Tukio lililotokea mwezi uliopita linanithibitishia kuwa "binadamu wote ni sawa ila hatupo sawasawa"

Mimi nimeapa kutopiga mwizi ,na kama kuibiwa nimeibiwa kwelikweli kuanzia nyumbn wakati naishi kwetu tulivamiwa na wezi zaidi ya 15 waliiba kila kitu ,wakat naanza maisha pia nilivunjiwa gari yangu my 1st car waliiba taa ,power window ,side mirrors....urembo wa dashbord lakini haijastify mimi kupiga mwizi ,coz naogopa nisije ingia kwenye makosa ya kudhulumu nafsi ya mtu
Mwezi uliopita majira ya saa 9 usiku zilisikika kelele kutoka kwa majirani wakisema "mwizi, mwizi"

Japokua nilisikia hizo kelele lakini sikutaka kutoka nje moja kwa moja kwasababu ni risk sometimes na hii nimejifunza baada ya tukio baya lililomtokea ndugu yangu.

Wakati niko ndani nikasikia sauti nje ikitokea kwenye ile nyumba iliyokua ikipiga kelele za kuita mwizi kuwa "aah wana bahati wamekimbia siku nyingine watakuja kufa kijinga"

baadhi ya majirani waliamshwa na ile sauti na ikabidi kuwauliza waliokua wanaita mwizi nini kimetokea. "Kuna wezi walikua dirishani wanataka kuiba na ndio maana tumeita mwizi"

Basi mimi niliposikia hivyo nikaona haina sababu ya mimi kutoka nje kama mwizi kasepa na hakuna alichoiba so ikanibidi niuchape usingizi tu.

Kesho yake tena majira ya saa 10 na robo usiku nyumba ile ile tena nikasikia kelele za kuita mwizi. Round hii nikachomoka na kinondo flani hivi huwa nakiweka nyuma ya mlango nikafungua geti ili niweze kukabiliana na huyo mwizi.

Katika hali isiyo ya kutarajia nikaona yule aliyeitwa mwizi anakuja kwangu na wakati huo mimi nipo getini bado sijafunga hata geti.

Huyo aliyekuwa akiitwa mwizi alikimbia na kuingia getini kwangu huku mimi nikiwa nimeduwaa. Kivipi mwizi akimbilie ndani mwangu wakati humu si sehemu salama kwake yeye wakati akijua kua itawarahisishia wananchi kumpiga kwa uraisi kwa sababu hatakua na sehemu ya kukimbilia.

Ikabidi nimfuate lakini nilishtushwa na sauti yake "Scars wananiua bure mi sio mwizi"

Nikataharuki kwa mshangao mkubwa kwasababu sauti hiyo ilikuwa si ngeni masikioni mwangu. Hapo ndipo nilipomsogelea kwa ukaribu na nikapata kujua kuwa yule ni mshkaji wangu wa kitaani.

Wakati huo alikuwa amelala chini huku damu zikimvuja kama maji, aah nilidata nikajikuta namuuliza maswali ambayo yalikuwa yananitatiza "daah mwanangu imekuaje umekuwa mwizi na mtaani wote wanakujua kuwa wewe ni fundi"?

Jamaa alijibu kwa shida sana maneno yake yalisikika kwa mbali kama mtu anayeweweseka, "Scars nilipigiwa simu kuwa kuna kazi inabidi nikaifanye na ndo maana nimejihimu asubuhi ili kuepukana na foleni maana kazi naenda kufanyia mbali. Lakini nilipofika hapa nashangaa wamenivamia na kunichoma visu kuwa mimi ni mwizi japokuwa niliwaambia kuwa mimi ni kijana wa mtaa huu huu"

Hapo nikaona niwaite vijana makamo yangu tusaidiane kumbeba mshkaji kumpeleka hospitali

Tulivyokua tunamnyanyua pale chini ndipo tulipobaini kuwa jamaa kashambuliwa vibaya sana. Shingoni kulikuwa na kitobo ambacho kilikuwa kinavuja damu ambazo zilimfanya akose nguvu ya kusimama peke yake.

Tukamchukua mpaka dispensary ya mtaani hapa ili aweze kupata matibabu ya huduma ya kwanza lakini wauguzi hawa hawakumhudumia chochote ndugu yetu wakatuambia tumpeleke Amana huku tukifuatilia PF3.

Tukakodi bajaji fasta fasta tukampakia huku akiongozana na kaka yake kuelekea hospitali ya Amana. Huku mimi nikirudi home kusafisha mazingira ya pale maana damu ilitapakaa ndani kiasi cha kufanya paonekane kama ni Vingunguti.

Majira ya saa 4 asubuhi tuliletewa taarifa kua jamaa kashafariki na ukweli halisi ni kwamba jamaa kauliwa kimakosa. Waliyemdhania kuwa ni mwizi alikimbia na walipotoka kumkimbiza wakakutana na huyu mshkaji wetu ambaye alikuwa mpita njia tu asiye na hatia akielekea kazini. Aisee nilihuzunika sana siku hiyo.

Hata kama angekua mwizi kweli Japokuwa wanasema huwezi kuthubutu kumpiga mwizi kama hukuwahi kuibiwa. Lakini hapana sio kwa kiwango cha kufikia kumpiga visu vya shingoni binadamu mwenzako bila huruma.

Halafu bora hata wagemkuta anavidhibiti kuwa ni yeye kafanya, maskini hata yule mwizi halisi aliyekimbia naye hakufanikisha kuiba chochote.

Wapumbavu wachache walikuwa wakisema siku yake ilifika

It's Scars

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimeapa kutopiga mwizi ,na kama kuibiwa nimeibiwa kwelikweli kuanzia nyumbn wakati naishi kwetu tulivamiwa na wezi zaidi ya 15 waliiba kila kitu ,wakat naanza maisha pia nilivunjiwa gari yangu my 1st car waliiba taa ,power window ,side mirrors....urembo wa dashbord lakini haijastify mimi kupiga mwizi ,coz naogopa nisije ingia kwenye makosa ya kudhulumu nafsi ya mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kuondoa uhai wa binadamu mwenzako ni tendo la kinyama sana haijalishi umeibiwa nini

Kuna wanaofanya uhalifu kulingana na shinikizo fulani halafu baadae wanakuja kujutia makosa yao na kuacha kabisa tabia hiyo. Sasa hawa ukiwaua watakua wamejifunzaje?

Mfano kuna dogo alienda kuiba kwenye duka la tajiri ili apate pesa ya kumtibia mama yake aliyekua amelala kitandani baada ya kukosa pesa ya kupelekwa hospitali. Sasa dogo huyu alikamatwa dukani akichukua hizo pesa lakini kama zari tu mwenye duka hakupiga kelele akamuuliza kwanini unaiba akajibu nataka kumtibu mama yangu anaumwa

Jamaa akamchukua dogo akamuoneshe mama yake ili naye athibitishe ile kauli ya dogo akakuta kweli mama yake yuko hoi anaumwa. Alichokifanya yule jamaa akakodi taxi na kumuwaisha hospitali halafu kuanzia pale yule dogo akapewa kazi ya kuuza lile duka na dogo hajawahi muibia jamaa

It's Scars
 
Weee utamkamataje Jesus unaleta masihara. Mnamdharau Jesus kwasababu mpole. Jarib kuingia anga za kibano cha haja utakachopokea.
Jesus gani kwanza?

Ebu eleza isije ukawa unamzungumzia Gabriel jesus wa man city

It's Scars
 
Aisee hata mimi nilitaka kujua hili swali inamaana watu hawakuona kama kambilia umo kwako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu waliona ila hawakuchukua action yeyote kwasababu walishamjua kua ni kijana wa hapa hapa mtaani na cv yake wanaijua hana skendo ya wizi hata katika kazi zake hajawahi dhulumu mtu

Waliomshambulia walikua niwatu kutoka nyumba moja tu, na kelele za kuita mwizi zilikua zikifanyika wakati wakiendelea kumdunga visu. Kwaiyo muda ambao majirani tunatoka jamaa alishakua attacked

It's Scars
 
inasikitisha lakini usiombe ukutane na Mwizi kweli..mwizi anapoenda kuiba ana manne kichwani mwake, Afanikiwe ama akamatwe, aue ama auawe, wezi wengi huwa wanajihami, ukikosea kidogo anakuua wewe fasta na anatokomea, unaposikia kelele za mwizi kuwa makini sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi ni moja ya watu ambao nilikuwa sipendi mwatu wampige/ kumuua mwizi hata kama amekutwa na "exhibit". Niliwahi kuibiwa spea za ki IST kangu nilikonunua kwa taabu sana. Nikasamehe. Mara ya pili wezi wakaingia kwangu wakati niko safari na kuiba TV yangu inchi 48. Nikasamehe. Mara ya tatu wakaja kuiba tena TV this time niliwashtukia wakiwa wanakata grill nikawakurupusha wakakimbia. Juzi kazi niko mitaa fulani vikakwapua simu yangu kwa bodaboda. Sijasamehe.

Kwa sasa popote nitakapokuta mwizi anapigwa/ kuuliwa nami nitaunga juhudi. Nimegundua sisi tunaowasamehe wezi ndo maana wanaendelea kuiba kwa kutuona mafala.
 
Sasa mzee huoni kushiriki kupiga mwizi ambaye huna uthibitisho kua ameiba kweli kunaweza kukuingiza matatani?

Kiufupi ni kwamba ndugu wa marehemu hawataridhia kuendelea kukuona una-bang tu kitaa wakati ulishiriki kudhulumu uhai wa ndugu yao ambaye mlimuua kimakosa??

Kiukweli ni kwamba kuibiwa kuna machungu yake. Unarudishwa nyuma sana kimaendeleo. Lakini machungu hayo hayafikii machungu ya kumpoteza ndugu yako umpendae ambaye ameuliwa bila hatia.

Kipi bora hapo, uwasilishe taarifa polisi na swala liwe chini ya sheria au uchukue sheria mkononi ambayo serikali na ndugu zake watakusaka na kukufanya uishi kwa mashaka?

It's Scars
 
inasikitisha lakini usiombe ukutane na Mwizi kweli..mwizi anapoenda kuiba ana manne kichwani mwake, Afanikiwe ama akamatwe, aue ama auawe, wezi wengi huwa wanajihami, ukikosea kidogo anakuua wewe fasta na anatokomea, unaposikia kelele za mwizi kuwa makini sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli, lakini unadhani kumpiga mwizi na kumuua ndo solution ya kutokomeza wizi?

Sikufichi kuna mwaka flani nilikaa tunduma wezi walikia wanaiba mno ikafikia hatua wananchi wakisikia mwizi tu wanaua.

Kilichofanyika nao wakakaa kikao halafu wakatunga sheria wakaweka bango mitaani ambalo lililokua linasomeka "sisi tunawaibia tu ila hatuwadhuru ila nyie mkitukamata mnachukua vitu tulivyoviiba kisha mnatuua kwa kutuchoma moto. Sasa basi nasisi tumeamua kua ukabaji wetu utahusisha na mauaji pindi ambapo tutakua tukiwaibia"

It's Scars
 
Sasa mzee huoni kushiriki kupiga mwizi ambaye huna uthibitisho kua ameiba kweli kunaweza kukuingiza matatani?

Kiufupi ni kwamba ndugu wa marehemu hawataridhia kuendelea kukuona una-bang tu kitaa wakati ulishiriki kudhulumu uhai wa ndugu yao ambaye mlimuua kimakosa??

Kiukweli ni kwamba kuibiwa kuna machungu yake. Unarudishwa nyuma sana kimaendeleo. Lakini machungu hayo hayafikii machungu ya kumpoteza ndugu yako umpendae ambaye ameuliwa bila hatia.

Kipi bora hapo, uwasilishe taarifa polisi na swala liwe chini ya sheria au uchukue sheria mkononi ambayo serikali na ndugu zake watakusaka na kukufanya uishi kwa mashaka?

It's Scars
Mkuu mtu akiuwawa kimakosa ni jambo baya sana.
Mimi nawasemea wale ambao wamekutwa wameiba au wako kwenye harakati za kuiba. Hawa wauliwe bila kupepesa macho. Suala la wezi/ vibaka ukipereke Polisi utaishia kuliwa pesa zako na mwizi hata ukimkamata mizinga utakayopigwa na "afisa upelelezi" si ya kitoto.

Ukitaka kujua machungu ya kuibiwa ngoja siku yakukute. Wakupige panapoumwa hasa. Juzi walimkwida mdada moja ofice mate wangu wakachukualia pesa alizokuwa anakwenda kumlipia mtoto wake ada.
 
Mwanangu ww unakaa kiwalani nin??
Nakuambia watu wanakufa kwa kupandikiziwa uongo kwasababu wananchi hawatoi mwanya wa kukupa nafasi ya kujieleza

Huku kitaa kuna kibaka alikua ni albino, anakukaba halafu ukitaka kujitetea ukimshinda nguvu anapiga kelele kua "jamani mimi albino anataka kunikata viungo vyangu" na watu wakifika hapo hawaulizi wakiangalia kweli jamaa ni albino wao wanakutembezea kichapo tu

It's Scars

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom