si daraja la wananchi Na serikali Yao Bali ni ajira, mlo Na kutunza wa kwao. Na ndio sababu kuu kwamba wabunge wengi wa Chama chetu hiki ni wabinafsi, mafisadi Na makatili Kwa wananchi wao. Look here Sioi, mwanasheria Wa BOT, mfanyakazi wa benk, Mtu mwenye Mji wake huko DSM, Leo anapigiwa debe apate ajira Kwa ugali Wa marehem baba yake? Je wananchi Wa kawaida waliofiwa Na wazazi wote wawili wasemeji Kwa hili.,
  Hatulaumu kila kauli za viongozi wetu hawa ila wao ndio sababu ya sintofahamu juu ya uwezo Wa akili za kujieleza walionao wenzetu hawa. Juzi jamaa mmoja karopoka 'kitu' kuhusu mambo ya kifamia ya marehem bosi wake, kauli inayomghalim misamaha kila kukicha, mwingine mzee Wa kuchapa miusingizi Bungeni nae kajiropokea kauli anazozijutia , huyu nae kaja Na viroja vingine..
  Nadhani Kwa kuwa Kampeni zilifinguliwa Kwa kiongozi wetu kuropoka, nadhani mtindo Wa uropokaji utakizika Chama chetu jamani.. Kuna Mtu mkubwa kwenye Chama hili alisema Kama utani kwamba CCM itakuwa ya nne au tatu ikijitahidi, usemi ambao naanza Kama kuukubali.
  Kuna mdudu anakitafuna Chama Na dawa yake ni rahisi ila ngumu sana kutekelezeka.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hili kweli linazidi lile la za Vicent Nyerere kuacha kunadi sera na kuanza kumulaumu mungu kwa kutokana na kifo cha Marehemu Baba wa taifa kwa kisingizio kuwa liuawawa?
   
 4. M

  Mbuki Feleshi Senior Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwan kunawatanzania wangapi kila kukicha wanapoteza mihimili ya familia zao kwa vifo na sababu nyingine nyingi?! Kweli tukisema tuwakusanye watu wooote hawa tuwape ubunge patakuwaje pale Dodoma? Je watakuwa ni wabunge wa wananchi walochaguliwa kutekeleza majukumu yale matatu ya mbunge kwa mujibu wa katiba yetu...au watakuwa wabunge wa watu walofiwa na babazao?!!! Ila ni vyema limekuja katika wakati muafaka, wakati ambapo watanzania tupo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya....inatia hasira sana
   
 5. kijenge

  kijenge Senior Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Ndugu yangu unapata tabu bure kuwazia watu kama hao,na masaburi alishasema wabunge wengi wa magamba wanafiri kwa kutumia makalio na huyo ni mmoja wao.wenzao wanakaa usa wao wanaka mount meru hotel na ngurudoto.mchemba ye2 na machangudo.kweli ccm hajui walichofata arumeru.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hayo maneno yametoka kwa binadamu mwenye akili timamu?
   
 7. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  binafsi naamini kili ni zaidi ya hlo.
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii ni dharau na dhihaka kwa wameru na wananch wote.
   
 9. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe umeona mmoja tu...wapo zaidi ya hao watano unaowataka wewe...wengi wao wanamawazo mfu kabisa...Lusinde ni mmoja kati ya watu waliokwenye list yangu ambao ninamashaka kama wananchi wa Tanzania hii kweli waliwachagua....hafai mi nadhani ameenda arumeru kumpuguzia kura "haoi"....
   
 10. kijenge

  kijenge Senior Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
   
 11. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Nadhani atakuwa ni binadamu mwendawazimu,kwa hiyo sumari haendi bungeni kuwakilisha wana Arumeru, bali anaenda kuwakilisha tumbo lake na familia yake,kweli CCM ni mzigo kwa taifa.
   
 12. K

  KIGIGI Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wala siwezi kumshangaa Lusinde ndivyo alivyo. Ashukuriwe sana kurahisha kifo cha magamba!
   
 13. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,929
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  Tusimlamu Lusinde,huo ndio ukomo wa fikra zake
   
Loading...