Tukio la timu ya Simba kupigwa mawe na fundisho muhimu la kisiasa

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,011
2,000
Kuna tukio moja ambalo limesahaulika katika kumbukumbu zetu. Miaka fulani ya mwishoni mwa 1990s, timu ya Simba ilienda kucheza mechi mjini Khartoum, Sudan.

Simba wakakaza sana na mpira ulipoisha, Wasudan wakakasirika na kuanza kuwarushia mawe uwanjani pale wachezaji wa Simba.

Naamini tukio lile ukichunguza kwa umakini, lilikuwa na ushawishi fulani kutokana na matendo ya kihalifu na kiubaguzi ya serikali ya Omar Al-Bashir dhidi ya Wasudan weusi.

Ni muhimu sana kukumbuka, maamuzi na matendo ya serikali yoyote, hasa yakiwa yanajirudia hadi kuonekana na kuaminika ni itikadi na mlengo rasmi wa serikali, yana tabia ya kisaikolojia kuambukizwa kwa raia wa kawaida, hasa wale wasiojielewa au walio rahisi kushawishika.

Mwisho wa siku, bila kutambua raia wanaanza kufanya vitendo vinavyoshabihiana na vile vya serikali yao. Hayo ndiyo yaliyotokea Sudan.

Tukatae siasa za woga na ubaguzi wa aina yoyote. Serikali ijitahidi sana kuepuka kubagua au kunyanyasa watu kwa sababu zozote zile. Historia inaonyesha mwisho wa hayo mambo huwa si mzuri hata kidogo.
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
179,900
2,000
Hebu anzeni kumchakata domo kwa mawe tuamini hampendi siasa ichanganywe kwenye michezo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom