Tukianza kupongezana hivi tutaharibu

Lordita

Member
May 11, 2017
16
16
Ukweli ni kuwa Tz ni kati ya nchi zinazoibiwa raslimali zake si kwa kulazimishwa bali kwa maslahi ya viongozi wa afrika wakiwemo watanzania.

Raslimali zimeibiwa mno chini ya uongozi wa ccm japo hoja ya sasa utaambiwa aliyesababisha si hoja kubwa kitu ambacho sio sahihi.

Jambo zuri au baya ni aliyeasisi wizi huu ndie huyohuyo anaetwaminisha anataka kukuukomesha, inaweza ikawa kweli japo utaratibu uliotumika kusimika wizi huu ndo utaratibu unaotumika kupambana na wizi kitu ambacho kinatengeza wigo finyu wa kupambana na dhuruma hii.

Rais kuthubutu kupambana na wizi huuu hilo ni moja ila namna na wigo wa kukomesha wizi huu ni jambo la pili ambalo ni mhimu sana. Hivyo utaratibu huu wa kuwapuuza watu fulani kisa kwa lengo la kuwakejeli au kutokubali juhudi zao za mda mrefu ni tatizo katika vita hii. Wapinzani waliotetea maslahi haya zaidi ya miaka kumi ni vizuri serikali ikawatumia badala ya kuwakejeli.

Rais ameanzisha vita ambayo inapaswa kutengeneza msingi na ukuta wa kulinda mslahi ya watanzania katika raslimali hizi. Hivyo sio vizuri taifa zima kujadili hili kwa ushabiki tu kwani ushabiki huohuo ndo uliotumika kutengeneza na kupisha sheria hizi ambazo hata wale waliozishangilia wakati huo leo wanakiri ni mbovu. Hoja kubwa hapa watu walioko karibu na watawala hawajawahi kuwa wakweli bali kujikomba na hata ccm haina uwezo wa kuisimamia serikali kwa maslahi mapana.

Si jambo la mhimu kuanza kupongezana mda huu kwani ni mapema sana badala yake twendelee kujadili na kuongeza wigo wa mijadala namna ya kuhakikisha tunaweka ukuta thabiti ili kulinda raslimali zetu wakati wote hata kama mtu fulani hayupo. Rais abaki kama nguzo kuu ila asituwekee mipaka ya kupambana na hili kwani mipaka yake inweza acha maslahi fulani nje.

ccm wangekuwa wangwana walipaswa kuanza kwa kuomba msamaha kwa watanzania hata kabla ya kuanza kuzongazonga hizi juhudi, wao ndo waasisi kwa kila kitu katika hili.

Upinzani wasipinge kila kitu katika hili bali wazidi kutoa ushauri wa namna yoyote iwe sheria au uchumi kwa lengo la kuimalisha ukuta wa kulinda raslimali zetu na namna ya kufaidika na hiki ambacho kimepotea tayari. Kama kweli ACACIA wamekiri kupitia executive chairman wao basi tusiishie kupata kidogo bali wapinzani waangalie namna ya kuishauli serikali ili tufaidike zaidi.

SHIDA NI KUWA TUNAHUBILI TUSICHOKIAMINI.
 
Endeleeni kupongezana tu
na mpeane na tuzo na nishani
msimsahau na babu wa Loliondo
 
Back
Top Bottom