Uchaguzi 2020 Tukimkata watasema tumemuogopa na tukimuacha atatusumbua: Ndio mtihani walio nao NEC kwa sasa kuhusu Tundu Lissu

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,548
6,102
Huu ndio mtihani walio nao NEC kwa sasa kuhusu Tundu Lissu wanashindwa wamfanye nini mtu huyu ambaye ameshaonekana ni mwiba mchungu sana kwenye kampeni za mwaka huu

Ushauri wangu kwa NEC muacheni Tundu Lissu agombee kwani kwa kumkata kama watu wanavyofikiria sio njia ya kupunguza makali yake kwa namna yoyote ile

NEC acheni mwaka huu tuone hoja zikijibiwa kwa hoja kisha wananchi tutoe maamuzi yetu mwezi Oktoba. Naamini mtafanya hivyo

Tukutane Oktoba.
 
Yaaani hii inanikumbusha Walimu wa Dini walivyomfuata Yesu kumjaribu kwa swali Eti kama yeye ni masihi au vipi?

Yesu aliwajibu kwa swali. ”Mamlaka ya Yohana mbatizaji kubatiza yalitoka kwa Mungu au Binadamu?

Jamaa walienda pembeni wakanong’onezana- Tukisema yalitoka kwa Mungu atatuuliza, sasa Mbona basi hamkusadiki? Na tukisema yanatoka kwa Wanadamu watu wote watarusha mawe maana wote hapa wanaamini Yohana Mbatizaji ni nabii!

Mwaka huu, CCM wana hali ngumu mbele ya watanzania kama Mafarisayo na walimu wa Dini walivyokuwa na hali mbaya mbele ya Yesu Kristo!!! Hawajui wafanye nini!

Mungu aendelee kumbariki na kumlinda Tundu Antipas Lissu!
 
Back
Top Bottom