onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,346
- 1,303
Amani na utulivu huvunjwa na wahubiri wake. Inapotokea mhubiri akatoa hubiri kusisitiza jambo halafu yeye akaenda kinyume chako basi matokeo lazima yawe hasi. Ukihubiri amani halafu ukaanza kuwa katili unaowahubiri watakuwa wakatili kuliko wewe. Tujifunze kuishi maneno tunayatamka kwenye mahubiri.
Kampeni zilizoanza jana ziwe za kistaarabu na amani. Polisi wafuatilie hao vijana wanaosadikiwa kuandaliwa kuteka ,kuua na kuumiza watu. Sera na ilani safi siyo kulaximisha na kutoa roho za watu. Vyombo huru za habari kemeeni la sivyo wanasiasa wanaweza kuchoka na kutoa matamko ya kulipiza kisasi. Mbona viongozi wetu mnatupeleka kubaya. Kama wewe ni DC unawatumia vijana kumfurahisha aliyekuteua basi ujue sisi hatufurahishwi na wala hatupendi kuumizwa. Tufanye kampeni kwa amani