Tukio la Morogoro: ITV imeitendea haki CHADEMA, POLISI na Watanzania!



WanaJF

Kituo cha Habari cha ITV ndicho kimeonyesha balanced story kwa mauaji haramu yaliyotokea Morogoro leo.ITV imeweza kumuonyesha mtu aliyekuwa jirani na muuza magazeti aliyeuawa kinyama ambaye amesema kwamba kijana aliyeuawa amepigwa risasi na polisi kichwani huku akiwa ameshika magazeti yake.

Pia imeonyesha kwa kina mkutano wa CHADEMA, maoni ya wananchi pamoja na polisi wakipiga watu.Kupitia ITV watanzania wameweza kushuhudia vijana wa CDM wakiwa hawana hata fimbo bali wakionyesha tu alama ya vidole viwili na kubeba bendera za chama chao. Vyombo vya habari vinapaswa kuiga mfano huu.

Hongereni ITV


clouds t.v nao walionehsa?????????
 
Last edited by a moderator:
Habari kutoka vizuri inategemea Reporter, Msimamizi wa matangazo(Mhariri) na Mmiliki.

Habari ya ITV jana imeonyesha Reporter alikuwa mkweli na Mhariri alitenda haki(Fair).

Bahati mbaya sana BBC radio ambao huwa tunawaamini katika kutoa habari kwa uhakika walivurunda vibaya sana, na tatizo ni Reporter wao Eric David Nampesya(kada wa magamba) kugeuka msemaji wa polisi badala ya kuripoti habari kwa usawa. Ninaamini huyu reporter hakuwa Morogoro na alitengeneza story yake akiwa Dar tena bar. Muda si mrefu najua atafukuzwa BBC kwa aibu.
 
Kikosi hiki cha kuzuia raia wanaoenda kwenye mkutano wa CHADEMA kimeongozwa na RPC wa Morogoro na askari aliyeua ni kwa amri yake na amri hiyo ni kwa niaba ya IGP na Amiri Jeshi Mkuu.

Je, hapa tukisema rais amempiga risasi raia asiye na hatia kupitia watendaji wake Watanzania hatuko sahihi?

Kuthibitisha hilo watanzania tutashuhudia RPC na askari wake muuaji watapewa vyeo na viongozi wa CHADEMA kufunguliwa mashitaka.

Rais wangu, IGP, RPC na askari uliyemwua Mtanzania mwenzako kwa neno la Mungu aishiye milele duniani mtashinda kesi zote lakini Mungu wa mbingu na nchi atawahukumu kwa haki.

Watanzania wengi kupitia jina la Yesu wanamlilia Mwenyezi Mungu kwa watawala kuvunja amri ya Mungu hasa ile inayosema USIUE. Watawala muwe na utu hata kama hamna hofu ya Mungu.
 
Namna reporter alivyokuwa ana ripoti habari hiyo inanikumbusha Ufoo Saro wakati anaripoti matukio ya CHADEMA kutokea Arusha.
Inavutia na kusisimua sana. Hongera kwa waandishi wazalendo kama hawa.
 
A big up ITV; na kwa mtu serious kama anatafuta a balanced news coverage; Not perfect but trying their best! the networks to watch ni ITV na Star TV.

TBC are praise singers; communism era style; wachumia tumbo, afterall "He who pays the piper calls the tune"
 
Mimi nafikiri tuungane tuigomee TBC,hakuna kupeleka matangazo yetu pale.Halfu
2015 wasiruhusiwe kukanyaga ikulu wakati Dr wetu anaapishwa.Manake wana
kimbelembele sana hawa watu.
 
Jamani mbona mnaongea kwa mafumbo?
TBC ni nini? naombeni anayejua anijuze tafadhali.
 
ITV inapochemsha ni kile kipindi cha DK 45.Siminyu hafai angetafutwa mtu mbunifu
zaidi.Huwezi kila siku unahoji watu wale wale wa mrengo uleule.Changanya mambo
ili kivute watu tofauti wa mrengo tofauti.Star TV juzi walikuwa na NAPE na wameahidi
kuwaalika chadema J2 ijayo hebu tuone.
 
tatizo siku hizi ugowvi sio ccm-chadema, bali polisi-chadema, yaani polisi wamedhamiria kabisa vita dhidi ya wafuasi wa chadema na viongiozi wao, kwa polisi wafuasi wa chadema sio raia wa tanzania ni wahuni flani...aisee kuna kazi nyingine za kwenda motoni tu.
 
Ingekuwa tumekosa busara bila kuwapa hongera ITV, hawa jamaa wapo kwa ajili ya watanzania wote na si kwa maslahi ya watu au kundi fulani tu, NAWAPONGEZA KWA MOYO WOTE na Mungu aendelee kuwapa ujasiri wa kutenda kazi zao kwa uhuru na kwa kuzingatia taaluma zao.Thank you ITV.
 
Jana nimesikiliza BBC, mwandishi wa BBC alilyeripoti alionyesha kama vile Chadema hawajatii amri ya Polisi ndiyo chanzo cha vurugu, na hata risasi aliyopigwa huyo kijana inachunguzwa na Polisi kwani kwa maelezo ya mwandishi kutokana na watu wengi inawezekana risasi ilipigwa na mtu tofauti. Mimi nilipata hisia anajaribu kuwa cover Polisi.

habari kama hizi zinazoelezea upande mwingine wa shilingi watu hawazipendi kwani zinafichua uovu.....tupishe uchunguzi
 
TBC mbuzi kabisaaaa! yaani hata main news za leo wao hawaoni umuhimu wa kutaja jambo hili la kihuni linalofanywa na serikali.

TBC Uchafu kabisa!!

Kwani ni lazima TBC waripoti?
Nadhani wahuni ni viongozi wa CDM walioitisha maandamano haramu..
 
...Mie nimeshasema hapa kwamba hii Serikali ni Serikali DHALIMU ambayo ina wasiwasi mkubwa sana dhidi ya CHADEMA kiasi cha kufikia kuwauwa wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA. Mauaji hayo yanayofanywa na hii Serikali DHALIMU yameshafanyika kule Arusha, Igunga, Tarime, Mbeya na sasa Morogoro. Mauaji hayo yataendelea ili kujaribu kuzima harakati za CHADEMA za kuchukua nchi 2015. hakuna kulala mpaka kieleweke moto umeshawashwa hakuna wa kuuzima.

:peace::peace::peace:



Alutta continua! continua!




WanaJF

Kituo cha Habari cha ITV ndicho kimeonyesha balanced story kwa mauaji haramu yaliyotokea Morogoro leo.ITV imeweza kumuonyesha mtu aliyekuwa jirani na muuza magazeti aliyeuawa kinyama ambaye amesema kwamba kijana aliyeuawa amepigwa risasi na polisi kichwani huku akiwa ameshika magazeti yake.

Pia imeonyesha kwa kina mkutano wa CHADEMA, maoni ya wananchi pamoja na polisi wakipiga watu.Kupitia ITV watanzania wameweza kushuhudia vijana wa CDM wakiwa hawana hata fimbo bali wakionyesha tu alama ya vidole viwili na kubeba bendera za chama chao. Vyombo vya habari vinapaswa kuiga mfano huu.

Hongereni ITV
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom