Tukikamilisha miradi ya Stiegler's Gorge na SGR pekee. Ona habari hii na fanya hesabu kuhusu sisi kuendelea kukopesheka na utathimini tunaelekea wapi

wakuu huu mradi stiegler's gorge navyojuua mimi ina cost trillion 3 sasa hii mara trillion 6.5 mara 11 trillion ipo vip wakuu mwenye maelezo ya ziada naomba anifadanulie kidogo
 
Mkuu kiuhalisia gazeti la mwananchi na citizen NI magazeti ya Kenya ambao ni wapinzani wetu kiuchumi ambao hawaitakii Tanzania mema.
Wao wanajua ya kuwa usitawi wa Tanzania ni kifo Cha Kenya kiuchumi.
Watafanya watakavyofanya ili kutuvuruga Watanzania
Kenya wana SGR.mpya walijenga kwa ajili ya soko la Africa mashariki.
Tanzania tunajenga SGR kwa ajili ya soko Africa mashariki,kwa hesabu ndogo tu Kenya unadhani wanafurahi?
Ukizingatia kwamba Tanzania kwenda Uganda,Rwanda,Burundi na DRC ni karibu kuliko Mombasa Kenya?
Tukiwa Wazalendo wa kweli,Tanzania itakuwa giant kiuchumi in the next twenty years kwa ukanda was Africa Mashariki,Wakenya wanalijua hilo,unafikiri wanafurahi?
TAFAKARI
Yaani Aga Khan amekuwa mkenya tena jamani
 
wakuu huu mradi stiegler's gorge navyojuua mimi ina cost trillion 3 sasa hii mara trillion 6.5 mara 11 trillion ipo vip wakuu mwenye maelezo ya ziada naomba anifadanulie kidogo
Ukiona hivyo ujue kuna upigaji na ndio maana kila siku wanakuja na figure mpya.
 
Yaani hao wachambuzi ni vichekesho kweli. Wameiangalia hii miradi kama tunachonga kinyago cha panya ili tuwe na fahari ya kukitazama. Hawasemu kuhusu hiyo miradi namna itakavyochochea uchumi na kupunguza gharama za ufanyaji biashara na uzalishaji viwandani hivyo kukuza pato la taifa

Ha ha ha haaaaa!
Umenikumbusha kile kibonzo cha jamaa anafikiria namna ya kuziweka kwenye akaunti yake ya benki mapesa mengi anayowaza kichwani mwake!
 
Tazara on tanzania side, aas the easiest easiest, kwa sababu inapita maeneo ambayo ni grain and food baskets ya nchi hii , lakini wafanyabiashsra wote wanaona heri watumie malori, na kadhaa zote kuliko kutumia tazara, hata kwa vitu kama mbao au mahindi, tumeshindwa tumeshindwa, leo subir SGR , utacheka hapo itakaposhindwa na vi fuso
Mkuu Tazara iko hoi sana na kwa kweli inasikitisha maana ile ni mult billion project ambayo ilikuwa msaada mkubwa sana, china amejitahidi mnooooo kuisaidia serikali lakaini haibebeki sometime Tazara inakosa hata mafuta ya kuendeshea train!!!!! na serikali wala haijali am sure hata hii SGR kama serikali isipojipanga sustainability yake itakuwa kaa la moto huko mbele.
 
Nina wasiwasi na mradi wa stiglers gorge kama wazungu wakiukataa kamwe wamisri hawatajenga kwa kuwa misri ni ally(soma stooge) wa marekani litakaloamuliwa washington huwa limetimizwa cairo,riyadh,tel aviv ni hayo tu
 
Kama hesabu yangu iko sahihi, naona ni kama tutakuwa tumebakiza trilioni moja tu kabla ya kufikia ukomo wa kukopa iwapo tutaenda hivi tunavyoenda(tutaamua kuikamilisha yote) unless tunajitaahidI kulipa haya madeni na hii miradi tukaendanayo taratibu(kwa hatua) hasa huo wa SGR.
Kuilipa kwa kasi kwa sasa ni ndoto, miradi haijakamilika na hata ikikamilika itakuwa haizalishi kiasi cha fedha chakutosha kujilipa.
 
Nchii hii bora ipigwe bomu LA nuclear tu tuanze upya.
Si utakuwa marehemu wakati huo. Hasira za mkizi hizi, tena umerishwa matango pori na kigazeti chenye affiliation na Kenya ambaye ni mshindani kwa kila nyanja.
 
Ha ha ha haaaaa!
Umenikumbusha kile kibonzo cha jamaa anafikiria namna ya kuziweka kwenye akaunti yake ya benki mapesa mengi anayowaza kichwani mwake!
Hiyo miradi italeta Pesa kedekede. Nafikiri Tanzania itajisajiri Paris club kama donner country. Hatutashindwa kuwasaidia vinchi kama Fiji, Timor hata Lethotho
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom