Tukinyamaza, mafisadi watashinda

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Tukinyamaza, mafisadi watashinda
Mradi wa UV-CCM, kashifa tupu
Na Saed Kubenea
YUSUPH Makamba, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni mwongo, MwanaHALISI limegundua. Wiki iliyopita Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkataba kati ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mwekezaji ulikuwa haujatiwa saini...
Serikali yakosa uvumilivu
Na Ndimara Tegambwage
HATUA ya polisi kuvamia ofisi za MwanaHALISI na kupekua kompyuta kwenye chumba cha habari na nyumbani kwa mtedaji mkuu wa gazeti hilo, ni ushahidi tosha kwamba sasa serikali imekosa uvumilivu...
Hakuna vitisho vitakavyotusimamisha
Tahariri
NI jambo la kustaajabisha kwamba Polisi wamepata ujasiri wa kutumiwa ili kuvitisha vyombo vya habari. Ijumaa iliyopita Polisi walivamia na kupekua ofisi za gazeti la MwanaHALISI pamoja na nyumbani kwa Saed Kubenea, Mkurugenzi wa kampuni ya Hali Halisi Publishers (HHP) inayochapisha gazeti hili na lile la Mseto...
Kiingereza na ‘uhuru wa kujiua’
Na Rehema Kimvuli
WAZAZI wengi wa Tanzania wamekuwa wakikimbilia kupeleka watoto kusoma katika shule zilizo nje ya nchi hasa Uganda, bila kufuatilia wasifu wa ndani na nje wa shule hizo...
Mafisadi wanazidi nguvu kuishinda serikali
Na Mbasha Asenga
HALI ya mambo inavyoendelea nchini sasa juu ya mapambano dhidi ya ufisadi inatoa picha moja kubwa, kwamba serikali inakaribia kusalimu amri. Huu ni ukweli ambao hakuna kiongozi wa wa juu serikalini atakayekubali kuukiri hadharani...
Tukinyamaza, mafisadi watashinda
Na M. M. Mwanakijiji
IJUMAA wiki iliyopita Watanzania wameshuhudia jaribio dhaifu la vyombo vya serikali vya usalama kujaribu kufunga kitambaa kwenye midomo ya vyombo vya habari. Serikali imejaribu kuliziba mdomo gazeti la MwanaHalisi...Msumari wa mwisho katika 'jeneza' la Lowassa abakia na 'galasa'
Na Saed Kubenea
Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba sasa wanaelekea ukingoni kisiasa. Kitakachowaumbua na hata kusababisha wajiuzulu nyadhifa zao au waodolewe kwenye uongozi ni mgogoro unaotokota kuhusu utoaji wa mradi wa ujenzi wa kitega uchumi cha UVCCM...
Iweje Zanzibar nchi ndani ya Muungano
Na Joseph Mihangwa
WANASHERIA wakuu wa serikali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanashughulikia tafsiri sahihi ya kisheria kuhusu utata ulioibuka nchini wa kama Zanzibar ni nchi. Hii inafuatia tamko la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilotoa bungeni wakati akijibu swali...
CCM kimbilio la hata wahalifu wadogowadogo
Na Stanislaus Kirobo
“UKITAKA mambo yako yaende vyema ingia CCM,” alisema Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye kwenye mkutano wa hadhara mkoani Singida mwaka 1997...
Muungano wa paka na panya basi
UTATA wa muungano umeshaonekana. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umekuwa na utata zamani, sema tu haujaathiri matakwa ya watawala...
Uvamizi MwanHALISI, Wasomaji wanasemaje:
IJUMAA 18, mwaka huu, majira ya saa tisa jioni, makachero walivamia ofisi za kampuni ya HaliHalisi Publishers Limited (HHP) inayochapisha magazeti ya MwanaHALISI na Mseto na kupekua ofisi na nyumba ya Mkurugenzi na Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo, Saed Kubenea...
Manji anadhamira na Yanga?
KWA mwanayanga yeyote, ni lazima atakuwa anatembea kifua mbele kutambia usajili wa kufuru uliofanywa na bilionea kijana mwenye umri wa miaka 30 tu! Yusuf Manji...Na M. M. Mwanakijiji
IJUMAA wiki iliyopita Watanzania wameshuhudia jaribio dhaifu la vyombo vya serikali vya usalama kujaribu kufunga kitambaa kwenye midomo ya vyombo vya habari. Serikali imejaribu kuliziba mdomo gazeti la MwanaHalisi. Imejaribu kuifunga mikono ya uandishi ya waandishi na wahariri wa gazeti hili.

Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya KLH News International, mashabiki, wakosoaji na wapenzi wa uhuru wa vyombo vya habari nchini, kulaani kwa lugha kali inayowezekana kitendo cha vyombo vya usalama kujaribu kwenda kutafuta chanzo cha habari kwa kutumia nguvu za kijeshi wakisukumwa na mkono wa mahakama.

Kitendo hiki kilichofanyika siku ya Ijumaa hakina budi kukebehiwa, kudharauliwa. Lazima kioneshwe kuwa ni kitendo cha hatari, chenye kujenga msingi mbaya kabisa wa mahusiano kati ya vyombo vya habari na watoa habari. Tunalaani vikali na pasipo kuumauma maneno. Kitendo cha mashushu kuvamia na hatimaye kulazimisha kupatiwa vyombo au zana za kazi za waandishi ili wajue kilichomo ni hatari kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Kuna wale ambao wanaamini kuwa kitendo hiki kilikuwa ndani ya nguvu za serikali, hasa kwa vile imedaiwa kuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Saed Kubenea alikuwa na nyaraka za kibenki na amekuwa akitangaza namba za akaunti za watu na viwango vya fedha zilizomo kwenye akaunti hizo. Kwa kutumia saikolojia ya vitisho, Waziri wa Habari na Utamaduni, George Mkuchika, amehoji eti itakuwaje kama Kubenea angekuwa na akaunti za mtu wa kawaida tu!

Hofu hii haina msingi kwa sababu wangeweza kumuuliza Kubenea au kuangalia kwenye gazeti hili ni akaunti za watu gani zimekuwa zikitajwa na kuandikwa au wangefanya kile ambacho mimi nilikifanya. Jumamosi iliyopita nilipata nafasi ya kuzungumza na Kubenea, nikamuuliza swali jepesi kujua ni akaunti za watu gani ambazo zimekuwa zinaandikwa na gazeti lake. Jibu lake nililielewa, na wala sikuhitaji kuomba vyombo vya dola kwenda kutafuta jibu hilo.

Alisema wazi kuwa akaunti ambazo wanazifuatilia ni za watumishi wa umma na viongozi wa umma; na hata mara moja hawajatafuta akaunti za mtu wa kijijini au mkulima aliyeuza "mazao yake na kuweka fedha benki". Kimsingi nami nakubaliana na MwanaHALISI kuwa mambo ya viongozi si siri, na hayapaswi kuwa siri. Hivyo, akaunti zao hazipaswi kuwa siri. Utaratibu huo unakubalika sehemu nyingi duniani, kwani inaaminika kuwa ukiwa mtumishi wa umma, kuanzia chakula unachokula, wapi unalala, na nani unalala naye, si siri ya taifa!

Utaona basi kuwa ni jukumu la vyombo vya habari kutafuta habari kwa namna yoyote ile inayowahusu viongozi wa umma na kama habari hiyo inahusu maslahi ya Taifa basi vyombo hivyo vinajukumu la kuweka habari hizo hadharani. Mahakama itafanya makosa makubwa kama itakuwa inaendelea kutoa waranti kama hizi dhidi ya vyombo vya habari.

Maswali ambayo hatuna budi kuyakabili ni haya hapa: Je, habari za akaunti za viongozi wa umma ni muhimu zijulikane kwa wananchi? Je, kuna ulazima wa vyombo vya habari kutangaza fedha zilizomo kwenye akaunti hizo za watu hao ambao wamepewa dhamana ya kusimamia mabilioni ya fedha za wananchi? Lakini swali jingine muhimu ni hili: Je, vyombo vya habari vina sababu ya kutangaza akaunti za makampuni yanayofanya kazi na serikali au kwa namna yoyote ile kupokea fedha kutoka katika hazina za wananchi? Majibu kwa maswali yote hayo ni NDIYO!

Ukiwa kiongozi wa umma ambaye unasimamia mabilioni ya fedha za Watanzania au kwa namna yoyote ile unahusishwa katika mapato na matumizi ya fedha za umma basi akaunti yako na familia yako vyote ni "fair game". Haiwezekani usimamie mabilioni ya shilingi halafu wananchi wasijue wewe mwenyewe unashilingi ngapi? Kwanini?

Sasa kuna ubaya gani kuangalia akaunti za wale ambao wanasimamia idara hizo? Kama Wizara ya Miundo Mbinu inaonekana (katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali) kutumia Sh. bilioni moja vibaya au bila maelezo, na hakuna mtu anayewajibishwa kutokana na hilo na bahati nzuri chanzo fulani kinawanong’oneza waandishi habari hiyo, kuna ubaya gani kwa waandishi kufuatilia akaunti za viongozi wote wa idara hiyo? Je, wakishafanya uchunguzi na kuthibitisha hayo yote, waache kuandika kwa vile ni za wakubwa?

Kimsingi, chombo cha habari kitakachonyamaza baada ya kugundua habari kama hiyo, hakifai kuitwa chombo cha habari. Ninafahamu kuwa watawala wetu wana haraka ya kusema kuwa "Tanzania ina sheria zake na tamaduni zake, msitulee mambo ya nje." Lakini hizi wanazorejea ni sheria ambazo sote tunajua ni mbaya na za kipuuzi. Haziwasaidii wananchi bali viongozi wezi na mafisadi wenzao.

Nilipomuhoji Mkuchika alidai kuwa waandishi lazima wafuate taratibu za kupata habari badala ya kutumia njia za vichochoroni. Akasema kama watu wanataka kujua kiongozi ana mali gani na fedha kiasi gani basi waende kwa mwenyekiti wa Tume ya Maadili, wajaze fomu na kufuata taratibu zote.

Nilimwambia kuwa hata wakifanya hivyo waandishi bado wanafungwa na sheria inayowazuia kutangaza hicho wanachokiona. Yeye akasema "sheria yetu ndivyo zilivyo, hata kama mimi na wewe hatuzipendi, lazima tuzitii".

Dhamira ya mwanadamu haimlazimishi kutii sheria ovu au ya dhuluma. Waandishi wa habari hawalazimishwi kutii sheria mbaya. Ni wajibu wao kama waandishi na raia wema kuikataa na kuidharau. Hata kama sheria imepitishwa na chombo halali au ambacho kinaamini ni halali, kama ni ovu, haina maana kuwa sheria hiyo ni njema.

Sheria ya ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini ilipitishwa na chombo ambacho kiliamini kuwa ni halali, na ikaheshimika sheria hiyo kuwa ni halali. Hata hivyo, watu kadhaa si tu waliidharau sheria hiyo, bali pia walitumia nguvu zao zote - ikiwemo kuikaidi - wakaibadili sheria hiyo.

Ni kwa sababu hiyo naungana na waandishi wengine ambao wanaamini kuwa fedha, akaunti, vitabu vya fedha, na mali na amali za viongozi wetu wa umma vyote ni vitu vya hadhara, na wananchi wana haki ya kuvijua pasipo kuomba kibali kwa mtu yeyote yule.

Kama hawataki tuandike kuhusu fedha zao, na mapato yao, na kama wanataka tusiandike kuhusu fedha zao na mambo yao binafsi waamue kutoka kwenye utumishi wa umma na kuweka manyanga chini.

Lakini kabla hawajafanya hivyo wakumbuke kuwa yote waliyoyafanya wakiwa madarakani ni mali ya umma na tunaweza kuyachambua na kuyaumbua; si hayo ya kwao tu bali pia ya wanafamilia wao wa karibu.

Jukumu la kulinda habari ni la serikali na wananchi wote, na jukumu la kulinda ufisadi wa watumishi wa umma ni la mafisadi wenyewe na viongozi wanaowasimamia (mafisadi wakubwa). Wasitarajie kupata ushirikiano kutoka kwa vyombo vya habari, wakidhani vitaficha usifadi huo. Kama walifunga ndoa yao na ya unafiki na baadhi ya wachungaji, viongozi wa dini, nan wanahabari kadhaa, wasidhani sote tumo katika makundi hayo. Wale wachache walionao tayari wanawatosha.

Sisi wengine tutaendelea kuwa huru na kusimamia uhuru wetu. Wananchi wakiona uovu wasiufumbie macho. Wananchi hawaviamini vyombo vya dola katika kudhibiti ufisadi. Kimbilio lao la sasa ni nguvu ya kalamu. Na hilo ni jukumu ambalo tunalibeba kwa umakini mkubwa.

Kwa kumalizia: Akaunti ya Deep Green Finance iliyofunguliwa NBC ni . 011103024840 na kuchotewa mabilioni ya fedha zetu.

Akaunti ya Tangold nayo ni 011103024852 iliyofunguliwa NBC Corporate Branch. Ilikuwa ni akaunti hii ya Tangold ambako fedha zilitoka na kupelekwa kwenye akaunti ya Meremeta ambayo tuliambiwa imefilisiwa na ambayo akaunti yake bado ni inafanya kazi. Hiyo Meremeta haijulikani ni kampuni ya nani katika taifa la mashushusu wanaojiona mahiri kwa kuzishambulia ofisi za MwanaHALISI.

Huku wakishindwa kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wakuu wa ufisadi uliokithiri waliotajwa na Dk. Wilbroard Slaa pale Mwembe Yanga, Bar es Salaam, tangu Septemba 15 mwaka jana (2007).

Mashushushu wetu wanajidhalilisha wanapowaacha hao na kumsumbua Kubenea na wafanyakazi wa MwanaHALISI. Hizi ni dalili kwamba mafisadi wameanza kuanguka. Na wanadhani atakayesaidia kuwaokoa ni polisi! Ujumbe wa leo ni huu: Hatunyamazi, maana tukinyamaza tu, tutawapa ushindi mafisadi. Hatutaki.

mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Mafisadi tayali wameshashinda au kuna mpya yoyote inayohatalisha ulaji wao naona mambo yamekwisha na wanatanua mitaani tena kwa mbwembwe nyingi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.
Maanu hakuna wala husikii Chenge wa Chungu ,mambo ni poa tu.
 
Mafisadi tayali wameshashinda au kuna mpya yoyote inayohatalisha ulaji wao naona mambo yamekwisha na wanatanua mitaani tena kwa mbwembwe nyingi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.
Maanu hakuna chenge wa chungu ,mambo ni poa tu.
Wahalifu wote waliowahi kutawala walitanua wakidhani hakuna siku yao. Lakini mwisho wao haukuwa mzuri. Na mara nyingine hata vizazi vyao havijawahi kufaidi wizi huo.
Sasa si unasikia hata vijana wetu wameanza kukasirika na kujua viongozi wetu ni mafisadi? si umesoma zile jumbe zao katika maandamano yao?
Ohhhhhhh mafisadi wana hali ngumu siku zijazo.
 
Wahalifu wote waliowahi kutawala walitanua wakidhani hakuna siku yao. Lakini mwisho wao haukuwa mzuri. Na mara nyingine hata vizazi vyao havijawahi kufaidi wizi huo.
Sasa si unasikia hata vijana wetu wameanza kukasirika na kujua viongozi wetu ni mafisadi? si umesoma zile jumbe zao katika maandamano yao?
Ohhhhhhh mafisadi wana hali ngumu siku zijazo.
hakuna kitu chochote,labda kama ingekuwa pemba naamini wangelikwisha funga virago na kukaa tayari kurudi vijijini.
Ila upande wa Tanzania Bara jamaa akiweka debe la tindi kali zile nyepesi nyepesi na kumwaga kofia na fulana mbele zimeandikwa uhuru na umoja na akina dada nao wakiachiwa upande wa kanga zimeandikwa Si mie,basi kura zote zinaelekezwa huko tena inakuwa hawaoni wala hawasikii kama wamelogwa.Kule zenji kuna sera ya wapiga kura ambayo huku bara haijafika ,kule jamaa siku hizi hawatoi tena vitu kama hivyo maana watu wanavichukua na kama ni feza wanaila na kura hawakupi ni kiboko kibaya sana ambacho wananchi wanafaa waelimishwe ili wakitumie.
 
Back
Top Bottom