Tukipiga marufuku majenereta na matanki ya "SIMS", tutatatua tatio la umeme na maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukipiga marufuku majenereta na matanki ya "SIMS", tutatatua tatio la umeme na maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 27, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mnafikiri ni kwa haraka kiasi gani watawala wetu watajaribu kutatua tatizo la umeme na maji endapo majenereta na matanki ya maji yatapigwa marufuku mijini? I bet you very soon...wouldn't you agree?
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Ni kweli tangu 1994 wakati wa mgawo mkuu wa umeme, ndo watu walipogundua kuwa majenereta ni dili. Lakini naamini kuwa kupiga marufuku majenereta hakutaondoa tatizo la msingi la wabongo la ufisadi. Utapiga marufuku watabuni mbinu nyingine ya ufisadi.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hofu yangu ni kuwa matajiri na watu wenye uwezo hawasumbuliwi na tatizo la nishati na maji kwa sababu they can afford the alternative...
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kuna mambo mengi yanayofanana majenereta na matanki ya maji. Kukiwa na matatizo ya shule, mtu anatafuta pesa ampeleke mtoto wake shule nzuri ya kulipia. Wakati wa zamani shule ya kulipia walikwenda waliokosa nafasi shule za umma. Barabara zikiwa mbovu, mtu anataka kununua SUV, shangingi. Na vitu vingine vinasababisha sehemu fulani ya inflation.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Wa kuyapiga marufuku ni nani kama si hao hao watawala wenyewe?
   
 6. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  HAITAKAA IWEZEKANE BANA!!

  Tanzania bila ya ufisadi na rushwa hiawezekani (hasa kwa serikali hii ya JK)
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  unajua kama jua haliwapigi wao unafikiri wanasumbuka kuona wengine wanapata vivuli? Mimi naamini ni kama template fulani hivi inatumika. Yaani, kwa mfano lile la taasisi ya Moyo.. shule zetu na hata kwenye jeshi la polisi.. can you imagine kuna mashirika ya kuzima moto ya binafsi yanayofanya kazi ya umma kwa malipo? Hata Polisi imefikia kuwa na ubinafsishaji wa aina fulani..
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni template na ambayo ina-negative impact kubwa sana kiuchumi. Mtu mmoja anapokuwa na jenereta na akaongeza comfort yake, basi hata jirani yake ambaye kipato chake sio kikubwa atataka kuwa na jenereta. Hivyo jirani ataiba au kwa lugha ya sasa kufisadi kwa kiwango cha chini. Na ununuzi wao utaongeza demand ambayo itafanya atokee supplier ambaye atatumia pesa ya kigeni kuagiza jenereta kutoka nje ya nchi. Matokeo ni kuongeza demand ya dollar na kuwa na currency ambayo sio stable.

  Kwa maoni yangu binafsi sioni sababu ya form six anayefanya TRA kupata mshahara mkubwa kuliko university professor. Ukiangalia kwa undani hili mtu wa TRA asiibe inabidi alipwe mshahara utakaomwezesha kununua simm tank, jenereta n.k

  Na kuhusu wao kutopigwa na jua, huo ni ulimbukeni tu.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Fikiria mlolongo wa hili ulivyo:

  Nunua jenereta
  Nunua mafuta
  Nunua spare parts


  Lakini jingine ni kuwa unaweza ukakuta nyumba ina jenereta kubwa na lina uwezo hata wa kugawa umeme kwa jirani lakini hakuna utaratibu ambao ungeweza kuhakikisha utaratibu wa kuunganisha majirani. Matokeo ni kuwa jirani na jirani wana umeme wa kutosha kwenye majenereta ambao wangeweza kutangeneza hata ka network fulani hivi.. maana nimewahi kuona jamaa anayo yale ma industrial generators kwa matumizi ya nyumbani..
   
 10. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Swala la nishati na madini linaendeshwa kisaani humu nchini kwetu hadi hapo tutakapo kurupuka na kujua ni kipi cha kufanya. Bila kuitikisa seriklai ni sawa na kutwanga tu maji kwa kinu. Sera ni mbovu hazi wezi kutuletea maendeleo kamwe Umeme utakuwa wa mgao tuu siku zote mfano mzuri mpaka leo watanzania wengi hawajui chanzo cha mgao huu bali wachache wanasikila kuwa kuna tatizo la vipuli vimeharibika huko Dar sasa kwanini huku mikoani tukumbwe na hilo tatatizo la umeme je ingekuwa ni mwanza wana tatizo hilo je Dar wange wekwa kwa mgao nao???

  Kama Tanesco wanashindwa tuu kuagiza Transformer tokea Tanelec Arusha ambako zinatengenezwa na kubadirishi ile iliyo haribi mfano hapo masaki labda ianawachukua miezi 2. Haliingii akilini kabisa
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  Proposal iliyoko kwenye title ya thread inaangalia zaidi symptoms. Is it sustainable? Not quite...I will say.

  Mzuie mlevi kunywa bia..... atatengeneza gongo mwenyewe (uliza watu wanaoishi maeneo fulani kule UAE).
  Mlevi hata petroli atakunywa.

  Solution ya tatizo hili is one radical bing-bong....so for starters, ditch those pretenders currently occupying that Magogoni house.
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  interesting thinking...ivi umeme kutoka makampuni binafsi ni marufuku?
  sidhani kama ku-ban majenereta itawezekana!dawa ni kuja na alternative means ya ku-dili na hii ishu! kuanzisha kampuni binafsi inaweza kuwa moja ya alternatives!
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mi mwenyewe na mpango wa kuanzisha duka la vifaa vya majenereta Dar nzima hakuna likiloga ndo basi tena.
  Kufa kufaana hapo
   
 14. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Wala tatizo si transformer mkuu hii ilikuwa ni kisingizio cha kwanza, jana nilimsikia msemaji wa Tanesco dada mmoja nafikiri ni Badru Masoud kama sikosei. Sababu alizozitoa zinakatisha hata tamaa, mgao si wa leo wala kesho, huu tunao na huenda tukamaliza nao mwaka.


   
 15. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naungana nawe Chapakazi, dawa ni kuishinikiza Serikali iache ukiritimba kwenye huduma hii, iruhusu makampuni binafsi yaingie, yazalishe na kusambaza umeme kama zilivyo kampuni za simu! Haja jeuri ya TANESCO itakwisha kama TTCL!
   
 16. H

  Haika JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  ni maajabu sana, kuwa badala ya wenye bajeti kuimarisha zimamoto, wanakodisha binafsi ha hela ya kulipa inapatikana!!! haya yanawezekana Tanzania tu!! nikati ya sife zetu maalum za pekee
   
 17. T

  Tom JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Toka lini serikali yetu ikawa na ufanisi kwa lolote? Hata wakiamua kupiga marufuku (kwa raia) wala hawatafanikiwa kuleta umeme wala maji na haitapita muda wataacha hayo majenerata na matanki yarudi kinyemela. Labda ni pale tu watapojua kua bila luleta umeme na maji watakosa kushika serikali, lakini ubabe wao bado unawahakikishia kushika serikali.
  Inanikumbusha historia yetu pale ambapo mashamba ya binafsi yalipopigwa mkwara ili mashamba ya vijiji yaendelee - bado vijiji havikuimarika.
   
 18. T

  Tom JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si ajabu, wanasababu nzito na watakuambia FIRE wanaiba spea na mafuta. Kazi ya kukodi ni rahisi kuliko kazi ya kusimamia kuimarisha hizo zimamoto.
  Chukulia kua pesa ipo: Pia ni kazi rahisi kufikiria na kuchimba visima vya maji Dar kuliko kujenga mtandao wa mabomba ya mji toka Mto Ruvu ama Rufiji, pia rahisi kufikiria na kununua SUV ili waheshimiwa waweze kupita kwenye barabara zisizopitika. Ndivyo walivyo kwenye serikali yetu ama ndivyo tulivyo - tunapenda kilicho rahisi kufanya leo ili kupooza tatizo kwa leo, ya kesho tutajua kesho. Ni ubinafsi pamoja na akili finyu katika kuendesha shughuli zetu.
   
 19. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Wakati kampeni zinaanza, kuna jamaa alidai ataipigia kura ccm, ili aendelee kuuza maji ya kisima alichochimba.

  ...Point yake ikiwa;ku-maintain status quo kunampa ulaji mzuri.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni kufikiria jinsi gani jamii hasa watendaji wetu wakubwa wa serikali ambao kwao umeme siyo tatizo wala maji siyo tatizo wataona umuhimu wa kutafuta suluhisho? Watu binafsi sina tatizo kabisa wao wanapata vipi umeme lakini watendaji wa serikali (nafikiria wale wa Tanesco) hili kweli hawana majenereta majumbani kwao na hivyo umeme unapokatika wao wenyewe haiwagusi?
   
Loading...