Tukimaliza uhakiki wa Vyeti na Umri sasa tutaingia Uhakiki wa Wazazi, Rangi.Baada ya hapo Mishara itapanda

Ha ha ha ha ha ha Nimecheka sanaaa....

Ila tabia ya ubaguzi huwa haiishii njiani.
Baba wa Taifa alituonya akasema mtu akiianza ni sawa na kula nyama ya Mtu, itaenda mbeeele sana.
 
Mkuu watahakiki pia na jinsia. Kuna watu wana jinsia mbili hivyo lazima kuhakiki ili kujiridhisha kuwa utendaji wao unaendana na upande ulio na nguvu zaidi (dominant). Si kuna mkimbiaji mmoja wa sausi (south africa) naye aliwahi kupigiwa kelele za namna hiyo?
 
Leo nimesikiliza clip moja ikizungumzia msimamo wa Nyerere. Alicho sisitiza ni kutoogopa kukosoa viongozi wetu

Yeye Nyerere alikuwa hataki kukosolewa na waliemkosoa aliwafukuza Nchini na wengine kuwafunga Maisha kwa uhaini
 
Kama watanzania humjui mnaongozwa na washamba na wapumbavu ndiyo hao sasa. Huyu mkuchika mwenyewe limezeeka mpaka basi bado linakula nguvu za wanyonge nyambufuuu
 
Waje wakague na vikojoleo kama zinafanya kazi. Tushawacha na maigizo yenu
 
Jambo la Msingi na la Sekondari.

Ni kuachisha kazi watumishi wote wa umma na kuanza kuajiri upya,
Katika uajiri huo kuwe na Fomu ya kujaza yenye vipengele vyote vyote vinavyohitajika, kuanzia Nafasi ya kazi, hitaji la elimu, tarehe zote, picha, vyeti, nk. yaani kilakitukilakitu kinachohitajika cha msisitizo.
Hapo Serikali itarahisisha zoezi la udhibiti wa udanganyifu wote na kuwapa wafanyakazi wa umma maslahi yao kwa wakati muafaka.
Mfanyakazi jukumu lake ni kufanya kazi alizoainishiwa kwa juhudi na maarifa kwa mujibu wa sheria za kazi.
Mwajiri naye jukumu lake ni kumlipa mwajiriwa haki zake zote kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kazi.
Kila mtu atimize wajibu wake kwa wakati.
Haki inayocheleweshwa ni sawa na haki iliyonyimwa, kwani kuna wafanyakazi hukumbwa na mauti au kuacha kazi kwa hiari huku wakiwa wamekosa haki ya malipo iliyocheleweshwa.

Kama mtu ana cheti halali ni bora sana aanze mkakati wa kujiajiri, kuliko kukesha usiku kufikiria malipo yanayocheleweshwa kwa kisingizio kisichokuwepo katika sheria za kazi au barua ya mkataba wa kazi.

Tumsifu Yesu Kristo.
 
Kama mnasubiri Huruma ya mtu mmoja kuwapa haki zenu za msingi basi hapo mnajidanganya kweupe.

Fanyanyi maamuzi mapema achani njaa za kioga najua hata vyama vyenu kama vile TUGHE, TUICO, CHAMA CHA WALIMU TZ, n.k havina uwezo wa kuanzisha solidarity Forever kudai haki zenu kwasababu viongozi wenu wote waoga tena wengine ni makada ya CCM.

Amini usiamini baada ya uhakiki ya umri serikali itakuja na drama nyingine kwasababu inawajua udhaifu wenu na mwisho kabisa mtabaki kulalamika tu bila kuchukua hatua dhidi ya serikali hii onevu, wenzenu wakina mkuchika wanakula mema ya nchi kwa kufuata bendera.
 
Back
Top Bottom