'Tukio' la Mzee Harry Kitilya limenifikirisha sana. Wenye nafasi za kiuongozi kuweni makini!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,176
25,446
Kwanza, nawasalimu waungwana wote wa Jamiiforums. Pili, nakiri kuwa jambo ninalotaka kuliandika hapa limetokea juma linaloisha (Alhamisi). Nimechelewa kuandika hapa kwakuwa nilijipa nafasi ya kutafakari vya kutosha. Nimejifunza jambo kubwa kwenye maisha yangu.

Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu majira ya saa mbili na robo asubuhi nilikuwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutekeleza majukumu yangu ya kikazi. Nilikuwa nimeambatana na Profesa mmoja wa UDSM (jina kapuni) ambaye alikuwa mteja wangu na shahidi yangu siku hiyo mahakamani hapo kwenye shauri lililonipeleka.

Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mlango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ilikuwa ni kama tunapishana na gari hilo. Mzee Kitilya alipomuona Profesa anayefahamiana naye (akijitahidi kuchangamka na kusahau kwa muda maswahibu yake) alimwita Profesa kwa jina na kumsalimu. Akajitahidi kumfahamisha na mwenzake kuwa yule ni Profesa na ni rafikiye. Hakujali hata askari wa Magereza waliokuwa wamewasimamia kiulinzi. Kwa bahati njema,dereva alisimama kwa muda 'kuruhusu' salamu hiyo.

Baada ya salamu, Profesa akamwambia Mzee Kitilya: Pole. Akionekana kusawajika, kutamani kuwa nje ya gari ile huru kama mwanzoni na mwenyewe kujiamulia cha kufanya na kusema, Mzee Kitilya akajibu: Asante Profesa, tupo! Gari ikamalizia kona na kuondoka.

Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.

Ikiwa mti mbichi unatendwa vile, itakuwaje kwa miti mikavu? Nawasihi viongozi mbalimbali waweke akiba ya maneno na matendo yao. Maisha hayana formula!
 
Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mpango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ngosha ana lakujifunza katika ili pia
 
Inatukumbusha pia kuwa, tuwapo makazini na wenye mamlaka tutende kazi zetu kwa weledi.
Toshekeni na mishahara yenu, kuibia wanyonge na kupiga dili hakulipi
Kuonea watu na kufanya upendeleo katika ofisi ya umma siyo jambo jema
Anyways, kama alitenda mema na anatendewa haya kwa dhuluma basi atalipwa mara mia, lakini kama anatendewa yaliyo stahili yake, basi mbingu na nchi ni mashuhuda wake
Mniombee kwelikweli
Hizi ni kazi za watu. siyo permanent job
 
Kwanza, nawasalimu waungwana wote wa Jamiiforums. Pili, nakiri kuwa jambo ninalotaka kuliandika hapa limetokea juma linaloisha (Alhamisi). Nimechelewa kuandika hapa kwakuwa nilijipa nafasi ya kutafakari vya kutosha. Nimejifunza jambo kubwa kwenye maisha yangu.

Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu majira ya saa mbili na robo asubuhi nilikuwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutekeleza majukumu yangu ya kikazi. Nilikuwa nimeambatana na Profesa mmoja wa UDSM (jina kapuni) ambaye alikuwa mteja wangu na shahidi yangu siku hiyo mahakamani hapo kwenye shauri lililonipeleka.

Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mpango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ilikuwa ni kama tunapishana na gari hilo. Mzee Kitilya alipomuona Profesa anayefahamiana naye (akijitahidi kuchangamka na kusahau kwa muda maswahibu yake) alimwita Profesa kwa jina na kumsalimu. Akajitahidi kumfahamisha na mwenzake kuwa yule ni Profesa na ni rafikiye. Hakujali hata askari wa Magereza waliokuwa wamewasimamia kiulinzi. Kwa bahati njema,dereva alisimama kwa muda 'kuruhusu' salamu hiyo.

Baada ya salamu, Profesa akamwambia Mzee Kitilya: Pole. Akionekana kusawajika, kutamani kuwa nje ya gari ile huru kama mwanzoni na mwenyewe kujiamulia cha kufanya na kusema, Mzee Kitilya akajibu: Asante Profesa, tupo! Gari ikamalizia kona na kuondoka.

Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.

Ikiwa mti mbichi unatendwa vile, itakuwaje kwa miti mikavu? Nawasihi viongozi mbalimbali waweke akiba ya maneno na matendo yao. Maisha hayana formula!
Mheshimiwa umenena suala la msingi mno kwenye maisha,hakuna anyejua kesho yake,kuna jamaa yangu alikuwa na nafasi nzuri tu lakini kwa yeyote yule ata kama umekutana naye husingeweza jua yeye ni nani,aliishi maisha ya kiasi na utu kwa kujali wengine kama yeye alivyo.Viongozi wanapaswa kujua maisha ni fumbo.
 
Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.
Kila Masika ina Mbu wake!
 
Mara ya kwanza wakati mzee Kitilya anaingia mahabusu pale gereza la keko alipokelewa na vijana ambao yeye mwenyewe aliwapeleka gerezani baada ya kuwafungulia mashtaka ya kuiibia TRA

Nilimsikia wakati huo kwa masikio yangu akisema jamaa hao waliokua wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu wa Mamlaka ya Mapato wameiba kwa njia mbalimbala ikiwemo ya udanganyifu wa kodi mabilioni ya hela na kwamba hawapeleki polisi bali TAKUKURU maana TAKUKURU hawana mchezo!

Wale jamaa kina Robert Mbetwa, Eric Talemwa, Samuel Renjue na wenzao sasa hivi wako nje baada ya kushinda kesi na baada ya kukaa ndani takriban miaka mitano! Hiyo ilikua ni baada kumkaribisha Mzee kwa kumpa godoro la kulalia wote wakiwa watuhumiwa!
 
Kwanza, nawasalimu waungwana wote wa Jamiiforums. Pili, nakiri kuwa jambo ninalotaka kuliandika hapa limetokea juma linaloisha (Alhamisi). Nimechelewa kuandika hapa kwakuwa nilijipa nafasi ya kutafakari vya kutosha. Nimejifunza jambo kubwa kwenye maisha yangu.

Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu majira ya saa mbili na robo asubuhi nilikuwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutekeleza majukumu yangu ya kikazi. Nilikuwa nimeambatana na Profesa mmoja wa UDSM (jina kapuni) ambaye alikuwa mteja wangu na shahidi yangu siku hiyo mahakamani hapo kwenye shauri lililonipeleka.

Mimi na Profesa tukiwa tunaingia mlango wa Mahakama husika (mlango mkuu), gari ndogo ya Magereza ya pickup ilikuwa ikirudi nyuma kutoka Mahakamani hapo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na Washtakiwa/Mahabusu wawili walioketishwa chini kwenye gari hilo kwa nyuma. Mmojawapo alikuwa Mzee Harry Kitilya, Kamishna Jenerali wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aka TRA.

Ilikuwa ni kama tunapishana na gari hilo. Mzee Kitilya alipomuona Profesa anayefahamiana naye (akijitahidi kuchangamka na kusahau kwa muda maswahibu yake) alimwita Profesa kwa jina na kumsalimu. Akajitahidi kumfahamisha na mwenzake kuwa yule ni Profesa na ni rafikiye. Hakujali hata askari wa Magereza waliokuwa wamewasimamia kiulinzi. Kwa bahati njema,dereva alisimama kwa muda 'kuruhusu' salamu hiyo.

Baada ya salamu, Profesa akamwambia Mzee Kitilya: Pole. Akionekana kusawajika, kutamani kuwa nje ya gari ile huru kama mwanzoni na mwenyewe kujiamulia cha kufanya na kusema, Mzee Kitilya akajibu: Asante Profesa, tupo! Gari ikamalizia kona na kuondoka.

Mzee Harry Kitilya alikuwa Mkuu wa TRA iliyokusanya kodi nyingi nchini zilizojenga na kulipia mambo mbalimbali ya kiserikali. Alikuwa Mkuu wa wakusanya mapato ya Serikali na alifanya aliloliweza. Alikuwa akiheshimiwa na wadogo kwa wakubwa wa nchi hii na wakati mwingine kuogopwa. Leo yuko kwenye hali ile.

Ikiwa mti mbichi unatendwa vile, itakuwaje kwa miti mikavu? Nawasihi viongozi mbalimbali waweke akiba ya maneno na matendo yao. Maisha hayana formula!
Kama ambavyo sheria za nchi zilivyo,kosa ni kosa ,kosa hufuta mazuri yote,hakutakiwa kufanya kosa ili alinde heshima na mazuri yake,badala yake akaingiwa tamaa,ndio iliomponza ,awajibike tu.
Pesa waliotafuna ilisabisha vifo vya watu wasio kua na hatia ,mfano ingenunua ,dawa na ambulance,ada kwa watoto maskini wasio na uwezo.

Kiujumla tamaa ilimponza ,awajibike,ndio maana china wananyongwa,simuonei huruma hata kidogo linapokuja suala la rushwa,jamaa zake wa karibu na nduguze ndio wamuonee huruma kwa kua walinufaika na uhalifu wake
 
Alienunua kivuko kibovu kwa gharama ya mabilioni ya shillingi na baada ya awali kuhonga hawara zake nyumba za serikali (tukiachilia mbali madudu mengine) ni mchaga wa wapi vile?
Nenda kafungue jalada kama Kitilya na wenzake walivyofanyiwa
 
87 Reactions
Reply
Back
Top Bottom