Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Hakika sote tumeumia kama taifa, kwa kupoteza wanetu wapendwa!
Poleni ndugu zangu!
Mungu wetu utupe faraja za rohoni zile ambazo hakuna mwanadamu awezae kuzitoa.
Pamoja na haya; Mfalme Suleimani anasema kwamba, siku ya mema ufurahi lakini siku ya mabaya ufikiri.
Nimewaza sana kuhusu hii ajali ya vijana wadogo hawa.
Hivyo basi mara baada ya msiba huu kuna mambo yanapaswa kubadirika au tuseme kubadirishwa ndani ya jamii yetu.
1) Kuhusu safari za jumla kwa taasisi zetu za elimu.
Nadhani iko haja kabla ya safari kuwe na kibali maalumu toka katika mamlaka husika.
Kibali hiki kitolewe mara baada ya kukamilisha mambo yafuatayo.
a) ukaguzi wa vyombo vya usafiri vitakavyohusika.
b) ukaguzi kwa dereva atakaeendesha chombo.
c) Hata hivyo Safari hiyo ianzie polisi.
2) Ukaguzi wa magari ya mashule yote yanayowachukuwa wanafunzi wakati wa kwenda na kurudi mashuleni.
Maana magari haya mengi huwa ni mabovu sana.
3) Wazazi wawe wanashirikishwa wakati wote wa uwepo wa safari ili wajiridhishe namna watoto wao wanavyosafirishwa.
Sio ikitokea ajari ndio wanataarifiwa!
Karibuni tuliweke hili sawa.