falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,287
Jana gari yangu aina ya coaster mayai inayopaki ma external ilikodishwa pamoja na coaster zingine mbili jumla zikawa tatu,kusafirisha msiba kutoka tabata kuelekea ileje mkoa wa songwe umbali wa mita kadhaa kufika mpaka wa malawi.
Safari ilianza vizuri majira ya saa tisa mchana huku gari yangu ndio ikiwa imepakia mwili wa mwendazake,basi tulijitahidi kutembea kwa kasi japokua tulikua na vituo vingi vya kusimama.
Ilipofika saa nane tulikua mpakani mwa mafinga na makambako porini huku eneo hilo likiwa linaendelea na ujenzi wa upanuzi wa barabara gafla kwenye mteremko mkali wenye kona nikakuta mawe makubwa manne yamepangwa katikati ya barabara huku penye nafasi ndogo ya kupita ilikua imesimama toyota cresta na pembeni palikua na noah,hali iliyopelekea kutumika kwa akili ya haraka sana ya kuingiza gari mtaroni na kuforce ipite kwenye barabara ya rough road na kurudi tena barabara kuu baada ya kukosa kuanguka(thanks god)
Basi ndipo ile gari ndogo ilipogeuza na kuanza kutufukuza kwa kasi huku zile coaster zingine zikiwa nyuma umbali wa dk 20,basi tulifukuzana kwa muda wa nusu sasa kwa mtindo wa kuyumbisha gari ili ile gari ndogo isitupite huku tukipishana na gari zingine bila kujua kinachoendelea,basi baada ya dk 40 hatimaye tukapata sehemu ya kuingiza gari kwa kasi ili kupata kupata msaada .
Cha kushangaza zaidi kipindi hicho chote hatukupata msaada kutoka kwa askari wa eneo husika licha ya kupigiwa simu njia nzima.
Zile coaster mbili zilitukuta makambako nusu saa baadae tumepaki kwenye kituo cha mafuta ndio tukaendelea na safari
Sasa hapa nikifanya comparison fupi ni kwamba serikali ya kenya imejidhatiti zaidi kuwalinda raia wake licha ya changamoto mbalimbali,kenya huwezi kutembea umbali mrefu vile bila kupishana na polisi wakiwa kwenye patrol
Wanajamiiforums wenzangu tuliokua nao safari moja ya msibani watakuja hapa kulaani vikali uzembe wa jeshi letu la polis