Tukio gani ulifanya shuleni mpaka leo haujalisahau?

Nilisababisha darasa zima kukosa hesabu

Kama sikosei tulikiwa darasa la tano au la sita mwalimu wa hesabu alikiwa anatupa majaribio ya wiki na mwezi harafu anabandika matokeo kwenye ubao.

Majibu ya mvulana yaliandikwa kwa wino wa blue wakati nyekundu ilikuwa ya watoto wa kike.

Sasa alikuwa na mtindo wa kichukua daftari au karatasi tatu ambazo anasahihisha njia mpaka jibu ktk darasa langu tulikuwa wanafunzi watatu ambao akisahihisha mojawapo anaifanya marking scheme, sasa mtihani ule akachukua karatasi la kwanza akakosa swali la 11 akachukua la mwingine naye akakosa la 11 kuchukua langu mpaka swali la 18 nimepata yote akaamini hata yanayofuta nimepata yote kumbe lililokuwa linafuata nimekosa nikapata

Malinipiga kishenzi waliolipata hafu wamekoseshwa
 
Me nilikuwa sijaleta visa lakini acha nianze na hiki kimojawapo, wakati niko secondary kuna mwalimu mmoja alikuwa mtata sana shule nzima anaogopeka mwembamba sana hana hata nyama, yaani hautamani hata kupishana naye hakawii kukupa msala, sasa kwa kuwa nilihamia kutoka shule nyingine nikasema acha siku moja nimtingishe kaingia kwenye dormitory asubuhi asubuhi kaanza kuchapa washikaji ambao hawajadamka vitandani alivyofika kwangu nikajifanya kama niko usingizini, alivyonikurupua na fimbo aisee nilipiga ngumi za mvululizo na kichwa juu nikijifanya nina wenge la usingizi, masela wakaanza kupiga kelele oya zeebaba ni mwalimu huyo ndio nikajifanya kama wenge limekata nikaanza kuomba msamaha hapo hapo akaniambia niende baadaye ofisin akaenda kunisemea kwa walimu wengine japo walimu siku zote wako upande wao mmoja tu ndio alikuwa ananitetea kwamba yawezekana alikuwa na usingizi sasa kama ww umemchapa akiwa usingizini ndio hasara zake hizo.

Nilipewa adhabu lakini ndio ilikuwa mwisho wa yule teacher kuja Dom asubuhi asubuhi, tulikuwa hatusemeshani mpaka nimemaliza shule.

Visa vingine vitaendelea viko vingi tu, ipo ya kuchukua counter book za form one baada ya msela wa form 6 kujifanya mwalimu wa hesabu me nikatumwa nikusanye madaftari tukapita nayo yote yakiwa mapya yameandikwa ukurasa mmoja tu
 
Kama kichwa cha habari kinavyoonyesha hapo juu katika harakati za kupata elimu kuna kukutana na watu wengi sana wakiwemo watoto watukutu na wakati mwingine kujifunza tabia mbaya!! tililika hapa ni kisa gani hautakisahau?

1: Nakumbuka **** siku nipo mtwara technical form2 2011 siku hiyo mida ya prepo nilichoka kwenda kusoma na ukikosekana ni msala kinoma roko lazima ipite bhas nikapata wazo la kwenda kukata fuse kweny transfoma sijui nilipata wap ujasir nikaenda kuchomoa fuse na kuitupa mbali sana

2:nipo form 3 nikahamia moshi technical siku hiyo nakumbuka baba angu alipata likizo ya kikaz akaamua kuja kunisalimia xul

bhas niko class nikaitwa kufika pale mbele ya baba angu na walimu wengine km wanidhamu,headmaster,sec master na walimu wanoko wanoko bahat mbaya nilikuw nmevaa mnyonyo(modo)ikachanwa mpk mapajani na walet yangu ilikuw imetuma wakajua nmeficha simu, bhas kuanza kuipekua wakakutana na paket moja ya kondom msala ukaanzia hapo nikaambiwa nitaje hizo “condom mbili nilimla nan hapo xul na nikakutwa na kucha ndefu moja nikaulizwa ninamchomaga nan vidole kweny K(tunda)”hilo ni swali kutoka kwa mkuu wa shule ilikuw ni baaalaaaaaa ila cha ajabu nikalimwa stiki 3 tu tena ni baba angu aliomba anichape nikajua nikitoka hapo mzee wangu atanizingua san kuhus huo uhuni wa condom lkn cha ajabu mpk na leo hajawai kuniuliza na nilivyoachiwa pale walimu wakaanza kuniita mwanaume wa kwel kuwa natembea na silaha wakat ile siku walikuwa wananichongea
 
Duuuh asee kuna tukio moja ilo nipo kidato nilikuwa na washkaji zangu wanne tulikuwa na ki gang chetu tulikiita haki elimu kama unavyojua tulikuwa haki elimu kweli, namaanisha tulikuwa darasani tunafaulu vzri,na tulikuwa bangi tunaivuta kweli ssa tukio nisilolisahau ni hili

Siku hyo nyumban kulikuwa na birthday ya brow nyumban mida kama ya saa 10 jion, bi mkubwa akanambia we nenda shule ila uwah kurud ili nisikose misosi,Kama unavyojua haki elimu sijawah kuipinga shule, kweli nikaenda shule ila moyoni nikasema huo msosi utanikoma niki uvutia bangi ndo nitakula vizur na ntaula kwa wingi nikaingia asubuhi,kufika mida wa mapumziko sijala kutegemea nikirud nyumban ntakula chakula kingi zaidi tena ni kizur kuliko cha shule, pesa yote ya kula nikaenda kununua bangi, kweli nilivyotoka mapumziko nikanunua puri langu la elfu 2 nikamoka lile puri mpaka nikabakiza vi stock viwili hapo ndo nikakumbuka kurud darasan, kufka class nikasinzia had mida ya kutoka mana nilikuwa high, kweli mida ya kutoka gang langu la haki elimu likanishtua tukapitia maskan tuka nyonga kadhaa nikitegemea tutaondoka mapema, daaah bhas hilo ndo likawa kosa nikanyonga vistock tuwili nikajikuta nimesinzia hadi mishale ya saa moja na nusu nipo maskan kwa mwana nimembonji duuh njaa ilikuwa inaniuma, nikapiga moyo konde nikasema kwa kuwa nilienda shule na home wanajua lazma wataniwekea msosi,kweli kufika om naulizia msosi wangu bi mkubwa ananiambia kuna ngeni kaja nikaona wwe umechelewa kurud nikampa chakula chako ila dada yako anasonga ugali mtakula pamoja daaah kuangalia sahan alokula mgeni pemben nakuta chupa ya soda mifupa ya kuku maganda ya ndizi alafu ulikuwa wali wa pilau roho iliniuma zaidi pembeni nakuta vipunje punje vya keki daaah nilishindwa kujua nimlaumu nani🤠😭😭😭😭😭
 
Pole sana Bangi haifai
 
1. Kipindi niko primary enzi za mwalimu shule wetu ilikuwa na michungwa na michenza kibao ingawa ni mjini (siku hizi hata ukipanda ua halioti mijitu ilvyo na dhambi). Sasa kuna siku tulikuwa na watoto wenzangu tukahamua muda wa breki kwenda kuiba machungwa, sasa ile tumeingia kwa kujificha shambani tukakutana na dada mmoja alikuwa darasa la chini amejificha anakata gogo, aisee utoto acha uitwe utoto yaani tulisahau issue ya machungwa tunamtoa nduki kama mwizi ingawa alituzidi kukata mitaa tukashindwa kumkamata. Mpaka leo uwa najiuliza kama tungemkamata tungemchukulia hatua gani zaidi ya kumchoresha tu

2. Nyingine wakati tuko darasa la tano tulitoroka shule kipindi cha breki ya saa sita tukaenda kuiba zambarau kwenye mti uliokuwa kwenye shirika moja kubwa nchini. Basi kuna mwenzangu mmoja akapanda mie niko chini naokota zambarau naweka kwenye mfuko. Jamaa juu kule akakutana na bonge la kinyonga uso kwa uso akawa anapiga kelele kinyongaa kinyongaa jamaa alijiachia kufika chini alifikia kichwa akapoteza uhai hivi naona. Ilibidi niweke ule mfuko wa zambarau pembeni yake nikakimbia kurudi darasani nikajikausha huku roho ikinienda mbio. Katika akili yangu nilijua nikigundulika nilikuwa nae naweza kukamatwa na kupelekwa jela na kunyongwa. Nilijiapiza kutomwambia mtu. Baadae ule mwili ulionekana na ikagongwa kengele shule kuelezwa msiba. Nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana na sikulala karibia wiki nzima nikikumbuka lile tukio.

Mpaka leo hakuna anayejua kama mie niliona lile tukio na leo ndio mara ya kwanza naliweka hadharani na uwa naliota sana lile tukio mpaka nimefikia umri huu wa mzee kijana

3. Kuna kipindi niko std 6 nilimpenda sana binti mmoja (sasa hivi ni mke wa mjeshi kiongozi fulani mkubwa wa JWTZ). Sasa kumwambia nilikuwa siwezi kabisa na nilichokuwa nafanya akiniangalia namkonyeza au nabenua kope hivi naye anajibu kwa kufanya kama nilivyomfanyia. Issue ilikuwa nzito kwenye kumwambia na nilikuwa nampenda sana toka moyoni. Sasa kuna siku kuna jamaa mmoja akamla halafu wakafumwa vichakani huko na habari inaenea shule nzima. Niliumia moyo kama nimegongewa mke. Nilikuja kumfuata na kumuuliza kwa nini alitembea na yule jamaa wakati anajua nampenda (nilienda kama kumlaumu hivi) kumbe wakati namwambia vile nae alikuwa amevurugwa kisaikolojia na lile tukio na kufumwa, aisee alinitoa mkuku kwa kunirushia maneno makali sana ya maudhi. Toka hapo sikutongoza tena mpaka nafika form three
 
Asante mdau kwakuweka mambo yaliyotokea, nimesikitika sana juu ya mwenzio aliyefariki dah Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
Niliiba Muhuri wa Shule nikawa naandika Barua za michango nagonga muhuri Nampelekea Mzee Father ,navuta mpunga Natia Mfukoni.

Nilikuja kukamatwa baada ya kuutumia Muhuri ktk karatasi za Kupigia kura ,Maana nilikua Nampango mkakati wa kuwaweka madarakani watu wangu,
Baazi nilifanikiwa kuwaweka madarakani, hekaheka ilikuja ktk kura za Head Boy(HP),ndiko nilipofumwa na siraha zangu za maangamizi mfukoni, kumbe kunajamaa alichora ile Raman ya Mimi kudakwa. Kibaya zaidi nikakutwa na ule muhuri ktk Bag yangu. Taarifa zikafika kwa mzee Father.
Kilichoendelea sitokuja sahau

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
We naye ulikuwa balaaa hakuna muhuri wa ikulu hapo kweli? LOL
 
2001 hivi drs 4 nilichapwa viboko vya matakoni nikamjambia mwl adi Ali ahirisha kuendelea kunichapa.
 
Daah,,Mimi nikiwa form two nilikuwa na kundi langu hilo shule hatukai saa nne tushatoroka, basi siku ya kufunga mwezi wa 6 na 12 shule ilikuwa na utaratibu wa kuita wazazi wafanye kikao, kwa kundi langu hiyo ni fursa ndo hatuonekani shuleni kabisa tangu asubuhi ila home natoka nimekula uniform na beg kama kawa najua mwenyew napoelekea. Bas bwana siku ya kikao mjomba akatimba school ila Mimi sipo shule wakafanya kikao chao mjomba akawa kinara wa kuongea akawa anaponda sana wazazi wanaoshindwa kulea watoto wao vizuri mpaka wanakuwa wahuni, hawaji shule, wanavaa milegezo na mambo kibaooooo. Baada ya kikao wakaitwa wanafunzi mule hall ili kusomewa matokeo(ten best) kwa kila darasa. Utaratibu ilikuwa akisomwa mtu anasimama na mzazi wake wanaenda kupokea zawadi, si nikasomwa Mimi nimekuwa wa kwanza kwa darasa langu mjomba akasimama kwa mbwembwe zote akacheki upande wa wanafunzi kijana hatokei wazazi wakamshambulia kwa maneno kwamba alikuwa anasema wenzake kumbe mtoto wake pia kashindikana. Aisee akajaa vibaya yule mzee akachukua zile zawadi akatulia. Kama kawaida yangu muda wa kurudi home ukafika nikarudi kama natoka shule vile sijui hata kilichoendelea wala sijui hata kama nimekuwa wa kwanza sababu hata mitihani mingine walikuwa wananichukulia watu. Nikamkuta wanakula mezani nikamsalimia murua kabisa akaniuliza vipi za shule nakamjibu safi na nimekuona kwenye kikao anasema kweli nimekuja. Akauliza umekuwa wa ngapi nikamwambia wamesoma washindi kumi tuu wengine tunapewa ripoti kesho zenye matokeo yetu akasema poa. Kesho nafika school watu wananiambia nimekuwa wa kwanza na nilisomwa sikuwepo mjomba akanichukulia zawadi aseeeeeeee kidogo nizimie kwa mteru, nikamuwaza yule jamaa atakuja anichinje mchana kweupe, nikapokea matokeo nikapeleka home nikaweka mezani mbio wiki sipo home kulalake. Akaanza kunisaka aliponitia mikononi enheee....
 
Siku ya kumaliza mtihani wangu wa darasa la 7. Nilimvizia mwalimu wahesabu alikua anaitwa Mwalim nakajumo, alikua anatoka shuleni kwenda kwake, sasa nikamfatilia nyuma nyuma huku nimeshika jiwe kama ninja. Alipofika uchochoroni nikqmpa la kichwa kisha nikachapa lapa kuelekea njia nyengine. Hata sikupoteza muda maana niliskia yowe tu "aaaaggghhhhrrr"
 
Niliiba Muhuri wa Shule nikawa naandika Barua za michango nagonga muhuri Nampelekea Mzee Father ,navuta mpunga Natia Mfukoni.

Nilikuja kukamatwa baada ya kuutumia Muhuri ktk karatasi za Kupigia kura ,Maana nilikua Nampango mkakati wa kuwaweka madarakani watu wangu,
Baazi nilifanikiwa kuwaweka madarakani, hekaheka ilikuja ktk kura za Head Boy(HP),ndiko nilipofumwa na siraha zangu za maangamizi mfukoni, kumbe kunajamaa alichora ile Raman ya Mimi kudakwa. Kibaya zaidi nikakutwa na ule muhuri ktk Bag yangu. Taarifa zikafika kwa mzee Father.
Kilichoendelea sitokuja sahau

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
Ww ulihujumu uchumi
 
Back
Top Bottom