Tukio la ajali ya lori la mafuta lililosababisha vifo: Je ujumbe umefika kwamba wanaolalamika ugumu wa maisha sio wapiga dili kama ilivyozoeleka?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,837
49,523
Niungane na wasamaria wema kuomboleza na kutoa pole kwa waliofikwa na janga la kuungua na moto wa mafuta
Ieleweke kwamba waliopatwa na janga walikuwa wakipambania riziki hata kama fursa hiyo haikuwa ya haki lakini walikuwa wanatafuta riziki na wengine yaliwakuta tu bila kutarajia
Hoja yangu kuu,je tukio hili linaweza kuwa limefikisha ujumbe kwa watawala kwamba kilio cha ugumu wa maisha sio cha wapiga dili bali wanyonge wanaopigiwaga chapuo na watawala? Ukiangalia video clip ya kabla ya moto kulipuka utakubaliana na mimi
Chonde chonde mtaani kugumu wenye mamlaka chukueni hatua kurekebisha sera zenu ili tupate nafuu kwenye hustle zetu maana leo ni lori usishangae ikaja lingine Mungu aepushie mbali
 
Ugumu wa maisha haujaanza Jana wala juzi. Wenye umri mkubwa watakwambia kuwa tangu enzi za waasisi wa taifa hili tumekuwa na ugumu wa maisha.

Cha muhimu ni elimu kuzingatiwa. Unapoona mafuta yamemwagika usikimbilie eneo hilo.

Wanaoweka maandishi makubwa DANGER pembeni ya malori ni watu wenye akili timamu.

Ukipuuzia neno hatari jiandae kukabiliana na gharama za upuuziaji.
 
Inasikitisha kwamba hizo tukio hazita isha hivi karibuni. Binadamu jinsi tulivyo, kumbukumbu zetu ni fupi na haswa watu waliyo na uwezo mdogo. Nafasi ilionekana na wata itumia tu bila kujali hatari zozote zitakapo kuwepo.

Kweli Mungu atuepushe tu.
 
Niungane na wasamaria wema kuomboleza na kutoa pole kwa waliofikwa na janga la kuungua na moto wa mafuta
Ieleweke kwamba waliopatwa na janga walikuwa wakipambania riziki hata kama fursa hiyo haikuwa ya haki lakini walikuwa wanatafuta riziki na wengine yaliwakuta tu bila kutarajia
Hoja yangu kuu,je tukio hili linaweza kuwa limefikisha ujumbe kwa watawala kwamba kilio cha ugumu wa maisha sio cha wapiga dili bali wanyonge wanaopigiwaga chapuo na watawala? Ukiangalia video clip ya kabla ya moto kulipuka utakubaliana na mimi
Chonde chonde mtaani kugumu wenye mamlaka chukueni hatua kurekebisha sera zenu ili tupate nafuu kwenye hustle zetu maana leo ni lori usishangae ikaja lingine Mungu aepushie mbali
Pascal Mayalla nikuulize hao nao ni wapiga dili wa Magu jamaa yako?
 
Ugumu wa maisha haujaanza Jana wala juzi. Wenye umri mkubwa watakwambia kuwa tangu enzi za waasisi wa taifa hili tumekuwa na ugumu wa maisha.

Cha muhimu ni elimu kuzingatiwa. Unapoona mafuta yamemwagika usikimbilie eneo hilo.

Wanaoweka maandishi makubwa DANGER pembeni ya malori ni watu wenye akili timamu.

Ukipuuzia neno hatari jiandae kukabiliana na gharama za upuuziaji.
Ugumu unatofautiana zile video zinaonyesha hali ni mbaya sana kwa wanyonge wanaopigiwa chapuo
 
Usitishike mkuu, Hali kama ile hutokea sana Nigeria na hufa wengi kuliko uliowaona lakini kiuchumi hatuwapati Nigeria.
Ufukara,umaskini na tamaa na kukosa tahadhari ndio chanzo hapo,hata huko Nigeria hali hiyo inawatokea wanyonge mtu mwenye uhakika wa kula hawezi fanya hivyo atasubiri wengine mchukue riski yeye anunue
 
Acha hizo wewe kuna wengine mimi naamini walienda kushangaa na wao wakapata shida. Yule mtoto nae alikuwa anasaka shilingi au
 
Ufukara,umaskini na tamaa na kukosa tahadhari ndio chanzo hapo,hata huko Nigeria hali hiyo inawatokea wanyonge mtu mwenye uhakika wa kula hawezi fanya hivyo atasubiri wengine mchukue riski yeye anunue
Mkuu huwezi kutajirisha kila mtu, mchango wa serikali una mipaka yake.

Ujamaa wa ndotoni ni lazima utoke vichwani mwetu. Tusilikuze sana hili suala la ajali.

Hao matajiri wa huko nje walijenga msisitizo katika elimu na kujituma. Sisi tunapita njia hiyo hiyo kwani hakuna ile ya mkato.
 
Pascal Mayalla nikuulize hao nao ni wapiga dili wa Magu jamaa yako?
Acheni kutumia sababu za kijinga kuhalalisha hoja zenu!!!lile hata lingekuwa Basi la abiria waswahili wangekimbilia kuiba na kuacha kuokoa wahanga,na tabia za wizi hazina masikini Wala tajiri ni hulka ya mtu!!!so hivi viposti vyenu vya hovyo hovyo kujaribu kuhalalisha wizi ili tu mpate uhalali wa kutweza utu was watanzania wote ni ujinga.wale walikuwa ni wezi Kama wezi wengine huo ndio uhalisia ndio maana hawakujisumbua hata kumuokoa dereva wa gari so kusema walikuwa wanaiba kwa sababu ni masikini ni ujinga wa kiwango Cha PhD!!
 
Mkuu huwezi kutajirisha kila mtu, mchango wa serikali una mipaka yake.

Ujamaa wa ndotoni ni lazima utoke vichwani mwetu. Tusilikuze sana hili suala la ajali.

Hao matajiri wa huko nje walijenga msisitizo katika elimu na kujituma. Sisi tunapita njia hiyo hiyo kwani hakuna ile ya mkato.
Huwezi lakini unaweza punguza maskini wakabaki wachache sana ambao ukawa unawasaidia japo kwa chakula
Hapa Tzn hakuna juhudi hizo specific kulenga kupunguza umaskini.Wewe lini umewahi sikia serikali inasema hadi mwaka fulani itapunguza umaskini kwa kiasi fulani? Serikali ya sasa inafanya kazi ya kuzindua miradi ambayo haisaidii hao vijana kujikwamua
 
Ugumu wa maisha haujaanza Jana wala juzi. Wenye umri mkubwa watakwambia kuwa tangu enzi za waasisi wa taifa hili tumekuwa na ugumu wa maisha.

Cha muhimu ni elimu kuzingatiwa. Unapoona mafuta yamemwagika usikimbilie eneo hilo.

Wanaoweka maandishi makubwa DANGER pembeni ya malori ni watu wenye akili timamu.

Ukipuuzia neno hatari jiandae kukabiliana na gharama za upuuziaji.
Sawa!
 
Hili tukio ni dogo sana kwa kujifunza. Hakika nakwambia hata sasa likipinduka tanker lingine watu wanaenda kunyonya wese. Sema kwamba laleo hawatatoa betri. Sasa kama wahanga wenyewe hawasikii je mtawala atasikia kweli.
 
Acheni kutumia sababu za kijinga kuhalalisha hoja zenu!!!lile hata lingekuwa Basi la abiria waswahili wangekimbilia kuiba na kuacha kuokoa wahanga,na tabia za wizi hazina masikini Wala tajiri ni hulka ya mtu!!!so hivi viposti vyenu vya hovyo hovyo kujaribu kuhalalisha wizi ili tu mpate uhalali wa kutweza utu was watanzania wote ni ujinga.wale walikuwa ni wezi Kama wezi wengine huo ndio uhalisia ndio maana hawakujisumbua hata kumuokoa dereva wa gari so kusema walikuwa wanaiba kwa sababu ni masikini ni ujinga wa kiwango Cha PhD!!
Hujui context ya post yangu! You must be stupid of the highest degree in deep reasoning!!
 
Huwezi lakini unaweza punguza maskini wakabaki wachache sana ambao ukawa unawasaidia japo kwa chakula
Hapa Tzn hakuna juhudi hizo specific kulenga kupunguza umaskini.Wewe lini umewahi sikia serikali inasema hadi mwaka fulani itapunguza umaskini kwa kiasi fulani? Serikali ya sasa inafanya kazi ya kuzindua miradi ambayo haisaidii hao vijana kujikwamua
Mataifa kama Brazil yanayoheshimika yameshindwa kuwatajirisha mamilioni ya vijana waliopo katika miji yao sembuse sisi.

Nigeria inayo idadi ya watu karibu milioni 200, imeshindwa kuwatafutia ajira mamilioni ya vijana.

Unapokuwa na rundo la vijana changamoto ya muhimu ni kutengeneza mazingira kwa mfano kupitia michezo, serikali inakuwa rafiki katika uwekezaji michezoni, na wao vijana wanachokipata kinaajiri wanaowazunguka.

Brazil na Nigeria wanajaribu kupunguza tatizo hilo kupitia kwenye sekta kama vile sinema na mpira wa miguu.

Ujamaa wa kusema serikali iwaajiri sehemu kubwa ya vijana, ulishashindwa kule ulaya ya mashariki tangu miaka ile ya tisini mwanzoni.
 
Kuna mambo yanasikitisha sana...

Huo ni mlipuko wa lori la mafuta umeleta maafa yote hayo...

Bado mlipuko wa ukosefu wa ajira... sijui utaleta madhara kiasi gani...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom