TUKISHAJENGA ACADEMY ZA YANGA KWENYE KILA MKOA KINACHOFUATA NI KUANZISHA LIGI YA HIZO ACADEMIES

BENEDICT BONIFACE

Senior Member
Aug 31, 2013
113
225
Kwa mfano ndani ya miaka mitano tukiwa tumefanikisha kujenga academy kwenye kila mkoa, vijana wa kike na wa kiume kutoka kwenye mkoa husika watajiunga na hizo academies, watalipa ada ambayo itasaidia kuongeza mapato ya club na kusaidia gharama za uwendeshaji wa hizo academies. Itaandaliwa ligi ya vijana wa U8, U10, U12, U14, U15, U17 ambapo vijana hawa kutoka kwenye hizo academy kutoka kila mkoa watashindana na mshindi atapewa zawadi na bonus zingine. Wale wachezaji bora watakaoonekana kutoka kwenye hizo ligi wakusanywe kwenye academy ya kitaifa ya yanga itakayounda timu zitakazoshiriki kombe la Tff la chini ya miaka 15 na U17.Nafikiri tukishafanikisha hili hatutakua na ulazima wa kununua wachezaji wengi kutoka nje ya nchi na kisoka Tanzania itakua haikamatiki barani Afrika.

Hakuna linaloshindikana chini ya jua

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom