Tukio la Rusumo: Kumradhi IGP kwa nilichoandika kwenye mada hiyo

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
248
253
Jana niliandika habari kuhusu kijana aliyejeruhiwa na majambazi huko Rusumo mpakani mwa Tz na Rwanda. Pia ktk habari hiyo nilielezea namna tukio hilo lilivyotekelezwa jirani kabisa na alipokuwa IGP.

Nieleweke,nia yangu ilikuwa siyo kumchafua IGP km baadhi ya wachangia ile habari walivyotuhumu!Bali nilikuwa najaribu kuonyesha ni namna gani uzembe wa baadhi ya askari wetu ulivyo!

Tukio hilo kutukia jirani kabisa na alipokuwa IGP ni AIBU kwa askari wa eneo husika.Ninao uhakika IGP hakufahamishwa hilo jambo kwa wakati na yeye IGP atakubaliana na mm alilifahamu jambo hilo baadae sana.

Pamoja na yote nachukua fursa hii kukupa pole na SAMAHANI (IGP) Kwa usumbufu wowote ulioupata kutokana na habari hiyo.Nia yangu haikuwa kukuchafua bali kukosoa uzembe wa baadhi ya askari kutokuwa makini kiusalama ktk eneo lile ambalo hata ww ulikuwepo.Ndiyo maana nilihoji km tukio km lile linatukia pahali ambapo ww upo!

Kumradhi hii haifuti dhana yangu ya kulaumu uzembe ule wa baadhi ya askari hasa walio kuwa doria siku hiyo.Lazima askari wetu (Baadhi) wawe makini ktk kutekeleza wajibu wao na si kujawa na hofu tu mara viongozi wao wa kitaifa wawatembeleapo na kusahau hata na kufanya na kuzuia baadhi ya matukio mepesi km hilo tena jirani kabisa na kiongozi!AIBU!

KUMRADHI IGP!

Mada husika: Rusumo: Kijana mbadilisha fedha auawa na majambazi karibu na alipokuwa IGP
 
Safi umekuwa Muungwana sana kwa kuomba radhi.IGP mimi nakuomba kama ndugu na Mtanzania Mwenzako.msamehe ndugu yetu amekiri amekosea na amekuwa Muungwana....pole sana IGP Wangu
 
Kwani ofisi yake huijui??,bosi wake humjui?? Kilichokukimbiza huku jf ninini??.unatuharibia chama chetu ccm majitu kama ninyi.Tafuteni ajira vijana hizo 7800/= per day zinawatoa ufahamu,wenzenu ccm damudamu lakini tuna kazi zetu ndo maana tunaongea ukweli kwa manufaa ya kizazi kijacho,wewe ni kama chief mangungo
 
Hakuna haja ya kuomba msamaha kwa jambo ambalo liko dhahiri, au umetishwa?
 
Mtoa mada ni msomi na mstarabu sana...kuomba msamaha ni jambo jema sana na lakiungwana sana..hakuna asiyekosea nakuungamkono kwa kutambua umekosa na umerudi sehemu uliyotoa taarifa na kusema samahani.nyie mnaopinga mnapinga nini.pingeni kwa hoja nasio hasira na visasi.hapa CCM na chadema inausika nini.
 
Kwani ofisi yake huijui??,bosi wake humjui?? Kilichokukimbiza huku jf ninini??.unatuharibia chama chetu ccm majitu kama ninyi.Tafuteni ajira vijana hizo 7800/= per day zinawatoa ufahamu,wenzenu ccm damudamu lakini tuna kazi zetu ndo maana tunaongea ukweli kwa manufaa ya kizazi kijacho,wewe ni kama chief mangungo
Soma vizuri andiko langu,hapapo popote pale nilipotaja chama cha siasa ndg.
 
Tukio hilo kutukia jirani kabisa na alipokuwa IGP ni AIBU kwa askari wa eneo husika.Ninao uhakika IGP hakufahamishwa hilo jambo kwa wakati na yeye IGP atakubaliana na mm alilifahamu jambo hilo baadae sana.

Mbona uliisema hii jana na ukaeleweka? kosa lako hukupayuka kuonesha kuna jambo baya linatokea ili ku-draw attention ya IGP na wafuasi wake
 
Hakika wew ni muungwana, mtu aombaye msamaha husamehewa ni kitendo cha kiujasiri
 
Mbona uliisema hii jana na ukaeleweka? kosa lako hukupayuka kuonesha kuna jambo baya linatokea ili ku-draw attention ya IGP na wafuasi wake
Ni msisitizo tu ndg maana wapo baadhi ya wachangiaji wallijikita ktk kuaminisha kwamba habari ile ni dhalilisho kwa IGP ndiyo maana nimeonelea niwe wazi hasa ni lipi lilikuwa shiko langu ktk ile habari.
 
Kwani ofisi yake huijui??,bosi wake humjui?? Kilichokukimbiza huku jf ninini??.unatuharibia chama chetu ccm majitu kama ninyi.Tafuteni ajira vijana hizo 7800/= per day zinawatoa ufahamu,wenzenu ccm damudamu lakini tuna kazi zetu ndo maana tunaongea ukweli kwa manufaa ya kizazi kijacho,wewe ni kama chief mangungo
yan we ndo mweupe kabisa!
 
Jana niliandika habari kuhusu kijana aliyejeruhiwa na majambazi huko Rusumo mpakani mwa Tz na Rwanda. Pia ktk habari hiyo nilielezea namna tukio hilo lilivyotekelezwa jirani kabisa na alipokuwa IGP.

Jana uliandika kwamba aliuawa na si kujeruhiwa. Hata hivyo ni jambo jema kuomba samahani japo hapa sijaelewa kwa nini unaomba samahani kwa IGP. Ni kwa vile habari uliiongezea chumvi kwa kusema kijana ameuawa wakati alijeruhiwa tu, kumtaja IGP katika habari husika au kuandika ukweli pasipo kuuchuja?.
 
Omba radhi kwa njia ile ile uliotumia kuandika habari hii. Sheria ya mtandao inafanyakazi vizuri.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom