Tukio hili linaweza kuwa ushahidi kwamba tukifa tunarudi duniani kwa miili mingine??

Majinni maovu hayo yanacheza na akili za watu.

Nakuunga mkono, hayo ni mapepo tu. Wapo watu wengi wenye maroho hayo ambao huweza kwa usahihi kabisa wakaelezea maisha ya utotoni ya mtu fulani.

Pia, waganga wa maruhani (majini yajiitayo Sharif) wanaweza elezea historia ya kale ya mtu fulani.

Huyo mtoto ana mapepo ya utambuzi. Mapepo aina hii yamejaa kwa wajiitao eti ni mitume na manabii.

Maandiko yanasema "zichunguzeni hizo roho".
 
Ukifa umekufa unasubiri azabu yako kwa makosa uliyotenda

Story za uyo punjaby ni za kijini na iyo asa ndio kaze yake ni kama ramli hawakoseagi uo ni uchawi men
 
Soma vitabu vya Lobsang Rampa ujifunze nini maana ya Reincarnation

Ahha!! Yanini mwenzangu ni kuchanganyana tu haya yenyewe ya kwenye dini yangu nayaona yananichanganya tu. Ila Asante nitajaribu kutafuta nione yaliyomo yamo...
 
Kuna madhehebu ya wahindi wanaamini hivo kiwa mtu akifa basi huzaliwa tena mahala pengine kama ulivyoolezea,hususan waliodhulumiwa ili kulipiza visasi....

Kuna movie pia yaitwa om shanti om
 
Kuna maisha yalikuwepo kabla ya haya maisha, na kuna maisha yatakuwepo baada ya haya maisha.
Kuna physical body ambayo ni huu mwili wa kawaida na kuna astaral body ambao upo katika hali ya roho (hauonekani) na kila binadamu anao.
Hivi hujawahi kuhisi kama umeshawahi kufika mahali fulani lakini hukumbuki ulifikaje na hata hivyo utakuta ni mara ya kwanza kufika mahali hapo!
Kwa mfano mm naishi dar, sijawahi kabisa kufika bukoba.
Lakini inatokea siku naenda Bukoba, baada ya kufika mahali fulani, naanza kupata picha kama nishawahi kufika siku za nyuma lakini sitakumbuka nilifikaje mahali pale kwa sababu kwa record za safari zangu za maisha ya kibinadami, sijawahi kufika.
Au ukamwona mtu kwa mara ya kwanza kabisa, halafu ukawa unahisi kama mlishaonana zamani but hukumbuki ni wapi!
Charge inaisha, ntarudi.
Hii inaitwa DEJA VU...walahii hii ni kitu cha kwe, kweli kappsa.
 
Naamini maisha baada ya haya ya dunia yapo, kwani mwanadamu ana roho ambayo kimsingi ndio mwanadamu halisi na roho hiyo haifi. Ila sidhani kama baada ya kufa mtu anazaliwa tena mara moja.

Ukweli mwingine ni uwepo wa uongo mkubwa kutoka kwa mapepo ambayo hutumwa na shetani ambaye ni baba wa uongo. Hata katika imani zetu za kiafrica watu huamini sana kwamba wafu waweza kuongea na kudai mambo fulani yafanywe kwa amri yao. Lakini hayo huwa ni uongo kutoka kwa mapepo na ni hatari sana kwa wanaoamini.

Huu uzi ni mzuri sana.

Kwanza wengi wetu tunashindwa kutofautisha maisha binafsi na maisha ya kufuata dini fulani. Kila mtu ana nafsi yake ambayo huwezi ku-generalise kwa kutumia maandiko yoyote yale. Ingawa haya maandiko yanasaidia kutuunganisha kama binadamu (mwili mmoja).

Je unajua ni kwa nini ulizaliwa kwa huyo unayemwita mama yako na baba yako? Ni nani aliyeamua uzaliwe kati yao? Na hayo maamuzi hufanyika vipi? Kwa kifupi ni kuwa nafsi yako ndio iliyochagua mahali pa kuingilia duniani.

Hivyo basi nafsi yako inamtambua Mungu. Vile vile nafsi yako inaweza kuwa ni nafsi iliyoamua kurudi duniani. Sasa basi, unapoingia duniani ndipo unakutana na hizi dini, ambazo ni taasisi za kibinadamu zenye malengo tofauti katika kumwabudu Mungu. Pitia historia ya dini tofauti na si maandiko (vitabu) vya dini husika.

Kwa kujua historia ndipo utaona binadamu tuna nguvu inayotuunganisha (Mungu) ingawa dini zinatutenganisha. Angalia matambiko ya maeneo mbali mbali yanavyofanywa, almost yote yanafanana kama kuchinja na kusoma utumbo. wanafanya wachaga, wasomali, na lost tribe of Papua New Guinea. Ukiangalia kijiografia ni maeneo mbali mbali lakini wanafanya vitu vinavyofanana je waliwahi kuishi pamoja?

Kwa hivyo basi, hili swala la mtoto kuzaliwa na kuwa na kumbukumbu za kuishi awali linawezekana kabisa ndugu zangu. Musikurupuke kukataa kama hujawahi kufanya utafiti.

Hayo mambo ya kusema kuwa ni mambo ya kishetani ni mapandikizi yaliyowekwa na waanzisha dini zetu mbali mbali ili waumini waweze kuwafuata. Kama umenielewa hapo juu kuwa maisha yako ni tofauti na dini, ulipozaliwa ulikuwa hauna dini ndo maana utabatizwa au utasilimishwa.
 
Mtoto mmoja wa kiume huko India aliwahi kuwaacha hoi wazazi wake baada ya kuanza kudai aliwahi kuishi kabla ya kizaliwa

Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.

Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.

Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.

Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.

Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.

Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.

Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.

Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .

Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.

Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.

Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.

Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.

Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.

Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.

Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibika

Jambo hili linathibitisha maisha baada ya kifo

Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.

Karibuni kwa maoni ndugu zangu woote!
Shetani ni baba wa uongo!!!! Anachezea akili za watu tu. Hii haiwezekani hata kidogo.
 
Mkuu Huyu Bibi Kiroboto Hili Si Jukwaa Lake,kazi Yake Ni Kutetea Magamba.
Mwacheni Faiza nyie Bavicha.. Hii topic inahusiana vipi na siasa.Yaani mtu akikushinda kwenye siasa ndo unamchukia kila mahali ni udwanzi huo
 
Back
Top Bottom