Tukio hili linaweza kuwa ushahidi kwamba tukifa tunarudi duniani kwa miili mingine??

mkuu Eiyer
kwanza naomba utupe source kwamba wewe umeipatia wapi?? pili hizi tamthiliya za kusadikika tu, zilizofanywa na familia hzo mbili.

Yaani unayarahisisha mambo tu kama vile ambavyo unakaa nyuma ya monitor yako na kuandika unachoijisikia ....

Kaazi kweli kweli!
 
Sitaki kuibeza hii habari... Inawezekan ikawa na ukweli au uhalisia fulani... Mara nyingi mimi binafsi nimekuwa na fikra hizo.. kwamba mtu akifa hafi completely, bali anaenda kuzaliwa mwingine the same mahala pengine.... Na hili linanijia mara nyingi kwani kuna nyakati nafanya kitu flani halafu hapo hapo fikra zinaniambia kwamba nilishafanya kitu kama hicho mahala flani na the same way.. So nna wasi wasi na maisha yetu binadamu kwamba ni recycling..

Hiyo inaitwa deja vu:

Déjà vu, from French, literally "already seen", is the phenomenon of having the strong sensation that an event or experience currently being experienced has been experienced in the past, regardless of whether it has actually happened.

Ila hii ya mtoto ni kweli kuna kitu kinaitwa "spirit" kwa kiingereza ambacho kwa kiswahili tunazo tafsiri nyingi kama malaika, pepo, roho, jini, mzimu nk. Hivi vitu vipo na kila mmoja anacho cha aina yake. Ni kutambua na kutumia ipasavyo.

Mfano mtu anakuwa na uwezo wa kuponya tunasema ana roho mtakatifu au "holy spirit"; mwingine anakuwa na uwezo wa kutabiri tunasema ana uwezo wa kuwasiliana bila kutumia njia za kawaida za mawasiliano au "telepathy"; na hivyo mwingine anazaliwa na kuwa na kumbukumbu za kifo chake, hii inaweza kuwa ni kwa ajili ya kusuluhisha jambo lake au kutoa ufafanuzi wa namna kifo chake kilivyotokea ili haki itendeke "life after death".

Kwa hiyo basi sisi binadamu tuna uwezo tofauti tofauti ila hizi dini (imani) zetu zinatuelekeza katika hali ya amani ya kutumia nguvu zetu na kuziita kuwa ni nguvu za giza, pepo wachafu, shetani nk.

Jitambue ili uishi madhumuni ya maisha yako hapa duniani.
 
je wewe au mimi unakumbuka tulikua wakina nani uko nyuma hakuna kitu km icho inamaana yeye pekee yake ndio mwenye kumbukumbu sahihi
 
kama unaamini hivyo, pia ujiulize ongezeko la watu duniani linatoka wapi?
 
Inamaana watu wangekua wanajirudia leo hii population ingekuaje?au balance ya wanao kufa na kuzaliwa ipoje?je existence ya mwanadamu after death n mda gan namanisha evolution kama hakuna jibu MUNGU atabaki kuwa MUNGU wengne hao n mapepo tu hakuna lolote.
 
mkuu Eiyer
kwanza naomba utupe source kwamba wewe umeipatia wapi?? pili hizi tamthiliya za kusadikika tu, zilizofanywa na familia hzo mbili.

Unataka source ili kule kwenye blog yako ujifanye umefukunyua? Source ni Eiyer wa JF mkuu .....hahahahahaha ......
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilikua naitwa 2pac au makaveli kabla sijafa...tena nakumbuka nlikua nachana hip hop...na niliuawa kwa risasi....nawakumbuka hadi marafiki zangu kina suge knight!!!
 
Tofauti yetu na wao huwa inaanzia hapa. Sisi hatuna muda wa kutafiti, kazi yetu ni kutafuta upenyo wa kutoa sababu isiyoelezea.

Btw, Mkuu Eiyer shukrani kwa hii "sharing", ila haya mambo huwa yananoga sana yakiambatanishwa na "source"

Majinni maovu hayo yanacheza na akili za watu.
 
Nch hiyohiyo wanaamin kwamba yule mjus mweupe\gong'ole ni watu wamefufu walio kufa zaman. Chek na hii alafu uje na uongo
 
Mkuu Eiyer, hebu jiulize wewe mwenyewe ukikumbuka unaona kama ulipata kuishi kabla ya mwaka unaoutambua kuwa ulizaliwa? Mimi sikumbuki kama nilipata kuishi kabla ya kuzaliwa na naamini hata wana jukwaa humu hawajui kama walipata kuishi kabla. Mbona huyo peke yake?
 
Last edited by a moderator:
2 Kor 2:11 Maana shetani mwenyewe hujigeauza awe mfano wa malaika wa nuru; Ufu 16:13 Nikaona roho tatu za uchafu zinazofanana na vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita siku ile kuu ya Mungu Mwenyeai. 15 Tazama naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake
 
Back
Top Bottom