Tukio la kuteswa kwa ulimboka: Maswali mepesi kwa kamanda kova na serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukio la kuteswa kwa ulimboka: Maswali mepesi kwa kamanda kova na serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by New2JF, Jul 16, 2012.

 1. New2JF

  New2JF Senior Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli haiingii akilini hata kidogo kuhusu hili suala.

  Nina amini hata kamanda kova mwenyewe nafsi yake inamsuta kuhusu alivyolielezea na hata kueleza kuhusu kukamatwa kwa ''mukenya''.

  Nadhani mlipofikia kamanda kova mnahitaji kuelezwa kuwa huo ni mchezo wa kitoto mnaoufanyia umma wa watanzania.

  Kamanda kova.....look here ( naamini una watu karibu wanaosoma hapa)

  kama kweli mlikuwa mnataka kutudanganya sio kwa mtindo huo.
  swali: Hivi siku ulimboka atakaporudi nchini na kuwaambia kuwa huyo mliyemkamata siye mtasemaje?? maana yeye anawafahamu waliomtesa kwa kuanzia na yule mtu aliyewapigia simu wakutane naye. swali: Kwanini uchunguzi wenu usianzie kwa yule jamaa aliyekuwa nao siku ya tukio maana yeye ndiye aliyewapigia simu ''jamaa'' zake waliomtesa ulimboka???? ulimboka alishasema anawajua waliomtesa. Haya hata mchungaji amekuruka kuwa huyo mkenya hakwenda kuungama kanisani kwake...na pia kakueleza kuwa huyo jamaa ana matatizo ya akili, jambo ambalo hatushangai akisema alimteka ulimboka...maana kichaa yeyote anaweza kutamka maneno yoyote yale hata akiamua kukutukana.
  Kamanda kova itakusaidia nini kutudanganya, maana hiyo ni kama kuwadanganya hata watoto wako, wapelelezi wako na intellijensia yako.

  Tafakari
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hata Deo rafiki yake Dr Ulimboka anawajua kwa sura wale watekaji.
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  na kwa nini apelekwe mahakamani kwa kificho?
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Nawadharau sana maafande wa TZ kwa sababu ya ujinga huu. We are not stupid, maelezo yao hayajitoshelezi.
   
 5. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Hata mwenye elimu ya SUNGUSUNGU, Uchunguzi ungeanzia kwa yule jamaa iliekua akiwasiliana na Dr Ulimboka hata kukamatwa na yeye kuachwa. Hii inamaanisha yule afisa usalama wa IKULU alikua akiwafahamu fika jamaa waliohusika na mkasa mzima.

  My take!
  Tumechoka na hujuma za serikali hii potofu, Kova unatumiwa kwa maslahi ya Ikulu na yote yatokanayo. Mwema....sitaki kujilaumu kuzaliwa Tanzania kwa kuona CV yako ni makaratasi tu na hujui hata kudanganya.....

  WEAKNESS: Mwema amekua akikusanya vyombo vya habari na kudai wamekamata silaha na mabomu kadhaa, akijinadi na KUZIKUMBATIA SILAHA HIZO WITH BARE HANDS...Swali: Huu nin utaalamu wa wapi coz kufanya hivyo ni kufuta ushahidi wa Fingureprints???? Hapa ndo ninapoamini yote hua ni changa la macho hasa kwa kua kila tukio kama hili hua umejiandaa na sehemu ya kuhadaa watanzania ili kuona ufanisi wako dhaifu. Sijapata ona UKIWA NA HAO WAANDISHI KATIKA ENEO LA TUKIO.....Does it sound in your mind sir?

  Kuhusu Dr Ulimboka tunataka ukweli even if it will be at their cost! You know them Mwema....
   
 6. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Afande mnachemsha, mkasome kwanza kazi imewashinda. Pole
   
 7. Kwizoo

  Kwizoo New Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KOVA acha sifa za kijanja kijanja wainchi tuna akili kuliko hata wewe, Tu wewe umewekwa hapo na unawezwa kusikilizwa na kuonekana kwenye vyombo vya habari? UMEANZA SIASA NA WEWE DHAHILI
   
 8. New2JF

  New2JF Senior Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lastname asante kwa comment yako.

  ZOMBA ( kama kweli ni wewe umeandika haya basi umepotea sana na hujui usemalo, inatia shaka kuwa yumkini ukawa mmoja wao...pole sana)
   
 9. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Swala jingine utakuta wanaitisha press kutuonyesha silaha au madawa lakini watuhumiwa hawaonyeshwi, au ndo eti kuepusha kupoteza ushaidi? sasa kwanini mnaitisha press conference?
   
 10. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ni muhimu polisi wajipange!
   
 11. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Ushahidi wa silaha wanazozikamata hua wanazifumbata kwa mikono mitupu bila hata gloves, hiki ni kiziba macho wanachukua silaha ghalani kuja kututisha kwenye vyombo vya habari. Mwema akiona hana cha kutokea magazetini hua ndo mbinu yake ili wajue yupo....
   
 12. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280

  Huyu kova alishawahi kuanzishiwa topic humu miaka 3 iliyopita kua ndo anaongoza kuuza sura kwenye tv, tangu akiwa Mbeya.

  Utakuta anaitisha press afu anasema kesho nitawapa habari kamili, ili aendelee kuuza.
   
 13. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Hawatumii akili, nia yao ilikua kumuua hivyo baada ya kumfikisha walitoa na kuanza mateso yao wakijua hata akiwatambua haisaidii kwa kua watamuua mwisho wa siku. Hii imedhihilishwa kwa hali aliyokua nayo, najua unakumbua.....
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu Mungu anataka kuiumbua serikali, imeshawafanya Watanzania hamnazo kwa miaka mingi sana
   
 15. M

  MIRIJA IKATWE Senior Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli
  Utandawazi
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu wanapenda sana kuonekana kwenye TV sijui kwa nini........kila tukio likitokea haraka kwenye dais hata kabla ya kuhakiki tukio lenyewe

  [​IMG]
   
 17. mamee

  mamee JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 236
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  nauliza hivi hamuangaliagi moviez za wenzenu kujifunza technique acheni vihoja vya hide n seek kamanda ngatuka baba...
   
 18. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Mwema alichukua kazi za watu.......ushemeji tu ndiyo umemuweka hapo, kwa ushushushu bora hata mke wake.
   
 19. kyemo

  kyemo Senior Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah!kesi ya nyani,mpelelezi nyani, hakimu nyani

  Yani hata mtoto wa chekechea hadangantwi kinamna hii
   
 20. M

  Masantula2012 Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli nimesikitishwa na taarifa ya polisi juu ya aliyetuhumiwa kumtesa Dr. Ulimboka. Tafakuri yangu iko namna hii kimaswali:-

  1. Hivi mtu ukikodiwa kujeruhi au kuua mtu, una haja gani ya kumuuliza juu ya nani aliyenyuma ya mgomo wenu (i.e. wa Madaktari? - Do you have that time sincerely?). Imani yangu ni kuwa uliyekodiwa na hasa kutoka nje ya nchi, ulitakiwa uue/ ujeruhi na kuondoka maana gawio lako (Malipo) liko tayari kibindoni.

  2. Hivi mtu anayekodiwa kuua/ kujeruhi katika hali ya kawaida kabisa, si anatakiwa awe amemfahamu anayemkodi na kukubaliana ujira/ gawio stahili baada ya kazi? Sasa inaporipotiwa kuwa huyu mtuhumiwa hamjui/ hawajui waliomkodi, inaingia akilini kweli? Acheni ubabaishaji. This is a cooked story/ Report.

  3. Hivi tukio kubwa kama hili la utekaji wa mtu (In this case Dr. Ulimboka) ambalo linahusisha watu kadhaa kimazingira (i.e Mr. Abeid - Aliyekuwa akiwasiliana nao, tangu awali [mtu wa UWT]; Dr. Deo - Rafiki wa karibu wa Ulimboka na ambaye siku ya tukio walikuwa naye; Ahmed Msangi - Afisa upelelezi anayetajwa; Mwenye Bar - pale Leaders Club alipokuwa Dr. Ulimboka na wenzie kwa mazungumzo na hadi utekaji unatokea n.k. Kwanini wasiisadie polisi katika uchunguzi kama ilivyozoeleka siku zote? Mbona sijasikia Dr. Deo mathalani ameitwa kuhojiwa? Au wamemuUlimboka naye??

  4. Kama Mtuhumiwa Joseph (Mkenya) anayedaiwa kuwa ni jambazi sugu (Umri wa miaka 26 au 31 - ambayo nayo ni kitendawili) alihusika kufanya unyama huo kweli, je huo ni umri tosha wa kufanya aende kutubu madhambi yake baada ya kumtesa Dr. Ulimboka? Kwa umri huo, amekwishaua watu wangapi waungwana hadi ajutie? Ingeliingia akilini laiti angelikuwa na umri kuanzia 45?

  5. Nilfurahia Mch. Gwajima kukanusha vikali taarifa hiyo na kuomba TUME HURU YA UCHUNGUZI KUUNDWA katika hili. Ingawa ukanushaji huo unaliumbua JESHI LA POLISI NA SERIKALI YAKE KWA UJUMLA, naamini mungu ni mwema na hawatomgusa/ kumsumbua/ kumuulimboka Mch. Gwajima. Hongera Mchungaji na wengine waige mfano huo na siyo kuwalamba/ kujipendekeza kwa viongozi ili hali TAIFA LINAANGAMIA. Sasa cha kujiuliza ni kuwa Afande Kova atatoa taarifa gani kwa taifa juu ya mkorogano huo??

  MY TAKE/ ADVICE:

  Ukiachilia mbali haja au umuhimu mkubwa wa uundwaji wa tume huru ya kulichunguza hili ambalo kimsingi Jeshi la polisi linaonekana kuguswa moja kwa moja, Binafsi nashauri Viongozi wa Jeshi la Polisi wajiuzulu (IGP, Kova, Msangi na wale wa Kituo cha Polisi - Bunju ambao hawakutoa ushirikiano kumuwahisha Dr. Ulimboka hospitali) kwa kuuhadaa uma kufuatia taarifa hii "fake" au ya "Kutungwa". SHAME ON THE LEADERS AND THE ENTIRE GOVERNMENT. Mkiambiwa ni wadhaifu, hamtaki. Akili kama ya chekechea!!! Dame!!! :shetani:
   
Loading...