Tukio hili linatupa fundisho gani?

Jogoo hasababishi yai we mjinga, ndo maana tunasema lumumba kumejaa watu wa milembe, kwani wale kuku wa mayai wanaotaga kila siku umewahi kuona jogoo mle ndani?
Wakubwa wakiongea, watoto tuacheni. Ona sasa unarukia treni hujui mbele wapi, nyuma wapi na linaenda wapi!
 
Kifo ni jambo la kuhuzunisha na binadamu wanapaswa kufarijiana kitokeapo.

Lakini vipi pale unapohuzunika na kifo cha jirani yako lakini wanae wana andamana kushangilia kwa vifijo na furaha kifo cha baba yao?
Na kama baba yao ni rafiki yako unajifunza nini hasa kwa vile kuna usemi usemao "ukitaka kumfahamu MTU angalia rafiki zake"?

Raisi Magufuli kaonyesha kuhudhunishwa na kifo cha rafiki yake Rais Nkurunziza na akatoa twita ya majonzi yake.

View attachment 1475678

Lakini RAIA wa Burundi wenyewe wanaandamana kufurahia kifo chake kwa nini?
Angalia jinsi wanavyo onyesha furaha yao!
Mi nachojua neno "NKURUNZINZA" limeingia kama tafsiri isiyo rasmi ya mtu anaeng'ang'ania madaraka au kitu fulani hata kama muda wake ushapita.

Yaani umekua msamiati mpya kama ule wa "KIHIYO"
 
Jogoo hasababishi yai we mjinga, ndo maana tunasema lumumba kumejaa watu wa milembe, kwani wale kuku wa mayai wanaotaga kila siku umewahi kuona jogoo mle ndani?
Huyo kilaza wa Lumumba anadhani Jogoo ndo anatungisha mimba ya Yai. Hiyo ndo aina ya watu tunaobishana nao kila siku wanatoka mishipa ya shingo kumtetea mtu kama Ndugai
 
Oneni maandamano yao yalivyo

View attachment 1475449
Kama kweli ni maandamano ya kufurahia kifo ni upumbavu,kwann kwa wingi huo wasingejitokeza kupinga uovu na udhalimu wa muuaji akiwa hai ili kumuonyesha awamtaki kwa kumfurusha madarakani na sio kusubiria amekufa.
All in all tunawaonea wivu Sana wenzetu kwa kufiwa maana kifo cha Mamba mtoni maisha ya wengi yameokoka.
 
Kizazi cha sasa cha waafrika hakichekani na kizazi cha watumwa the same kundi la wachache linaswaga na kuburuza wengi hii ipo Africa nzima ni sawa na wasagwa watumwa 3 wakiswaga lundo la watumwa enzi za biashara za utumwa.Angalau kidogo kizazi cha wapigania Uhuru kilikuwa strong pia kimshukuru kwa kua mkoloni alikuwa mweupe angekuwa mweusi asingetoka.
 
Huyo kilaza wa Lumumba anadhani Jogoo ndo anatungisha mimba ya Yai. Hiyo ndo aina ya watu tunaobishana nao kila siku wanatoka mishipa ya shingo kumtetea mtu kama Ndugai
Hiyo inaitwa lugha ya picha nyie wa kizazi cha mwendokasi. Hatuko kwenye mjadala wa anatomy ya kuku hapa. Msije mkakakomaa kwenda kusomba text books zenu kuja kubishana maana najua mko free baada ya shule kufungwa.
 
Hakuna lugha ya picha we kilaza. Picha ulioileta kutengeneza Lugha haifananii, we kubali tu umechemka na utushukuru kwa kukupatia hii elimu, manake ulikua huijui hapo kabla.
 
Kifo ni jambo la kuhuzunisha na binadamu wanapaswa kufarijiana kitokeapo.

Lakini vipi pale unapohuzunika na kifo cha jirani yako lakini wanae wana andamana kushangilia kwa vifijo na furaha kifo cha baba yao?
Na kama baba yao ni rafiki yako unajifunza nini hasa kwa vile kuna usemi usemao "ukitaka kumfahamu MTU angalia rafiki zake"?

Raisi Magufuli kaonyesha kuhudhunishwa na kifo cha rafiki yake Rais Nkurunziza na akatoa twita ya majonzi yake.

View attachment 1475678

Lakini RAIA wa Burundi wenyewe wanaandamana kufurahia kifo chake kwa nini?
Angalia jinsi wanavyo onyesha furaha yao!
Haya Mambo kuyaelewa ni Hadi uwe na akili na pia ujue kuhusu Mambo ya universe,ukiyajua haya huwezi ukimbiza upepo.Angalau wenzetu waislamu kitendo cha kufanya ibada kila siku kinawashape na kujua kusudio la maisha ni nini.Ukilishajua kusudio la maisha utohitaji kuabudiwa, kuumiza watu,kujilimbikiza,kufisadi, umaarufu,nk ili ukamilike.
 
Kama kweli ni maandamano ya kufurahia kifo ni upumbavu,kwann kwa wingi huo wasingejitokeza kupinga uovu na udhalimu wa muuaji akiwa hai ili kumuonyesha awamtaki kwa kumfurusha madarakani na sio kusubiria amekufa.
All in all tunawaonea wivu Sana wenzetu kwa kufiwa maana kifo cha Mamba mtoni maisha ya wengi yameokoka.
Mkuu tunafanana nao mazingira. Umesahau "kipigo cha mbwa koko"? Maisha ya baadhi ya nchi ni hatarishi sana, Uhuru wa kuandamana uko kwenye makaratasi na hauheshimiwi kabisa na kupoteza maisha ni kawaida tuu.
 
Akifa jiwe watanzania tutashangalia Kama warundi
Tetesi tuu za kigogo2014 baada ya kutoka Lindi zilileta taharuki kubwa sana. Kwa maumivu nakumbuka Siku ya kutoka hadharani kuna mtu alisindikizwa na wimbo wa Gozbeth wa "hauwezi kushindana na mwamadamu mwenye kinywa"
Nilidhani baada ya pale somo litakuwa limeeleweka lakini kumbe ilikuwa kama kuchochea moyo mgumu wa farao
 
Kifo ni jambo la kuhuzunisha na binadamu wanapaswa kufarijiana kitokeapo.

Lakini vipi pale unapohuzunika na kifo cha jirani yako lakini wanae wana andamana kushangilia kwa vifijo na furaha kifo cha baba yao?
Na kama baba yao ni rafiki yako unajifunza nini hasa kwa vile kuna usemi usemao "ukitaka kumfahamu MTU angalia rafiki zake"?

Raisi Magufuli kaonyesha kuhudhunishwa na kifo cha rafiki yake Rais Nkurunziza na akatoa twita ya majonzi yake.

View attachment 1475678

Lakini RAIA wa Burundi wenyewe wanaandamana kufurahia kifo chake kwa nini?
Angalia jinsi wanavyo onyesha furaha yao!
Linatufundisha mambo mawili.moja linatufundisha kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja na la pili linatufundisha kuwa Covid 19 haiko fair kihivyo otherwise ilipaswa ifanye the same na huku pia,ili wakapange Mambo ya uchumi na kutawala milele huko mbele
 
Naomba mniondoe kwenye kundi la watz waliosikitishwa na kifo cha huyu nduli, mimi hufurahishwa na VIFO VYA MADIKTETA HAIJALISHI ANATOKEA WAPI
Silika ya ukatili Mara nyingi huwa ni watu ambao wame
Mkuu tunafanana nao mazingira. Umesahau "kipigo cha mbwa koko"? Maisha ya baadhi ya nchi ni hatarishi sana, Uhuru wa kuandamana uko kwenye makaratasi na hauheshimiwi kabisa na kupoteza maisha ni kawaida tuu.
Uoga wa waafrika ndio kaburi la wengi, tofauti na wenzetu heshima haiji bila kudundana,Kati ya watawala na watawaliwa.
Kwa umoja wao kwa wingi wakijitokeza kwa pamoja ni lzm mtawala atafute mlango.Wachache watakaokufa ndio ukombozi wa wengi.Waafrika ni sawa na nyumbu 2000 kumuogopa Simba mmoja
 
Mi nachojua neno "NKURUNZINZA" limeingia kama tafsiri isiyo rasmi ya mtu anaeng'ang'ania madaraka au kitu fulani hata kama muda wake ushapita.

Yaani umekua msamiati mpya kama ule wa "KIHIYO"
Lipo mbona hata kabla marehemu ajawa maiti.Tafsiri ya neno Nkurunzinza ni mtu asiyeridhika asiyetosheka na madaraka
 
Ameuwa watu elfu 20,na laki 6 wamekimbia ukimbizini.Mungu awabariki Sana wazungu hasa wa USA na Wacanada ndio wamechukua warundi na wacongo wengi Sana kuwapeleka kuishi kwao kuwafuta machozi ya ukimbizi na dhuluma za mateso toka kwa ndugu zao waafrika.
 
Hakuna lugha ya picha we kilaza. Picha ulioileta kutengeneza Lugha haifananii, we kubali tu umechemka na utushukuru kwa kukupatia hii elimu, manake ulikua huijui hapo kabla.
Haya, tusubiri ikija mada kuhusu kuku na mayai yao tutashtuana tuendelee maana nikikuambia lugha ya jazanda ndio tutazidi kupoteana.
 
Back
Top Bottom