Tukio la Bwana Hamza kuwapiga polisi risasi ni matokeo ya mfumo wa utoaji haki kuoza

"amedhurumiwa dhahabu zake na polisi"... hapa tuwe makini kidogo, dhahabu zilifikaje kwenye mikono ya polisi ilihali kuna masoko ya dhahabu na taratibu zake kama leseni ( brokers licence) na ulipaji wa kodi nk..
Rudi nyuma kwenye sakata kina zombe arusha
 
Acha kumuhusisha huyo bwana wako (mungu wako) na unafiki wako. Kama ulisikia vizur maneno ya mshambuliaji, basi utapata jibu ni nani aliekuwa nyuma ya lile shambulizi. Inasikitisha kuona kijana kakubali kuuza utu wake, na uhai wake sababu ya laki 6 tu zilizozungumzwa mahakamani. RIP Chacha Wangwe.
Majibu ya hovyo kwa swali la maana. Majibu Kama haya msitegemee yameletwa na mtu wa hovyo ndani ya chama. Hapana hayo ndiyo mawazo ya wale mnaowaita vigogo ndani ya Serikali. Kusema kweli bado tuna safari ndefu. Tafuta ufumbuzi wa kutatua tatizo kwa mustakhari wa taifa

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Acha kumuhusisha huyo bwana wako (mungu wako) na unafiki wako. Kama ulisikia vizur maneno ya mshambuliaji, basi utapata jibu ni nani aliekuwa nyuma ya lile shambulizi. Inasikitisha kuona kijana kakubali kuuza utu wake, na uhai wake sababu ya laki 6 tu zilizozungumzwa mahakamani. RIP Chacha Wangwe.
Mbona unakuwa mjinga?
Ni unafiki mwana CCM kuua polisi?
 
"amedhurumiwa dhahabu zake na polisi"... hapa tuwe makini kidogo, dhahabu zilifikaje kwenye mikono ya polisi ilihali kuna masoko ya dhahabu na taratibu zake kama leseni ( brokers licence) na ulipaji wa kodi nk.... hivi ni huyu tu anayefanya biashara ya dhahabu Tanzania?.... migodi ya dhahabu tunaambiwa iko chunya, chunya pale na Mbeya kuna masoko ya serikali, ilifikaje Dar es salaam hiyo dhahabu? mbona hakudhurumiwa na polisi Chunya, Mbeya, Iringa, Moro ila imetokea Dar es salaam?...

sitetei polisi wala huyu jamaa, najaribu kuwa na fikra huru kuliko kurusha lawama...
Kama unauelewa na biashara hata kidogo usingehoji hayo uliyoyahoji kwa sababu lengo la biashara ni upate faida na ili upate faida basi utafanya biashara yako sehemu ambayo itakupa hiyo faida katika mazingira ambayo yatakupa faida.

Ishu ya kwanini hakuuzia Mbeya ni sawa na kumuuliza Bakhersa kwa nini bidhaa zake trade name ni azam na sio mchongoma.

Mambo ya dhuluma yapo mengi sana na mifano mingi tu ipo na sio Tanzania pekee bali duniani kote.

Polisi ni binaadamu kama wengine wote so wanatamaa, wanatenda dhambi, wanasema uongo, wazinzi na wanafanya uhalifu pia na wengine wanajitahidi kuishi kwa maadili.

Kuhusu muonekano wa jamaa hiyo ni uhuru wa mtu namna anavyotaka kuishi angalia kina kina Bill Gates, Bezos au Elon Musk... Wanamionekano simple sana so ni kawaida besides huezi kwenda vitani na suti mzee.

Hii ishu iko deep sana na ni uwazi kuna history hapa coz mtu huamki tu na lengo la kuua lazima kuna jambo limekuchosha hadi kufikia kufanya maamuzi fulani.
 
Yaani mtu mmoja afuate polisi wengi akapambane nao?Yaani wewe ni mmoja halafu ukatafute polisi wengi wa kupambana nao?Wewe unaona hii inamake sense?Hapo si unakuwa unatafuta kifo cha haraka sana kabla hata ya kusababisha madhara uliyokusudia?

Polisi na wenye vya kutaka kuficha kwenye kadhia hii utawajua kwa mitizamo yao
 
Mitaa ya upanga imeanza kusikika kwamba anayeitwa Gaidi, ni muathirika wa dhuluma za polisi wetu. Polisi wajichunguze pia, badala ya kutisha watu mitaani na kukuza neno 'Ughaidi.'
Ndugu watateswa ili wasiseme hili, lakini linasikika mitaani kwetu!
me binafsi nswe mnafiki hata cjaumia na hilo swala la kuuwawa polisi .

polis! ya sasa imezidi

kuna mtu jirani yangu alibambikiwa kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria walimpandikizia risasi alafu akalipa 5million ili yaishe
 
Majibu ya hovyo kwa swali la maana. Majibu Kama haya msitegemee yameletwa na mtu wa hovyo ndani ya chama. Hapana hayo ndiyo mawazo ya wale mnaowaita vigogo ndani ya Serikali. Kusema kweli bado tuna safari ndefu. Tafuta ufumbuzi wa kutatua tatizo kwa mustakhari wa taifa

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Ungekuwa ww ni mmoja wa watoto wa Chacha Wangwe sijui kama ungekuja na majibu ya aina hii. RIP Chacha Wangwe.
 
Yule mshukiwa wa ugaidi aliyeuliwa Jana ni nani?

-za chini chini na uchunguzi wangu niliokesha nao nimegundua huyu kijana ametokea familia ya madini.

-Baba yake alikuwa na mgodi chunya na mpaka anakufa hakufaidika na mgodi huo lakini pindi alipolifa ndipo neema ilianza kuwadondokea warithi.

-walitokea wachina na kununua kipande chao kieneo na walinunua kwa kiasi kikubwa cha pesa na hapo ndipo walipoenda kununua majengo upanga nk.

Inasemekana juzi kijana huyu alifanya biashara ya dhahabu na mmoja wa mteja na alipovutwa yule jamaa akishirikiana na polisi walimnyanganya Mali zile na kumpa vitisho...huenda alishindwa kuzuia hasira zake japo haiwezi kuwa sahihi moja kwa moja.

Kuna mengi kwenye hili fukuto tuachie vyombo vya usalama watupe majibu sahihi.

Tayari ndugu zake wawili kutoka chunya wamesafirishwa
 
Kama alipata kibali cha kusafirishia kuja kuuza Dar, polisi na kudhulumiana kunaingiaje....kama dhahabu yako iko kisheria na una makaratasi yote mnaanzaje kudhulumiana ( niko kwenye hii biashara najua kuna kitu hakiko sawa hapo)...
Kwa hiyo wanaodhulumiwa ni wale ambao huwa hawana kibali cha kusafirisha pekee?Kwa hiyo wanaodhulumiwa ni wale ambao dhahabu yao haina kibali?

Zombe alipodhulumu yale madini ya wafanyabiashara kipindi kile yale madini hayakuwa na kibali cha kuyasafirisha kuja Dar?Hayakuwa kisheria?

Zombe alidhulumu madini ya wafanyabiashara ambayo yalikuwa yapo kwa mujibu wa sheria zote.Kwa kifupi you don't make sense!
 
me binafsi nswe mnafiki hata cjaumia na hilo swala la kuuwawa polisi .

polis! ya sasa imezidi

kuna mtu jirani yangu alibambikiwa kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria walimpandikizia risasi alafu akalipa 5million ili yaishe
Nimeumia Sana, nimesikitika Sana kuuwawa mtu mmoja Kati ya wannne waliokufa Mungu aipe nguvu familia ya huyo jamaa, wengine watatu😃😃😃😃😃
 
Back
Top Bottom