Tukio hili linaonyesha ni vigumu sana kuiondoa CCM madarakani

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Kwa mtu anayechambua na kuchanganua siasa za Tanzania atakubaliana na mimi kuwa ni vigumu sana kuiondoa CCM madarakani.

Tukio la kuaga Mwili wa Marehemu Kingunge Ngombare-Mwiru limefikirisha zaidi na kunionyesha jinsi ilivyo vigumu sana kuchukua dola kutoka CCM.

Nilimuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akipepesa macho huku na kule kwenye eneo la wageni mashuhuli(VIP) lakini kila akiangalia huku na kule alikuwa anakutana na nyuso za wanaCCM wastaafu au waliobado active katika chama na serikali.

Tukio la Freeman Mbowe kuzungukwa na wanaCCM ambao wengi wao ni statesman lilinifikirisha sana kuhusu hatima ya CCM lakini pia majukumu mazito na magumu ya vyama vya upinzani katika kuchukua dola kutoka CCM.

Tukio hili limeondosha shaka kuwa CCM bado ni chama dola lakini pia vyama vya upinzani nchini vina jukumu ambalo liko juu ya uwezo wao. Huu ni ukweli mchungu kwa wapinzani wa kweli nchini.

Kuna baadhi ya watu hupenda kuja na kauli wakisema, kama Roman Empire ilianguka, kwa nini CCM isianguke? Ikumbukwe kuwa kuanguka kwa Roman Empire kulichukua miaka zaidi ya 1000. Ni kweli kuna siku CCM itaanguka lakini kwa upinzani huu sioni kama siku hiyo itatokea.

Tukio hili linatoa somo linalosema, ni bora vyama vya upinzani vikaendelea na siasa za uanaharakati na kupata wabunge lakini sio siasa za kupata dola/madaraka. Bado sana.

Kazi iliyofanywa na waasisi wa CCM katika kujenga msingi wa chama dola itachukua muda mrefu sana kwa wapinzani kuuvunja kwa sabahu hata ambao tunadhani ni wapinzani kumbe sio wapinzani bali ni kama watoto waliochukizwa tu na baba/Mama yao na kususa lakini mahitaji yao yakitimizwa wanarudi nyumbani.

Wakati mwingine kuukubali ukweli wa kimazingira katika maisha yako sio kosa!

Ukitaka kumuona Mbowe alivyokuwa akipepesa macho angalia kuanzia dakika ya 2:50.
[MEDIA]
 
We mwenyewe ccm damu,,kwaiyo una Haki ya kusifia chama chako cha majizi na kukosoa viongozi wa opposition
Mimi ninakuambia ukweli kama ulivyodhihirika katika mkusanyo wa kuaga Marehemu Kingunge.

Kama huwezi kusoma, hata picha huwezi kuangalia?
 
Ni kweli unayo yasema hasa kwa taifa lililojaa wajinga na masikini wa akili na Mali kama wewe ni vigumu sana kuiondoa
Huoni kuwa wewe ndio mwenye tatizo kwa sababu unakaa kwenye taifa lililojaa wajinga na masikini wa akili wakati wewe ni tajiri wa akili na umeelimika!
 
Ni kweli unayo yasema hasa kwa taifa lililojaa wajinga na masikini wa akili na Mali kama wewe ni vigumu sana kuiondoa
Angalia chama chenu kinavyopukutika, mkaambiwa lowasa fisadi hafai etc, mkaja badilishiwa gia kwamba lowasa anafaa na mkamchagua.
Na nakuhakikishia 2020 ndio maziko yenu.
 
Bro!!!! Umri unaenda huo utaendelea kuuza kapelo na scuff za ccm hadi lini???
Je ccm ikiendelea kukaa madarakani wewe utapata nini?.....wenzio kila siku wanakula shavu wewe unaishia kulamba buku 7 ambazo kwa maisha ya leo sio kitu ebu shtuka basi kutoka usingizini
Bro, kwani umri wako hauendi?

Kwa hiyo unataka niuze kombati za CHADEMA kama wewe?

Kwani wewe CCM ikishindwa utafaidika nini?

Anza kwanza wewe kushtuka kabla ya kunipa ushauri!
 
Wajinga na maskini wa akili ni chadema. Angalia chama chenu kinavyopukutika, mkaambiwa lowasa fisadi hafai etc, mkaja badilishiwa gia kwamba lowasa anafaa na mlivyo mbumbumbu mkamchagua.
Sijawai ona uwendawazimu wa aina hiyo maishani mwangu.
Ndio maana nasema wajinga na maskini wa akili ni nyinyi hapo.
Na nakuhakikishia 2020 ndio maziko yenu.

Hayo ni maoni yako

Huyo lowasa kama fisadi , ninyi si mna mahakama ya mafisadi mnangoja nini kumfungulia mashitaka huko??

Pili Mimi sina chama

Tatu kwa akili zangu timamu hao wanaohama vyama ni matumizi mabaya ya pesa zenu za kodi na bado hamhoji hapo nani mjinga

Punguza ushabiki hapa sio simba na yanga hayo ni maisha yako wewe na watoto wako
 
Ccm ni wababe wakandamizaji wenye mawazo mgando waonevu warafi wenye tamaa wasio tenda haki wanyang'anyi wabaka uhuru wa watu, hawajahi kushinda hata mara moja tangu vyama vingi viwepo wao wanatumia nguvu ya dola tu
 
Ni kweli unayo yasema hasa kwa taifa lililojaa wajinga na masikini wa akili na Mali kama wewe ni vigumu sana kuiondoa
Hata vipofu huongozana wakafika itakuwa kwa wajinga, maskini wa akili na mali ili mradi ujinga wao umaskini wao wa akili na mali unawapekeka wanakokutaka kwenda watafika tu
 
Back
Top Bottom