Tukikamilisha miradi ya Stiegler's Gorge na SGR pekee. Ona habari hii na fanya hesabu kuhusu sisi kuendelea kukopesheka na utathimini tunaelekea wapi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Jumatano iliyopita, Kampuni ya Arab Contractors ya Misri na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), walisaini mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme kwenye Mto Rufiji, maarufu kama Stiegler’s Gorge. Utilianaji huo wa saini ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, walikuwa mashuhuda wa utilianaji huo wa saini. Kukamilika kwa Stiegler’s Gorge kutaifanya Tanzania kuwa na umeme mkubwa, wenye kutosheleza nchi na zaidi tena kwa bei nafuu.

Mradi wa Kinyerezi ulipokamilika mwaka juzi, taarifa ya Tanesco ilieleza kuwa mahitaji ya umeme yalitimia kwa asimilia 100. Ilielezwa kwamba Kinyerezi inazalisha megawati 150, hivyo kufikisha megawati 1,500 ambazo ndizo mahitaji ya nchi kwa sasa.

Hata hivyo, hali halisi ya umeme kwa sasa, jinsi umeme unavyokatika mara kwa mara, huku nishati hiyo ikionekana kuwa si ya uhakika, ni dhahiri kuwa kiwango cha umeme kilichopo hakitoshelezi. Ama uwezo wa mitambo ya ufuaji ni mdogo au njia za upitishaji wa umeme zimezidiwa.

Stiegler’s Gorge ikikamilika, itaweza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 2,100. Kwa hesabu ya Tanesco mwaka juzi kuwa mahitaji ya nchi ni megawatt 1,500, maana yake, mradi huo ukikamilika, itawezekana hata kuzima mitambo mingine yote na kutumia umeme wa Stiegler’s Gorge na mwingine utabaki.

Mantiki hapo ni kwamba nchi itakuwa na umeme mwingi wa ziada. Itaweza kuuza hata nje umeme mwingine. Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), unaendelea awamu ya kwanza kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro. Matarajio ni kupitisha treni za umeme. Stiegler’s Gorge inaielekeza nchi kwenye umeme unaokidhi mahitaji.

Tuuhoji uhakika

Pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake njema pamoja na uthubutu wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme mwingi na wa bei nafuu, ukizingatia kuwa Stiegler’s Gorge ni mradi ambao upo kwenye mipango ya Serikali tangu miongo minne iliyopita.

Novemba mwaka jana, wakati Bunge lilipokuwa kwenye mjadala wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017-2018, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye aliikosoa Serikali kwa uamuzi wake wa kutoishirikisha sekta binafsi katika miradi inayoweza kujiendesha kibiashara.

Alikosoa utaratibu wa Serikali kujenga miradi mikubwa kwa fedha za ndani, wakati kiuhalisia inakopa na kuipa nchi mzigo mkubwa wa madeni. Nape alisema, kuishirikisha sekta binafsi kuna nafuu kubwa kuliko kuendelea kukopa, kitu ambacho alionya kwamba kitakuja kusababisha athari kubwa kwa nchi.

Jambo la kwanza Nape alisema kuwa Serikali inakopa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mikubwa ambayo ukamilikaji wake unachukua muda mrefu, wakati mikopo husika marejesho yake yanafanyika ndani ya muda mfupi. Kutokana na hali hiyo, alitahadharisha kwamba marejesho yataathiri miradi mingine.

Nape alisema kwa vile miradi itachelewa kukamilika, wakati wa marejesho ya mikopo, itabidi kuchukua fedha kwenye miradi ya huduma kama elimu, afya na kadhalika ili kuwalipa wadeni wa nchi. Katika hili Nape alisema anatilia shaka uzalendo wa wachumi ambao wanamshauri Rais Magufuli.

Tahadhari ya Nape

Upande wa pili, Nape alionya kuwa nchi inapiga hatua kwenda kuwa isiyokopesheka ikiwa itakopa kwa ajili ya miradi miwili tu; wa kwanza ni ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) dola 15 bilioni (Sh33.8 trilioni) na wa ufuaji umeme wa Stiegler’s Gorge megawati 2,100 dola 5 bilioni (Sh11.27 trilioni), jumla dola 20 bilioni (Sh45 trilioni).

Nape alisema taarifa za mpango zinaeleza Deni la Taifa lilifikia dola 26 bilioni (Sh58.6 bilioni) sawa na asilimia 32 ya uhimilivu wa deni. Kwamba ili Tanzania ifikie kikomo cha kukopeshwa, deni lake linapaswa kufikia dola 45 bilioni (Sh101.4 trilioni).

Kutokana na hoja hiyo ya Nape, endapo Serikali itaongeza mkopo kwa miradi miwili tu ya Standard Gauge na Stiegler’s Gorge, deni lingefikia dola 46 bilioni (Sh103.7 trilioni), yaani ongezeko la Sh2.3 trilioni kutoka kwenye kiwango chake cha mwisho cha kukopa.

Hata hivyo, hesabu ya Nape kuwa Stiegler’s Gorge ingegharimu Shi11 Trilioni haipo sawa, kwani wakati wa utiliaji saini kati ya Tanesco na Arab Contractors, Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, alisema kuwa mradi gharama yake jumla ni Sh8 Trilioni.

Nape pia alikosoa kutelekezwa kwa mradi wa gesi ambao uligharimu maisha ya watu kuhamishwa makazi. Mipango ya awali ilikuwa nchi ije kuwa umeme wa gesi. Hata hivyo, Rais Magufuli mwaka huu alizungumzia sababu ya kupuuza mradi wa gesi, kwamba ulishaandaliwa mazingira ya kifisadi.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amekuwa akipigia kelele mkataba wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge, kuwa unaminya fursa zilizopo nchi. Nchi ina chuma, makaa ya mawe na kila kitu chenye kutumika kujenga reli, lakini mkataba uliopo unafanya Waturuki waliopewa zabuni watoe malighafi nje ya nchi, badala ya kuwabana kutumia zilizopo nchini.

Wadau wa mazingira wanadai Stiegler’s Gorge ni hatari kwa mazingira, lakini wanapuuzwa. Haya ndiyo mambo ya kutazama kipindi hiki furaha ikiwa imetanda. Je, kila kitu kinakwenda safi au upo wakati majuto yataibuka. Hoja za akina Nape na Zitto hazina maana au utafika wakati itakuwa majuto mjukuu? Watu wa mazingira je? Vema kusikiliza hoja za kila upande, kwani hiyo ndiyo mantiki ya kujenga nchi moja.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama hesabu yangu iko sahihi, naona ni kama tutakuwa tumebakiza trilioni moja tu kabla ya kufikia ukomo wa kukopa iwapo tutaenda hivi tunavyoenda(tutaamua kuikamilisha yote) unless tunajitaahidI kulipa haya madeni na hii miradi tukaendanayo taratibu(kwa hatua) hasa huo wa SGR.
 
Viumeme vyenyewe unavyotupigia mayowe humu ni MB tu, mgefikisha hata GB 5 si mngemfyatukia risasi kila anayewakosoa, dunia wanahama kuzalisha na megawatts wanapigana kuzalisha ma gigawatts, sisi bado tunapongezana na ma mb, ukija kumaliza mradi tutakuta tayari Tanzania matumizi ya umeme yameongezeka na hautoshi tena, ili mradi wapoteze tu ile kodi ya kichwa ya elfu 20 tunayolipa kwa nkuu wa mkoa
 
Uzuri wa huyu mwandishi anakuachia ujibu mwenyewe alafu he's like Mimi "Simo",au "sijasema"

7bu tutakuwa tushapita ukomo huo.

Matokeo ndio haya maugomvi ya Nssf nk
We in a deep shit.
Mkuu,kwanza nakupa hongera kwa kugundua hiyo akili aliyotumia mwandishi, akili ambayo hata mimi nimeiona.

Kwa kifupi,kaepuka kuitwa mchochezi na kwahiyo kaacha kila mtu afanye hasabu alafu apate jibu mwenyewe.

Wacha tuone tunakoelekea.
 
Tufunge mkanda ndg zangu watanzania... tupo katika safari ya kuelekea Uchumi wa kati...! mataifa mengi haya pendi kutuona tukielekea huko hata wakenya hawa pendi hahahahahaaa.

hasa baada ya kutamka tuna pesa... tuna jenga kwa pesa zetu wenyewe... wana tuonea wivu sana.

hivi karibuni tutaacha matumizi ya haya maneno tuna... kwa pesa zetu wenyewe
 
Kama hesabu yangu iko sahihi, naona ni kama tutakuwa tumebakiza trilioni moja tu kabla ya kufikia ukomo wa kukopa iwapo tutaenda hivi tunavyoenda(tutaamua kuikamilisha yote) unless tunajitaahidI kulipa haya madeni na hii miradi tukaendanayo taratibu(kwa hatua) hasa huo wa SGR.
Yaani hao wachambuzi ni vichekesho kweli. Wameiangalia hii miradi kama tunachonga kinyago cha panya ili tuwe na fahari ya kukitazama. Hawasemu kuhusu hiyo miradi namna itakavyochochea uchumi na kupunguza gharama za ufanyaji biashara na uzalishaji viwandani hivyo kukuza pato la taifa
 
Tufunge mkanda ndg zangu watanzania... tupo katika safari ya kuelekea Uchumi wa kati...! mataifa mengi haya pendi kutuona tukielekea huko hata wakenya hawa pendi hahahahahaaa...

hasa baada ya kutamka tuna pesa... tuna jenga kwa pesa zetu wenyewe... wana tuonea wivu sana...

hivi karibuni tutaacha matumizi ya haya maneno tuna... kwa pesa zetu wenyewe
Kama hayo mataifa hayapendi na hayawezi kutuzuia tuhofu nini
 
Yaani hao wachambuzi ni vichekesho kweli. Wameiangalia hii miradi kama tunachonga kinyago cha panya ili tuwe na fahari ya kukitazama. Hawasemu kuhusu hiyo miradi namna itakavyochochea uchumi na kupunguza gharama za ufanyaji biashara na uzalishaji viwandani hivyo kukuza pato la taifa
Hawasemu=Hawasemi
 
Hata hivyo, hesabu ya Nape kuwa Stiegler’s Gorge ingegharimu Shi11 Trilioni haipo sawa, kwani wakati wa utiliaji saini kati ya Tanesco na Arab Contractors, Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, alisema kuwa mradi gharama yake jumla ni Sh8 Trilioni.
Mradi wa Umeme Rufiji ni Trillion 6.558 alafu sijasikia sehemu yeyote kuwa pesa hizo zimekopwa hivyo ni vema kwanza ukathibitishia kuwa hiyo hela imekopwa! Ujenzi wa Reli toka Dar-Dodoma hakuna mkopo ila phase 3 ina mkopo toka Stabdard Chatted
 
Mwandishi amesahau kuwa hiyo miradi ina awamu.

Haifanyiki yote siku moja wala haikopwi yote siku moja
Wewe mama acha unafiki, hata kama haifanywi ka wakati mmoja lazima mikopo yake ni long term, namaanisha labda miaka 20 na kuendelea, kwa hiyo lazima nasema lazima kutakuwa na wakati mikopo yote inalipika kwa wakati mmoja, mkopo mmoja unn miaka miwill mwingine minne, mwiangine sita, hiyo hela unayo, na nasema usijida ganye, kama gari, gari la milioni 500 service yake sii chini ya milioni tano, hata ufanye nini , kwani ughali wake wa gari ni vyombo vilivyomo, usitegemee utajenga stieglers gorge isiwe na gharama za matengenezo, cheat yourself, gharama za matengenezo zitakuwa sambamba na ughali wa mradi, uwezo huu tunao wanasiasa hawakuambii yote hayo, wao wakati huo wameshachukua chao wamesepa, wanafichama nyuma ya katiba
 
Mradi wa Umeme Rufiji ni Trillion 6.558 alafu sijasikia sehemu yeyote kuwa pesa hizo zimekopwa hivyo ni vema kwanza ukathibitishia kuwa hiyo hela imekopwa! Ujenzi wa Reli toka Dar-Dodoma hakuna mkopo ila phase 3 ina mkopo toka Stabdard Chatted
Tayari el sewedy jusi wamekopa usd 500 million kuanza huu mradi, unless serikali ya egypt huko mbele watakusamehe, angekuwa mzungu ningekuwa na uhakika , deni liko pale pale acheni uongo
 
Back
Top Bottom