Tukishindwa vita hii ya madawa ya kulevya hakika tumeshindwa sote

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,666
8,510
Sio Makonda wala mimi tu sote tutakuwa tumeshindwa isipokuwa wauzaji, wanufaikaji na watumiaji ambao watashangilia na kutanua huku watoto wa wanyonge wakizidi kuathirika na kubaki mateja.

Ukiukwaji wa taratibu au sheria kama kweli umejitokeza basi usiwe ''Kichaka'' cha wana mtandao kujinasua, kujisafisha na kujiimarisha zaidi, kamwe tusiruhusu wachomoke kwa mwanya, tuwafikishe watuhumiwa wote mahakamani ambapo ndio mahali pekee pakutoa haki.

Sioni mantiki ya watuhumiwa kudai eti ''wamechafuliwa'' wakati tuhuma zao hazijafikishwa mahakamani huu ni ujanja wa kumteza nguvu.
 
Nasubiri tamko, la kwamba, Tanzania imeshinda vita dhidi ya malaria kwanza.. ndio nianze kufikiria kuhusu madawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom