Tukio la Kihistoria la kupatwa kwa jua kutokea Tanzania Septemba Mosi.
Akitoa taarifa hiyo Mhadhiri wa fizikia na mtaalamu wa Sonomia katika kitivo cha sayansi chuo kikuu huria cha Tanzania Dkt. Noorali Jiwaji amesema kuwa kwa mara ya mwisho tukio kama hilo lilitokea nchini Tanzania mwaka 1977 na linatarajiwa tena kutokea mwaka 2031.
Wataalam wamelichagua eneo la Lujewa mkoani Mbeya kuwa ndilo enelo ambalo watu wataweza kuona vizuri jua likiwa katika muundo wa pete kutokana na mwezi kukaa katikati yake majira ya saa nne na dakika 17 asubuhi.
Dkt. Jiwaji ametoa wito kwa wanafunzi kuweza kufika eneo hilo kwa ajili ya kujionea yale waliokuwa wakiyasoma kwenye jiografia yakitokea kwa uhalisia , pia itakuwa kama ni sehemu ya kivutio kushuhudia jua likiwa linabadilika katika maumbo mbalimbali.
Aidha Dkt. Jiwaji ametahadharisha juu ya watu kuangalia tukio hilo bila ya kuvaa vifaa maalum vya kuzuia mionzi ya jua kwani ni hatari kwa afya ya macho, vifaa pekee vinavyoshauriwa kutazamia jua ni miwani maalum yenye uwezo wa kuchuja nguvu ya jua kwa asilimia 99.999.
===============================
Across Tanzania, millions of people will be amazed to see the Sun go evening-dim at midday as more than 90% of the Sun will be covered by the Moon in a Partial Solar Eclipse which will the leave the Sun as a thin crescent due to a large chunk being bitten off by the Moon.
The ANNUAL ECLIPSE will be seen as a thin bright ring on that day for hundreds of thousands of people living within a 100 kilometer band crossing southern Tanzania from Congo into Katavi to Mbeya, Ruvuma, to Masasi and out to Mozambique. For them 98% of Sun will be hidden by the Moon, just sufficient to leave a thin bright ring around the Sun.
An Eclipse event is a fascinating, once in a lifetime incident for everyone, especially for the young generation whose minds can be excited to learn the Science behind what they observe.
The next major eclipse in Tanzania is after 15 years so we need to use this opportunity to its maximum.
To view the eclipse, everyone will need to use eye protection “solar viewers”. It is dangerous to view the Sun directly or using homemade darkened materials.
The special solar viewer is a simple device made from special polymer filter material that suppresses 99.999% of the Sun’s intensity as well as removes all other harmful radiation including ultraviolet rays.
Fiat Physica