Tukio la utata Kupotea kwa rubani wa Australia 1978

Son.j

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
993
2,253
Frederick Valentich ni rubani mwanafunzi aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika mazoezi kwenye ndege ijulikanayo kama Cessna 182L light aircraft mnamo 21 October 1978. Tukio lililo acha maswali mengi ambayo yamekosa majibu mpaka leo kwani Nadharia za mamlaka na maofisa wa Australia zilidai kuwa huenda kupotea kwa kijana huyu kumesababishwa na UFO (ambapo inasadikika kilionekana kikizurura maeneo kadhaa Australia usiku kabla ya kupotea kwa Frederick). Kumbuka nchi ya Australia imekumbwa na visa vingi sana vya UFO.
Nadharia nyingine ilidai kuwa Frederick alipagawa na aliona reflaction ya mwanga wa ndege yake kwenye maji ama aliona mwanga kutoka kisiwa cha jirani wakati akiruka juu chini yaani upside down.
260px-Cessna_182_(5782498179).jpg
ndege aina ya cessna 182
FREDERICK VALENTICH KATIKA URUBANI.
frederick mzaliwa wa may 9 1958 alikuwa na kibali cha kuruka kwa jumla ya masaa 150 na pia alikuwa na kibali cha kuruka wakati wa usiku lakini akiwa chini ya uangalizi wa visual meteorological condition (vmc). alishawahi ku omba mara mbili nafasi katika Royal Australian Air Force (RAAF) Lakini alikataliwa kutokana na kutokuwa na viwango stahiki vya elimu.
Alishawahi kujifunza kuwa commercial pilot lakini alikuwa na maendeleo mabovu hivyo kufeli mara mbili katika mitihani mitano ya kupata leseni ya kuwa commercial pilot.
Miezi miwili kabla ya kupotea kwake alifeli mitihani mingine mitatu ya kupata leseni ya kuwa commercial pilot.
Pia alishawahi kujihusisha katika matukio kadhaa ya kurusha ndege mfano
Alishawahi kujiingiza katika controled zone ya Sydeney, ambayo alipokea onyo, Mara mbili mfulilizo aliruka juu mawinguni ambapo alifunguliwa mashitaka.
220px-Frederick_Valentich.png

Kulingana na baba yake, Frederick alikuwa anaamini kindakindaki juu ya uwepo wa UFOs na alikuwa na wasiwasi juu ya kushambuliwa navyo.

Kituo cha mwisho cha safari ya Frederick ni KISIWA CHA KING lakini matamanio yake ya kupaa kwakwe hayakujulikana. Aliwaambia maafisa wa kurusha ndege kwamba anaenda kisiwa cha king kubeba marafiki zake, wakati huo huo aliwaambia wengine anaenda kuchukua crayfish, ambapo ilikuja kugundulika baadae kati ya sababu zake zote hapakuwa na lolote lenye ukweli. Frederick pia hakuarifu Airport ya kisiwa cha King sababu za kwenda kutua, kitu ambacho ni kinyume na taratibu.

KUPOTEA KWAKE.
Frederick alitaarifu kwa redio MELBOURNE Air traffic Control mnamo 7:06 pm akiripoti kuwa anafuatiliwa na aircraft(ndege) isiyotambulika ikiwa futi 4,500(mita 1,400). alisema anaona unknown aircraft ambayo inaonekana inamulika mwanga mkali unaoashiria kutua, alishindwa kutambua ni aina gani ya ndege lakini alisema imempita juu kama futi 1000 (300 m) na ilikuwa ikienda kwa speed kali. Baadaye Frederick aliripoti kuwa aircraft ile inamkaribia kutokea upande wa mashariki na kusema pengine rubani mwingine anamtania makusudi. Frederick alisema ndege ile sasa ipo usawa wake kwa juu na ina mwanga wa chuma wa kung'ara na mwanga wa kijani, Frederick alizidi kutoa ripoti kuwa ameanza kukumbana na tatizo la engine, Alipoulizwa abainishe hiyo aircraft, Frederick Valentich kijana wa miaka 20 alijibu "It's not an aircraft". mawasiliano yake yakaanza ingiliwa na sauti zisizoeleweka zilizobainishwa kama sauti ya vyuma vinayokwaruzana, kabla ya mawasiliano yote kupotea.
.
240px-Valentich_disappearance.png

KUTAFUTWA NA UOKOZI.
Msako wa majini na angani ulifanyika ikihususha vikosi vya Oceangoing ship traffic, RAAF lockheed P-3 Orion aircraft pamoja na Ndege nane za kiraia, msako ulichukua eneo la 1,000 square miles, msako ulisitishwa october 25 1978 bila ya matokeo.

UPELELEZI.
Upelelezi wa kupotea kwa Valentich chini ya Idara ya usafiri ya Australia ulishindwa kujua nini chanzo lakini F. Valentich alidhaniwa kufa.
miaka mitano baada ya kupotea kwake Sehemu ya control ya Engine ilipatikana imesukumiwa kufukweni mwa Flinders Island. july 1983 mamlaka ya usalama wa anga uliubainisha kwamba mabaki yale yanatokana na ndege ya Cessna 189 kati ya ya range ya sirial number kadhaa pamoja na ndege ya Frederick.

NADHARIA NA MAPENDEKEZO:
Nadhariwa yakwanza Inadhaniwa kuwa Valentich aliigiza kupotea kwake kutokana na kutofautiana kwa mipango ya safari zake usiku ule.
kuna jambo la ajabu kuhusu Frederick kwenda King Island, baba yake anasema mwanae alimwambia kuwa amechelewa dk 40 kuondoka kwenda king.
"Alipanga safari yake kwnda Moorabbin lakini hakuwataarifu King island airport kwahiyo hapakuwa na mwanga uwanjani. Hili linaonesha kwamba jamaa alipanga kutoweka kwake kiajabu au alitaka kujiua.
Lakini inaelezwa kwamba hakuwa na tatizo lolote na Familia yake wala gilfriend wake, wala hakuwa na msongo wa mawazo.

Nadharia nyingine inaelza kwamba Frederick alipaa juu chini na mwanga aliokuwa anauona ni reflaction kwenye maji na kwamba baadaye aliangukia majini, lakini ndege aina ya cessna isingeweza kuelea hivyo engine zingekatika mapema.

Mnamo 2013 mwanaanga mstaafu wa US Airforce Rubani James McGana na Mwandishi Joe Nickell walipropose kuwa Valentich alipagawa/kupigwa bumbuwazi nakujikuta akigeuza ndege wima akidhani anigeuza ndege chini kitendo kinacho julikana kama graveyard spiral ambapo mwanzo alichukulia kimakosa kama ndege nyingine juu yake, kulingana na mwandishi gravity force ya kugeuza ndege ingepunguza flow ya mafuta matokeo yake ni mngurumo mbaya, waliendelea kueleza mianga aliyoiona ni Venus , Mars na Mercury pamoja na nyota kali inayo ng'aa Antares.

UFO..
UFOLOGIST..
wanasema huenda ndege ya Valentich iliharibiwa au walimteka, kutokana na watu kuripoti kuona mwanga wa kijani unaotembea angani ni wakati Frederick aliporipoti juu ya mwanga wa kijani katika mawasiliano ya redio.
Kikundi Graund Saucer Watch kulingana na picha zilizopigwa na Roy Manifold siku ya kupotea kwake zilionesha kitu kinachotembea haraka kikipotelea karibu na lighthouse ya Cape Otway. Kulingana na mwandishi wa mambo ya UFO Jerome Clark, anasema picha zilionesha kifaa ambacho hakitambuliki chenye umbo la kiasi kikiwa kimezungukwa na kitu kama mawingu-mvuke kikipita, Hatahivo picha hazikuwa clear kiasi cha kutambua kifaa kile.

MWISHO:
A
ustralia ni bara na nchi yenye matukio mengi sana ya kupotea kwa watu, ambapo inaripotiwa zaidi ya watu 38,000 hupotea kwa mwaka,
pia limekumbwa na nadharia mbalimbali za ufo.
kumbuka kwamba swala la uwepo wa UFO halijawahi kuthibitishwa, na wapo wengi wanaopinga uwepo wa hivyo vitu.

Story na picha by wikipedia.
 
UFO for the record wanaonekana ni viumbe advanced kuliko sisi binadamu,

Kuna story ya captain moja wa meli ya kivita ya Usa , anasema alfajiri moja waliona chombo cha ajabu majini , walijpoaribu kukisogelea ni kama waiokuwa humo nao walikuwa wanawaangalia wao, walipofika karibu like chombo kwa Kasi ya ajabu kilinyanyuka na kupaa juu kwa speed ambayo captain anasema hajawai kushuhudia popote
 
Hivi inawezekana ukageuka upside down bila kujua! Sina hakika lakini naamini katika hii solar system kuna viumbe wengine hatujajuana bado. Pengine muda mfupi toka dunia ilipoanza inaweka ugumu wa kuwatambua wenzetu au umbali wa kutoka kwenye jua letu hadi nyota majirani.
 
Inawezekana UFO sio alliens Bali Ni binadamu flani walio endelea zaidi wanaviendesha hivyo vyombo na kufanya matukio kwa manufaa yao, hata Hilo tukio lenyewe ukiangali huyo bwana mdogo alikuwa na kitu Cha tofauti sana ukisoma zaidi personal information zake.
 
That's the fact , Ila haiwi addressed kwa sababu italeta mtifuano wa kiimani
itabidi wajiulize Kuna miungu wangapi, na kwa nini Mungu wa aliens yupo hivi au vile ,.kiufupi alliens wame advance maana wanatu treat Kama vile sisi tunavyo wa treat viumbe Kama sisimizi au wadudu flan , hata haya magonjwa ya corona na mengine makubwa nawaza binafsi inawezekana tumenynyuziwa dose na aliens just like binadamu anavyonyunyiza dawa ya kunguni, na kunguni anakuwa hana hata clue ya kujiokoa.
 
...Tuangalie sana hizi Story.
Unaweza kukuta huyu alipata ajali ya kawaida tu ya kutumbukia kwrnye bahari yenye kina kirefu na kupotea lakini hapa tunataka kuaminishwa kwamba ni story ya Kushangaza isiyokuwa na Maelezo!!

Nikiiangalia hii, ninaona ni ajali tu ya kawaida na ndio maana baadhi ya mabaki ya Ndege yake yalikuja kupatikana baadaye!!!
 
Frederick Valentich ni rubani mwanafunzi aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika mazoezi kwenye ndege ijulikanayo kama Cessna 182L light aircraft mnamo 21 October 1978. Tukio lililo acha maswali mengi ambayo yamekosa majibu mpaka leo kwani Nadharia za mamlaka na maofisa wa Australia zilidai kuwa huenda kupotea kwa kijana huyu kumesababishwa na UFO (ambapo inasadikika kilionekana kikizurura maeneo kadhaa Australia usiku kabla ya kupotea kwa Frederick). Kumbuka nchi ya Australia imekumbwa na visa vingi sana vya UFO.
Nadharia nyingine ilidai kuwa Frederick alipagawa na aliona reflaction ya mwanga wa ndege yake kwenye maji ama aliona mwanga kutoka kisiwa cha jirani wakati akiruka juu chini yaani upside down.
View attachment 1686785 ndege aina ya cessna 182
FREDERICK VALENTICH KATIKA URUBANI.
frederick mzaliwa wa may 9 1958 alikuwa na kibali cha kuruka kwa jumla ya masaa 150 na pia alikuwa na kibali cha kuruka wakati wa usiku lakini akiwa chini ya uangalizi wa visual meteorological condition (vmc). alishawahi ku omba mara mbili nafasi katika Royal Australian Air Force (RAAF) Lakini alikataliwa kutokana na kutokuwa na viwango stahiki vya elimu.
Alishawahi kujifunza kuwa commercial pilot lakini alikuwa na maendeleo mabovu hivyo kufeli mara mbili katika mitihani mitano ya kupata leseni ya kuwa commercial pilot.
Miezi miwili kabla ya kupotea kwake alifeli mitihani mingine mitatu ya kupata leseni ya kuwa commercial pilot.
Pia alishawahi kujihusisha katika matukio kadhaa ya kurusha ndege mfano
Alishawahi kujiingiza katika controled zone ya Sydeney, ambayo alipokea onyo, Mara mbili mfulilizo aliruka juu mawinguni ambapo alifunguliwa mashitaka.
View attachment 1686958

Kulingana na baba yake, Frederick alikuwa anaamini kindakindaki juu ya uwepo wa UFOs na alikuwa na wasiwasi juu ya kushambuliwa navyo.

Kituo cha mwisho cha safari ya Frederick ni KISIWA CHA KING lakini matamanio yake ya kupaa kwakwe hayakujulikana. Aliwaambia maafisa wa kurusha ndege kwamba anaenda kisiwa cha king kubeba marafiki zake, wakati huo huo aliwaambia wengine anaenda kuchukua crayfish, ambapo ilikuja kugundulika baadae kati ya sababu zake zote hapakuwa na lolote lenye ukweli. Frederick pia hakuarifu Airport ya kisiwa cha King sababu za kwenda kutua, kitu ambacho ni kinyume na taratibu.

KUPOTEA KWAKE.
Frederick alitaarifu kwa redio MELBOURNE Air traffic Control mnamo 7:06 pm akiripoti kuwa anafuatiliwa na aircraft(ndege) isiyotambulika ikiwa futi 4,500(mita 1,400). alisema anaona unknown aircraft ambayo inaonekana inamulika mwanga mkali unaoashiria kutua, alishindwa kutambua ni aina gani ya ndege lakini alisema imempita juu kama futi 1000 (300 m) na ilikuwa ikienda kwa speed kali. Baadaye Frederick aliripoti kuwa aircraft ile inamkaribia kutokea upande wa mashariki na kusema pengine rubani mwingine anamtania makusudi. Frederick alisema ndege ile sasa ipo usawa wake kwa juu na ina mwanga wa chuma wa kung'ara na mwanga wa kijani, Frederick alizidi kutoa ripoti kuwa ameanza kukumbana na tatizo la engine, Alipoulizwa abainishe hiyo aircraft, Frederick Valentich kijana wa miaka 20 alijibu "It's not an aircraft". mawasiliano yake yakaanza ingiliwa na sauti zisizoeleweka zilizobainishwa kama sauti ya vyuma vinayokwaruzana, kabla ya mawasiliano yote kupotea.
.View attachment 1686959

KUTAFUTWA NA UOKOZI.
Msako wa majini na angani ulifanyika ikihususha vikosi vya Oceangoing ship traffic, RAAF lockheed P-3 Orion aircraft pamoja na Ndege nane za kiraia, msako ulichukua eneo la 1,000 square miles, msako ulisitishwa october 25 1978 bila ya matokeo.

UPELELEZI.
Upelelezi wa kupotea kwa Valentich chini ya Idara ya usafiri ya Australia ulishindwa kujua nini chanzo lakini F. Valentich alidhaniwa kufa.
miaka mitano baada ya kupotea kwake Sehemu ya control ya Engine ilipatikana imesukumiwa kufukweni mwa Flinders Island. july 1983 mamlaka ya usalama wa anga uliubainisha kwamba mabaki yale yanatokana na ndege ya Cessna 189 kati ya ya range ya sirial number kadhaa pamoja na ndege ya Frederick.

NADHARIA NA MAPENDEKEZO:
Nadhariwa yakwanza Inadhaniwa kuwa Valentich aliigiza kupotea kwake kutokana na kutofautiana kwa mipango ya safari zake usiku ule.
kuna jambo la ajabu kuhusu Frederick kwenda King Island, baba yake anasema mwanae alimwambia kuwa amechelewa dk 40 kuondoka kwenda king.
"Alipanga safari yake kwnda Moorabbin lakini hakuwataarifu King island airport kwahiyo hapakuwa na mwanga uwanjani. Hili linaonesha kwamba jamaa alipanga kutoweka kwake kiajabu au alitaka kujiua.
Lakini inaelezwa kwamba hakuwa na tatizo lolote na Familia yake wala gilfriend wake, wala hakuwa na msongo wa mawazo.

Nadharia nyingine inaelza kwamba Frederick alipaa juu chini na mwanga aliokuwa anauona ni reflaction kwenye maji na kwamba baadaye aliangukia majini, lakini ndege aina ya cessna isingeweza kuelea hivyo engine zingekatika mapema.

Mnamo 2013 mwanaanga mstaafu wa US Airforce Rubani James McGana na Mwandishi Joe Nickell walipropose kuwa Valentich alipagawa/kupigwa bumbuwazi nakujikuta akigeuza ndege wima akidhani anigeuza ndege chini kitendo kinacho julikana kama graveyard spiral ambapo mwanzo alichukulia kimakosa kama ndege nyingine juu yake, kulingana na mwandishi gravity force ya kugeuza ndege ingepunguza flow ya mafuta matokeo yake ni mngurumo mbaya, waliendelea kueleza mianga aliyoiona ni Venus , Mars na Mercury pamoja na nyota kali inayo ng'aa Antares.

UFO..
UFOLOGIST..
wanasema huenda ndege ya Valentich iliharibiwa au walimteka, kutokana na watu kuripoti kuona mwanga wa kijani unaotembea angani ni wakati Frederick aliporipoti juu ya mwanga wa kijani katika mawasiliano ya redio.
Kikundi Graund Saucer Watch kulingana na picha zilizopigwa na Roy Manifold siku ya kupotea kwake zilionesha kitu kinachotembea haraka kikipotelea karibu na lighthouse ya Cape Otway. Kulingana na mwandishi wa mambo ya UFO Jerome Clark, anasema picha zilionesha kifaa ambacho hakitambuliki chenye umbo la kiasi kikiwa kimezungukwa na kitu kama mawingu-mvuke kikipita, Hatahivo picha hazikuwa clear kiasi cha kutambua kifaa kile.

MWISHO:
A
ustralia ni bara na nchi yenye matukio mengi sana ya kupotea kwa watu, ambapo inaripotiwa zaidi ya watu 38,000 hupotea kwa mwaka,
pia limekumbwa na nadharia mbalimbali za ufo.
kumbuka kwamba swala la uwepo wa UFO halijawahi kuthibitishwa, na wapo wengi wanaopinga uwepo wa hivyo vitu.

Story na picha by wikipedia.
Tujipumzishe na bangi jamani.... Duh
 
Inawezekana UFO sio alliens Bali Ni binadamu flani walio endelea zaidi wanaviendesha hivyo vyombo na kufanya matukio kwa manufaa yao, hata Hilo tukio lenyewe ukiangali huyo bwana mdogo alikuwa na kitu Cha tofauti sana ukisoma zaidi personal information zake.
UFO sio Aliens naungana na wewe, hizi frying Object wamezitumia sana wajerumani kipindi cha vita ya pili sijui ya kwanza, na yapo mashirika ya siri uanamiliki hizi ndude wakishirikiana na viumbe wengine miaka na miaka, na zaidi ni kwamba, hizo UFO hata hapa Tanzania baadhi ya maeneo huwa zinaonekana, na kama hujabahatika kuziona ata kwa mbaali basi fahamu ni suala la muda tu, mwezi uliopita, mwezi wa saba tarehe 22, location Unknown, nimeliona moja live bila ya chenga, Morogoro kusini.
Pia nishawah ona tukio la kuinuliwa semi ktk pori la ushirombo, semi imebebwa juu usawa wa nguzo mbili za umeme, limechanwa container na ikapigwa kikumbo kimoja matata sana kurudishwa chini, sijui waliopima ile ajati waliandika repoti gani...kuhusu haya madide anayebisha ni yule anayetaka tu kushuhudia kwa macho ya nyama ila yapo sana...

Nilikoyaona hayo madude yasiyoeleweka.

Mwanza

Morogoro kusini ( sitapataja jina ni mji upi hasa )

Ushirombo.
 
Back
Top Bottom