thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Baada ya Lissu kuvuliwa ubunge mengi yamesemwa, yanasemwa na yataendelea kusemwa, in a positive way or negative way kwa wahusika, kwa maana ya Lissu na Ndugai.
Wapo wanaokubaliana na kutenguliwa kwa ubunge wa Lissu, na wapo ambao hawakubaliani na kutenguliwa kwa ubunge wa Lissu, yote hiyo ni mitazamo ya wadau mbalimbali kwa kila mmoja jinsi alivyolipokea, na mjadala huu una afya kwa demokrasia nchini, kwani majibu na ukweli wa tukio hili hupatikana ndani ya mijadala hii inayoendelea jukwaani.
Nina uhakika uamuzi aliousoma Ndugai bungeni si wa kwake binafsi,kwani nijuavyo bunge lina sheria, kanuni na taratibu ilizojiwekea ,ambazo hutakiwa,kufuatwa na kutekelezwa na wabunge wote wa Jamuhuri ya muungano, ikiwemo na kile alichokisoma Spika Ndugai katika taarifa yake ya kumvua ubunge Tundu Lissu.
Jambo hili hupitia katika kamati ya uongozi ya bunge, kwa maana ya kupatiwa ufafanuzi wa kina ndani ya kamati,kamati ikijiridhisha ndipo azimio hilo hukabidhiwa Spika kwa mujibu wa taratibu walizojiwekea asome hadharani, Kwahiyo narudia kusema tena issue hii si ya Spika Ndugai peke yake.
Kumlaumu Spika haisadii chochote Katika kubatilisha maamuzi yaliyofikiwa na kamati ya uongozi ya bunge,ndio maana Lissu kasema atakwenda mahakamani kuutetea ubunge wake.
Wapo wanaodai kuna wabunge wengine hawapo bungeni kwa muda mrefu, lakini hatua hazichukuliwi, huu si utetezi, kwani inawezekana wabunge hao wanatimiza mashariti ,kanuni na taratibu zilizowekwa na bunge, nikimaanisha wana update taarifa zao kila mara japo hawapo bungeni .
Wapo wanaodai awamu zilizopita hazijawahi fukuza wabunge, niwaambie tu zama zinabadilika. hivyo watu wabadilike kulingana na zama zilizopo.
CHADEMA LAWAMANI TENA
Niseme Kitu kimoja, tukio la kuvuliwa ubunge wa Lissu chadema haiwezi kukwepa lawama hizi, (KUB) Mbowe ,katibu Mkuu Mashinji na kamati nzima ya uongozi ya chadema wanastahili lawama hizi wakiwa wa Kwanza kabisa Kabla ya Spika kulaumiwa.
Tukio la Kwanza lilikua ni la Mbunge Nassar wa Arumelu, linafanana na la Lissu,kukosekana kwa taarifa za udhuru wao bungeni officially ,je viongozi hawa walichukua hatua gani kuhakikisha taarifa za wabunge wao zinakua updated ndani ya bunge? ,au waliishia kulaumu kama wanavyolaumu sasa?, kuna shida ndani ya taasisi (chadema). hili hawawezi kulikwepa.
Chadema na serikali ya ccm wamekua wakifanya shughuli zao kwa kuviziana nani akosee mmoja akimbilie kwa wananchi kunanga mwenzie. Kupata kiki
Ndicho kilichofanya Lissu kuliwa timing kama alivyojaribu kuilia timing serikali ya ccm akiwa nje ya nchi kuongea na vyombo vya habari vya kimataifa (Uingereza, Marekani na Ujerumani) ili serikali iwekewe vikwazo vya kiuchumi .na alipokua akiongea alisisitiza nchi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi Kitu ambazo ni hatari kwa serikali ilioko madarakani, anafikiri walimpigia vigeregere na kutabasamu?, walikua na wenyewe wakimlia timing. Kajaa!
Huruma hufanyika tu pale wote mnapoonyesha kuhurumiana na kusameheana na si vinginevyo.
Unapo amua kupambana na mtu, taasisi, jumuiya au kikundi flani huitajika kuwa smart enough, Kitu ambacho kwa sisi wanadamu ni kigumu kiasili, kwani tuna mapungufu .mapungufu hayo hasimu wako hutumia kama advantage kwake katika kukushughulikia ikibidi.
kilicho fanyika kwa Tundu Lissu liwe somo kwetu, sehemu zetu za ajira, ndani ya taasisi tunazozitumikia,kwa kufuata taratibu, kanuni, sheria zilizowekwa na sehemu unayoitumikia ili sintofahamu kama hii isijetupata, tusiishi kwa mazoea, tuishi kwa kanuni taratibu na sheria zilizopo. huruma huja baada ya tathimini.
Niseme kwa kumalizia bado Lissu anayo haki ya ku appeal Kuhusu maamuzi ya bunge, ni haki yake kwa mujibu wa katiba ,ili sisi maamuma tujue mbivu na mbichi