Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,257
- 105,389
Mabalozi wana matatizo mengi sana, mengi sana, wanatakiwa kujiongeza pengi sana.Kwa experience yangu ni mabalozi wenye asili ya Zanzibar ndiyo huwa na msaada,kama ni wa huku kwetu Tanganyika ni wachache mno na mara nyingi ni wale wasio na asili za ulugaluga.
Kuna baadhi ya mabalozi huona kama ni wanapungukiwa wao binafsi pale wanaposaidia dharura mbalimbali kwa raia wa Kitanzania huko wanakotuwakilisha.
Mimi wala siwatetei.
Lakini jamani, balozi zetu hizi bajeti zake za manati.
Kweli tunataka zichukue gharama za kusafirisha maiti za watu?
Wakati hao watu wana ndugu zao?
Kwa bajeti gani zinazopewa hizi balozi?
Balozi zina struggle kulipa bili za umeme, maji, kodi za nyumba, mishahara.
Bado tunataka zichukue gharama za kurudisha miili Tanzania?