Tukimaliza uhakiki wa Vyeti na Umri sasa tutaingia Uhakiki wa Wazazi, Rangi.Baada ya hapo Mishara itapanda

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Serikali imeendelea na zoezi la uhakikia na sasa kuhamia uhakiki wa Umri. zoezi hili linaweza chukua muda kiasi pengine mwaka au miaka miwili. sijui itategemeana na Kasi ya waendeshaji wa zoezi hili.

Baada ya kumaliza zoezi hili sasa kuna uwezekano mkubwa sana wa kuanza kuhakiki hata wazazi. unajua ilitangazwa asilimia 40 ya baba za watanzania si baba halisi? unafaham hilo?so serikali itataka kujua je wewe unaiyeitwa Masumbuko Matupu ni kweli ni mtoto wa Mzee Matupu au ni mtoto wa Mwanaume mmoja huko mdandiaji. huu utakuwa uhakiki muhimu sana. maana isije ikawa serikali inakulipa pesa ambazo unatumia kumnufaisha mzee Matupu wakai baba yako halisi Mzee Kidumu anateseka kwa njaa na kubaki akilalamikia serikali.

Mambo haya yanasaidia sana kuinua uchumi wa nchi hii na kupunguza serikali kuwalipa watoto hewa. ndiyo hawa wanakuwa ni watoto hewa. maana wazazi walio nao kwa maana ya kuwa baba zao si halisi.

Lakini si hivyo tu njia hii itasaidia kugundua wazazi hewa. unakuta kumbe baba yako halisi ni waziri au mbunge flan au pengine mfanyabiashara,mfanyakazi mwenye uwezo. lakini ikatokea ubaba amepewa Mzee Koroboi ambaye amejichokea.... unasababisha serikali ikusomeshe kwa mkopo wakati babayo halisi ana uwezo mkubwa tu.. unaweza kukuta kumbe ndo mmiliki wa maviwanda makubwa makubwa hapa nchini... so ingejulikana tayari serikali ingekuwa imeokoa mabilion ya pesa ambayo ingetumika kwako.

Zoezi hilo likiisha kutakuwa na ukaguzi wa rangi halisi za wafanyakazi. je wewe ni mweupe wa asili? au unajichubua? maana serikali inakulipa pesa wewe unaenda kununua madawa.. watoto wako wanakosa huduma bora au ada za shule.unalazimisha serikali ikawasomeshe kwa sababu elimu bure. kumbe usingenunua mikorogo,cream na lotion hizo ungeweka ile pesa ungeenda msomesha mtoto wako private schools.

Zoezi litaendelea mpaka tukija kumaliza kimo,uzito na makabila tutakuwa tumesave pesa nyingi sana ambazo zilikuwa zinapotea pasipo sababu za msingi. na hivyo kuinua uchumi kwa kiasi kikubwa na kuziba mirija ya ufisadi kabisa.

Huko tunakoenda inawezekana kabisa tukawa hatuna hewa yoyote ile. yaani tukawa tuna hewa hewa. hivyo watu wakawa wanajifia tu kwa ukosefu wa hewa. tunataka nchi inyooke,ukiitizama ramani ya tanzania unashangaa huyu mchoraji alikosa kweli rula? kwan nin amepindisha pindisha hivyo? nchi itanyooka na tutakata hewa yoote.

Wapinzani wataisoma namba.... watajuta kuzaliwa kwa maisha yatakavyokuwa magumu kwao. sisi wa chama hiki maisha yetu ni mazuri tu sababu tunanuaa vitu kwenye masoko yetu maalumu. zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Serikali imeendelea na zoezi la uhakikia na sasa kuhamia uhakiki wa Umri. zoezi hili linaweza chukua muda kiasi pengine mwaka au miaka miwili. sijui itategemeana na Kasi ya waendeshaji wa zoezi hili.

baada ya kumaliza zoezi hili sasa kuna uwezekano mkubwa sana wa kuanza kuhakiki hata wazazi. unajua ilitangazwa asilimia 40 ya baba za watanzania si baba halisi? unafaham hilo?so serikali itataka kujua je wewe unaiyeitwa Masumbuko Matupu ni kweli ni mtoto wa Mzee Matupu au ni mtoto wa Mwanaume mmoja huko mdandiaji. huu utakuwa uhakiki muhimu sana. maana isije ikawa serikali inakulipa pesa ambazo unatumia kumnufaisha mzee Matupu wakai baba yako halisi Mzee Kidumu anateseka kwa njaa na kubaki akilalamikia serikali.

mambo haya yanasaidia sana kuinua uchumi wa nchi hii na kupunguza serikali kuwalipa watoto hewa. ndiyo hawa wanakuwa ni watoto hewa. maana wazazi walio nao kwa maana ya kuwa baba zao si halisi.

lakini si hivyo tu njia hii itasaidia kugundua wazazi hewa. unakuta kumbe baba yako halisi ni waziri au mbunge flan au pengine mfanyabiashara,mfanyakazi mwenye uwezo. lakini ikatokea ubaba amepewa Mzee Koroboi ambaye amejichokea.... unasababisha serikali ikusomeshe kwa mkopo wakati babayo halisi ana uwezo mkubwa tu.. unaweza kukuta kumbe ndo mmiliki wa maviwanda makubwa makubwa hapa nchini... so ingejulikana tayari serikali ingekuwa imeokoa mabilion ya pesa ambayo ingetumika kwako.

zoezi hilo likiisha kutakuwa na ukaguzi wa rangi halisi za wafanyakazi. je wewe ni mweupe wa asili? au unajichubua? maana serikali inakulipa pesa wewe unaenda kununua madawa.. watoto wako wanakosa huduma bora au ada za shule.unalazimisha serikali ikawasomeshe kwa sababu elimu bure. kumbe usingenunua mikorogo,cream na lotion hizo ungeweka ile pesa ungeenda msomesha mtoto wako private schools.

zoezi litaendelea mpaka tukija kumaliza kimo,uzito na makabila tutakuwa tumesave pesa nyingi sana ambazo zilikuwa zinapotea pasipo sababu za msingi. na hivyo kuinua uchumi kwa kiasi kikubwa na kuziba mirija ya ufisadi kabisa.

huko tunakoenda inawezekana kabisa tukawa hatuna hewa yoyote ile. yaani tukawa tuna hewa hewa. hivyo watu wakawa wanajifia tu kwa ukosefu wa hewa. tunataka nchi inyooke,ukiitizama ramani ya tanzania unashangaa huyu mchoraji alikosa kweli rula? kwan nin amepindisha pindisha hivyo? nchi itanyooka na tutakata hewa yoote.

wapinzani wataisoma namba.... watajuta kuzaliwa kwa maisha yatakavyokuwa magumu kwao. sisi wa chama hiki maisha yetu ni mazuri tu sababu tunanuaa vitu kwenye masoko yetu maalumu. zidumu fikra za mwenyekiti.

Hongera zenu kwa kunufaika na utawala wa kidunia
 
Leo nimesikiliza clip moja ikizungumzia msimamo wa Nyerere. Alicho sisitiza ni kutoogopa kukosoa viongozi wetu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata kampuni inayoelekea kifilisika hupunguza wafanyakazi wake..hili nalo liko wazi kabisa kwa serikali hii..pumzi zimekata wanashindwa kuweka wazi tu..
 
Kweli ujinga ni ufahari kwa maamuzi yasiyo na tija kwa uimara wa Taifa letu hivyo wazee hawaitajiki ama vijana? Mbona Mkuchika umri ule au ndio wananchi tufanye ukaguzi kwa wabunge wetu kama wamepatikana kihalali?
 
Umesahau mkuu GuDume, tutakwenda kuhakiki wazazi na kama wametangulia mbele za haki basi utatakiwa kutoa death certificates kutoka serikarini maana kuonyesha kaburi halitambuliki!
 
Baada ya hakiki zote kwisha, zitafuata hakiki za uraia/utaifa na hasa kwenye mikoa ile 8 inayopakana na nchi jirani. Sina hakika kama kuna watu watabaki zaidi ya ile mihimili mitatu ya nchi ambao wameshika mpini,milima mabonde na maziwa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom