Tukimbilie wapi na serikali hii?


L

Lawson

Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
70
Likes
1
Points
0
L

Lawson

Member
Joined Sep 25, 2007
70 1 0
JAMANI TUKIMBILIE WAPI NA SERIKALI YETU?

Nimambo mengi tumekuwa tukiyasikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya serikali yetu,mengi yametukatisha tamaa na wengine tunashindwa tutoe mchango gani kulinusulu taifa letu dhidi ya mafisadi tunaowaita eti viongozi
Nikiandika makala hii inanikumbusha story nilizikuwa nasoma kwenye vitabu vya muandishi Ngugi wa Thiongo hasa kitabu cha Things Fall apart wakenya walipo amua kutumia maneno kama othe government has betrayed us we fought for uhuru but whom do you see riding in beautiful cars?
Hali hii inaufanano kabisa na maisha yetu ya sasa ya watanzania zaidi ya yote viongozi wanadiliki kutwambia eti maisha bora kwa kila mtanzania, swali linakuja whom do you see riding beautiful cars and leaving in beautiful houses? watanzania sisi au viongozi wetu.Hakika haya ni maisha bora kwa kila kiongozi.
Nimeumizwa sana na vitendo vya bahadhi ya viongozi wa chama tawala wanavyotufanyia sisi wananchi hasa swala zima la kutetea maslahi yao na wala sio masilahi ya wananchi tuliowatuma bungeni.aWbunge wa chama tawala mna haki kabisa ya kufanya hivyo kwani hamkuingia bungeni kwa kupendwa na wananchi bali kwa dau lenu(hela) kama aliyekuwa katibu wenu miaka kumi iliyopita alivyosema mda sio mrefu mtafikia ku-bid. Mfano mzuri ni hule wa kugombea NEK mkoa wa Arusha.
Tamko la Mzee kinguge ngombali Mwiru ni mfano halisi wa viongozi wa sasa tulio nao, sikutengemea mzee kama huyu aliyekuwepo kipindi cha mwl. Nyerere akisikiliza nasaha zake akajichotea fadhila kutoka kwa baba yetu kipenzi mwl. ndiye angeweza kutoa tamko kama alilosema kuwa “CCM hamna rushwa bali wapinzani wameishiwa sera” viongozi wa vyama vya siasa naomba mjitahidi kuwafunua wanao hujumu nchi yetu, nafikiri wao ndio wamekosa sera. nahisi huo ndio ungekuwa mwanzo mzuri wa kuwapata wabadhlifu wa fedha yetu kwa kupitia ushahidi ulio wekwa wazi na vyama vya upinzani. Kitendo cha Kingunge kusema hamna rushwa CCM ina maana wale wabunge wa Arusha ni TLP,au CUF au ni CHADEMA? twamebi mzee maana unasema hamna rushwa kwenye CCM.we kama alivyosema Mzee rashidi kawawa mgewakarisha vijana na kuwaonya ila inaelekea wewe ndio unawatetea au si watanzania tukueleweje?Unastaili fadhila zaidi ya siasa wanchi tunawategemea wazee wa umri wenu muwaasi wala rushwa wenu.
Hutujasahau mikataba feki mnayo saini mfano mzuri karamagi,licha ya kelele nyingi kupigwa eti rais amekaa kimya jamani hivi serikali yetu tumewakosea nini wananchi?nilishangaa hotuba ya mwisho wa mwezi ya raisi wananchi tulifikiri atatoa tamko juu ya mikataba feki lakini hakuongelea chochote tukabaki kimya huku tukishuhudia akiwatembelea hao vibaraka kule Geita nakula nao sahani moja.
Ndugu wana ccm viongozi hasa mnaojiita wabunge msisahau mungu wa siku hizi si kama zamani mnalipwa hapa hapa duniani kwa matendo yenu tutawasoma kwenye habari na zaidi kuona maendeleo ya afya zenu muhimbili kama msipojilekebisha mtatoka madarakani viwete, mungu hatamlipa mmoja wenu kadli ya matendo yenu msisahau hata maandiko matakatifu yanasemavyo, lolote mtakalo tenda mmoja wenu mnanitenda mimi, pia mnayotufanyia nmamfanyia mungu pia atawahadhibu mmoja baada ya mwingine
 
K

Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,143
Likes
506
Points
180
K

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,143 506 180
preach preach brother...ni kweli tupu unayosema,dawa ni kuendelea kuibua uchafu wao na kuwapiga chini uchaguzi ujao then wataturudishia mali zetu walizoiba
 
Kisura

Kisura

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2007
Messages
364
Likes
13
Points
35
Kisura

Kisura

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2007
364 13 35
Mabadiliko hayawezi kuja kwa sisi kuongea na kufichua ubaradhuli wa viongozi, that model has failed. Tunahitaji kiongozi atayekuja kutuongoza na Machiavelli style. That is it!
 
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2007
Messages
11,391
Likes
3,141
Points
280
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2007
11,391 3,141 280
Ndugu Lawson, pongezi kwa maoni yako, lakini kitabu cha 'Things Fall Apart' kimeandikwa na mwandishi Chinua Achebe tokea nchini Nigeria, sio Ngugi wa Thiong'o wa Kenya. Naona maudhui ya makala yako yanaendana sana na kitabu kingine cha Achebe kiitwacho 'A Man of the People', kinachomuelezea kijana jasiri Odili Samalu alivyopambana na washika dola na wenye pesa chafu waliokuwa wameichafua nchi kwa rushwa wakiongozwa na Chifu Nanga.
Kama umesoma kitabu hiki, basi matukio yanayotokea Tanzania kwa sasa yanarandana kwa kiasi kikubwa kabisa.
Kitabu cha Ngugi chenye maudhui kama hayo pia kinaitwa 'Petals of Blood'. Kinasimulia visa vya Kimeria wa Kamia, Chui na Mzigo walivyonyang'anya ardhi ya wananchi kwa kutumia 'sirikali' na pesa chafu na kuwafukuzia mbali wananchi wa maeneo hayo bila fidia.
 
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
2,481
Likes
28
Points
135
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
2,481 28 135
No way out. Huwezi kukimbia kitu kimoja cha kujiuliza unafikiri ni kwa nini kule Nigeria kwenye mafuta kwa nini wazawa wameamua kuwateka wafanyakazi wa kwenye machimbo ya mafuta? Hawapendi kuishi? Maisha yao hayana faida? Kwa nini Palestina wanapigana hadi leo?

Mifano ipo mingi na hali ambayo inatokea nchi nyingine itatokea Tanzania soon rather than later, huwezi kuona maisha ya WTZ wenzako yanakuwa katika hali ngumu wakati wabunge na viongozi wachache wa CCM na serikali wanajichukulia mali kama vile haina wenyewe. Utajiri wa TZ ni mkubwa kiasi kuwa viongozi wamejisahau na kufikiria uongozi ni kujitajirisha.

Uongozi ni kutumikia raia wa nchi yako na kujitolea kwa hali na mali wakati wote kuwatumikia walipa kodi na walalahoi waliokupa dhamana ya kuwaongoza.
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
73
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 73 145
An enemy of the people.

Naomba muweze japo kukisoma ili kuona maudhui yaliyopo ni sawa na hapa bongo.
 
Nyangumi

Nyangumi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2007
Messages
508
Likes
1
Points
0
Nyangumi

Nyangumi

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2007
508 1 0
Suala sio kukimbia ni kuikimbiza serikali. Tangu lini baba mwenye nyumba akamkimbia mfanyakazi wake!!
 
mpenda pombe

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
1,261
Likes
441
Points
180
mpenda pombe

mpenda pombe

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
1,261 441 180
JPM kakomesha yote hayo.

Hapa kazi tu
 

Forum statistics

Threads 1,238,662
Members 476,083
Posts 29,325,912