Tukio gani la kijasiri ungependa mwenyekiti ajae wa CCM alifanye kwa manufaa ya taifa?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
1: Kuurudisha uwanja wa Kirumba Mwanza na vingine vyote serikalini. Hili dukuduku lilishika kasi nilipokutana na mtu wa makamo alivyoeleza walivyokuwa wanatolewa shule ili wakashiriki ujenzi si kwa sababu ni CCM bali kwa sababu ni wananchi, hii kazi ilipaswa kufanywa 1992 na nyerere lkn sielewi alizidiwaje.

Endelea...
 
1: kuurudisha uwanja wa Kirumba mwanza na vingine vyote serikalini. Hili dukuduku lilishika kasi nilipokutana na mtu wa makamo alivyoeleza walivyokuwa wanatolewa shule ili wakashiriki ujenzi si kwa sababu ni ccm bali kwa sababu ni wananchi, hii kazi ilipaswa kufanywa 1992 na nyerere lkn sielewi alizidiwaje.

Endelea...
Hujui kuwa kipindi hicho chama kilikuwa kimoja na kila Mtanzania alikwa CCM?
 
2. Kufuta mbio za mwenge wa uhuru. Mwenge unatumia gharama kubwa sana. Ikibidi uwe unawashwa na kukimbizwa kwenye willaya mojawapo ili wiki ya uhuru tu.
 
Watz wote wapate bima ya afya kama alivyoanzisha Rais mstafu Mkapa
 
Atoe ufafanuzi wa kivuko na nyumba za serikali hata kama alitumwa kwa nini hakujiuzuru kwa kuona ni jambo haramu kwa maslahi ya Taifa?
 
Ataifishe mali zote zinazomilikiwa na CCM ambazo zilichukuliwa kabla ya mfumo wa vyama vingi 1990s ikiwemo viwanja vya mpira kama kirumba,sokoine,mkwakwani,tabora ,majumba n.k la sivyo mapato yanayopatikana yapelekwe moja kwa moja hazina kwa manufaa ya wote.
 
Wale waliyotumbuliwa wafilisiwe Mali zao Na maigizo ya kushtukiza asiyasahau mana mi napenda sana Yale mashtukizo sijuwi imekuaje mana sasa ni kimya kabisa.
 
1: Aiunde upya Katiba Mpya ya CCM ili kubeba maudhui ya siasa safi,uongozi bora na uadirifu kwa vitendo na maneno

2:katiba Mpya ya JMT ili iwe na mapana ya falsafa yake yenye tija kwa vizazi vya sasa na baadae.

3:Afinyange Muungano Kichama kwa Manufaa ya nchi/Taifa

4:Asamehe wafanyabiashara wadogo na wa kati walioshindwa kutimiliza matakwa ya kisheria ktk masuala ya Kodi ili washiriki kikamirifu kulijenga taifa sasa kwenda mbele.

5.Awasamehe wote waliokichukia chama na kutoshiriki kikamirifu ktk kukisaidia chama sababu ya makando kando ya udhaifu,uozo uliokuwapo.

6.Atangaze msamaha kwa waliokihama chama sababu ya mihemuko ya mivutano ya kiuongozi chamani..

7.Awakaribishe wanachama wapya wenye nia ya kujiunga na hata waliotoka wenye nia ya kurudi.
 
Hujui kuwa kipindi hicho chama kilikuwa kimoja na kila Mtanzania alikwa CCM?
basi kwa hili wazo lako ikulu,bunge,airports,mashule,barabara, nhc,meli,treni zote ni mali ya ccm maana zilimilikiwa enzi ya chama kimoja.
source of income ya hizo rasilimali telekezwa ndio inahojiwa hapa. ndio maana hatujataja ukumbi mpya uliojengwa na jk. chama kimoja haimaanishi nchi nzima ilikiwa raia wote ni wanasiasa
 
Wachangiaji tofautisheni matukio ya Magufuli kama mwenyekiti wa CCM na Magufuli kama Rais wa nchi.
 
Aiweke CCM katika muundo utakaopelekea kufutika kwa vyama vya upinzani vya mfukoni. Vibaki vyama imara visivyopungua vitatu tu.

Mojawapo ya njia nzuri ya kuvinyong'onyesha vyama hivyo iwe ni kuwasamehe wanaCCM wote waliokimbilia huko wakati liCCM lilipokuwa limeoza kila kiungo.
 
waliong'oa meno tembo wetu wafilisiwe;
loliondo irudishwe iwe chini ya wazawa kama sehemu zingine nchini
 
Back
Top Bottom